Kauli ya First Lady wa Dk. Slaa, Josephine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya First Lady wa Dk. Slaa, Josephine

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Binti Maria, Sep 8, 2010.

 1. B

  Binti Maria Senior Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Josephine Mushumbusi, amezungumza kupitia Mwanasheria Mkuu wa Chadema, ambaye pia ni wakili wa Dk Willibrod Slaa, Tundu Lissu, akaviambia vyombo vya habari kuhusu tuhuma zinazowakabili yeye na Dk. Slaa kuwa kwa mara nyingine, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimerejesha mfumo wa uchaguzi unaobadilishwa kuwa mfumo ya kijinga (a silly season). Akasema kwamba CCM wamekuwa wakikishambulia Chadema kuwa ni chama Wachagga; kwamba baadhi ya viongozi wake ndio walimuua Chacha Wangwe; na kwamba Dk Slaa ametumwa na kanisa Katoliki kugombea urais; lakini baada ya kuona hadithi hizo zimepuuzwa, sasa wameibuka na suala jipya na "ndoa za Dk. Slaa" wakidhani zitawasaidia kugeuza macho ya umma kutoka kwenye masuala muhimu ya wakati huu.

  Akasema CCM hawataki Dk. Slaa na Chadema wajadili wizi, ubadhirifu wa fedha na mali za umma; hawataki wajadili wizi wa Sh. bilioni 772 zilizoibwa katika mwaka 2008/9 tu, kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali; hawataki Chadema itaje majina ya wezi wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT); hataki Chadema wajadili jinsi JK na rafiki zake, akina Edward Lowasaa, Nazir Karamagi, Andrew Chenge na Rostam Azizi walivyofilisi taifa hili; hawataki Chadema ijadili madai halali ya wafanyakazi wa Tanzania na ahadi za ‘maisha bora kwa kila Mtanzania.' CCM hawataki Chadema kijadili sera mbadala ambazo zinalenga kuwakomboa Watanzania kutoka lindi la umaskini.

  Wanataka kulielekeza taifa zima katika kujadili masuala ya ‘chumbani' kwa Dk. Slaa; analala na nani, ana wake wangapi, kawapata wapi na kadhalika; ili kwa kufanya hivyo mgombea wao awarubuni wananchi kwa ziara mikoani na ahadi kemkem zisizotekelezeka.

  Tundu Lissu amesisitiza kuwa kila wanapoona wamebanwa, CCM huwa wanabuni njama za kukomoa washindani wao, kama walivyofanya huko nyuma. Alitoa mifano ya kilichotokea miaka ya 1995 na 2005.

  Mwaka 1995
  : Kwa kumwogopa Mrema aliyekuwa tishio kwa CCM, walimtumia mwanamke mmoja, aitwaye Angelina, wakidai ni kimada aliyezaa na Mrema; akawa analala getini kwa Mrema, Masaki, Dar es Salaam. Wakamdhalilisha. Baada ya uchaguzi, Mrema akashindwa, na suala la Angelina halikujadiliwa tena.

  Mwaka 2005 tishio la CCM ilikuwa Chama cha Wananchi (CUF), hasa Zanzibar. CCM wakamtumia Inspekta Jenerali wa Polisi, Omar Mahita, siku chache kabla ya uchaguzi, kudai kuwa amekamata lori lenye mapanga, majambia, visu na silaha nyingine zenye nembo ya CUF. Wakakipaka chama matope. Baada ya uchaguzi, hatukuelezwa lolote kuhusu visu hivyo.

  Mwaka huo huo, katika uchaguzi wa ndani ya chama, baada ya kundi la JK kuona limezidiwa mno, likaamua kumzushia Dk. Salim Ahmed Salim likidai ni Mwarabu, na muuaji wa Rais Abeid Amani Karume. Wakamhujumu, Na baada ya uchaguzi hawakuzungumzia tena uarabu wa Dk. Salim.

  Mwaka 2010: Tishio la CCM ni Chadema na Dk. Slaa. Baada ya kuona upepo unawaendea vibaya, CCM wameamua kufanya siasa za mtaro wa maji taka; hizi wanazotumia watu kumwandama Dk Slaa.

  Tundu Lissu alisema kuwa Chadema hawako tayari kufanya siasa za majitaka; na kwamba Watanzania hawako katika kujadili mambo hayo, kama hali ya afya za wagombea, ambao baadhi wanadaiwa kuwa na virusi vya ukimwi kiasi cha kubadili damu kila baada ya miezi, na kwamba kwa sababu ya unyonge huo, baadhi yao waanguka mara kadhaa jukwaani.

  Akasema wao hawatazungumzia baadhi ya wagombea urais wana wake wangapi, mahawara wangapi, na wamewaweka katika ofisi gani za umma, wapi wamepewa mikataba minono ya fedha kwa upendeleo, na kadhalika. Akasisitiza kwamba Chadema haitajibu uchafu unaosambazwa na vyombo vya habari, lakini akasema, "sauti yetu itasikika iwapo wataenda mahakamani."
  Akasema Chadema itazungumzia umaskini wa Watanzania na namna ya kuupunguza au kuuondoa; jinsi Tanzania ilivyo nchi ya tatu katika Afrika lakini wanakijiji wanalazimishwa kujenga shule za kata huku serikali ikifuja mabilioni ya pesa (kama hizo bilioni 772/- zilizotafunwa ndani ya mwaka mmoja.

