Kauli ya Abbas Kandoro dhidi ya DC aliye acha kazi Kimolo

..Kandoro amethibitisha aina ya Viongozi Vibuyu-Wazi tulionao. Alichotakiwa kufanya ni kumtakia tu DC maisha mema huko aendako, basi. Tusimlaumu sana. Pamoja na kuwa wanasi-hasa, Viongozi wetu pia wamebobea kwenye fani ya Mipasho...!:loco:
 
Na mimi nimemsikia Kandoro na niseme tu Kandoro amefanya kosa kubwa sana kuanza malumbano kupitia vyombo vya habari. DC ameachia ngazi kwa hiari yake mwenyewe na hakuna mahali popote aliposema kuwa anaondoka kwa sababu jina lake halipo kwenye orodha ijayo ya wakuu wa Wilaya!

Kama Kandoro angekuwa na chembe ya busara basi angemtakia huyo DC mapumziko mema, lakini kitendo cha kumchafua DC ni sawa na kutibua nyongo na sitoshangaa huyo DC akaamua kumwaga ugali!
MAANDIKO KATIKA KITABU KITAKATIFU YANASEMA "Kila mtu awe mwepesi wa kusikia lakini sio mwepesi wa kusema"
 
Mkuu naomba nikukosoe!! umekosea sana!

Serikali haiumwi degedege..!