  Akasema Chadema itajadili malipo ya anasa kwa mawaziri, maisha duni ya polisi, walimu, wauguzi na makundi mengine yanayonyonywa katika jamii. Akasema Chadema itajadili jinsi ya kuboresha afya za wananchi.


  Akasema, "hatutaki siasa za chumbani, bali za hadharani."

  Kwanini wamshambulie Dk Slaa? Kwa sababu ni Dk. Slaa.

  - Ana rekodi ya kuwashinda CCM mara tatu, kwa miaka 15 mfululizo
  - Amekuwa sauti kuu ya wananchi Bungeni, inayotetea masilahi ya umma
  - Kuliko kiongozi yeyote aliyewahi kuwapo Tanzania ndani ya miaka 50, ni Dk Slaa pekee aliyetaja hadharani mafisadi 11 bla woga wowote. Walioathirika kwa ujasiri wake ndio hao wanaomsakama sasa kwa mambo ya chumbani badala ya mambo ya hadharani.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huh...
  Mama yake na mama!..Akuanzae mmalize!..Mababu walisema "if you are living in a glass house dont throw stones"!
  Leo nayaona live!

  Mambo yanaanzia hapa sasa!
  Hawa sisiem wakisemewa mambo yao hawa, hapa hapatakalika!
  Lakini wao wameanza, then sisi tutamaliza!....Ngoja waendeleze mambo ya chumbani waone moto...shiit!
   
 3. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,749
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Mimi simo!
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  josephine amesemaje sasa kuhusu tuhuma hizi

  sijaona katika taarifa hii
   
 5. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Duh, CCM sijui hapa nako watasema wametukanwa!
   
 6. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Hivi kweli Chama Cha Mafisadi nacho kinaweza nyooshea mtu kidole kwa ajili ya ufisadi?!!! Haya weee!
   
 7. Charles Mtekateka

  Charles Mtekateka Verified User

  #7
  Sep 8, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 310
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Haya nayo mazito!
   
 8. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tujadili Mambo y msingi kwa mustakabali wa Taifa...Safi sana ...!na ni Bora walivyoenda mahakamani...!!Kwisha kabisa...!
   
 9. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Makamba aliambiwa aseme sababu za kufukuzwa ualimu, hajafanya hivyo..., Kikwete, Mkapa, Lowasa na Rostam walitajwa kuhusika na EPA, hawajajibu,... wakasema wametukanwa, je, hili nalo watajibu??
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Edson,
  Soma sentensi ya kwanza..........''Josephine Mushumbusi, amezungumza kupitia Mwanasheria Mkuu wa Chadema...''
   
 11. T

  Tata JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa gazeti la Mwanahalisi la leo tarehe 8/9/2010, "Josephine anakiri kuwa alikuwa ameoana na Mahimbo lakini hawako pamoja kwa miaka mitatu sasa. Amesema kwa ufupi, kwa njia ya simu kutoka Singida, kuwa kama wewe ni mwanamme na unakaa miaka mitatu bila kumuona mkeo, na katika kipindi chote hicho huchukui hatua, basi wewe una matatizo".
   
 12. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hapa ndipo tulipokuwa tunasema mkuu, sasa kumekucha na makucha yake.

  Sasa sijui wataenda kortini? Navuta bakuli la popu koni...... movie ndo hilooo!!!
   
 13. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  JF IN ACTION!

  Fighting from Strategic Angle at the background!

  Big up guys, keep it up!
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sometimes the silence can be too loud,, and that is what josephine is doing

  she is not stupid
   
 15. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Aiiiiiii... kichwa kinauma sana panado wakuuu!!!
   
 16. K

  KABAZI JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 19, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Khaa hii kali "Ukijua kupiga ujue na kukinga"
   
 17. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ebu CCM pamoja na wengine angalieni hizi siasa zinapelekwa sehemu ambapo hazitatoka. Kutafikia hatua ya kulazimishana kupima afya za wabunge wote pamoja na wagombea urais. NEC mpo, tendwa unasemaje tunakoelekea si kuzuri
   
 18. S

  Seekype Member

  #18
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi naona mama kikwete naye amtetee mumewe na CCM sijui angesemaje?...

  I really wonder
   
 19. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #19
  Sep 8, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  :confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2: No comment.
   
 20. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mimi nina wasi wasi na huyu Josephine, hajatumwa kweli na CCM kumwangamiza Dr. Slaa maana jibu lake nimeona limekuwa rahisi mno. Eti 'kutokuonana na mumewe kwa miaka mitatu basi ndio kibari cha yeye kuolewa" huyu dada sidhani kama kweli, hayo ni maoni yangu tu na si ya mtu mwingine, maana huyo mumewe anadai mpaka march mwaka huu walikuwa pamoja na ndipo alipoanza kuonesha hali ya kutokuwa mwaminifu. Hivyo kama kutoonana ni kuanzia april mwaka huu.
  Dr. Slaa akipata pingamizi lolote kwa kugombea urais wa kubebeshwa lawama ni hawa wawili ndugu zangu watanzania, Josephine na huyu anayejiita mumewe.
   
Loading...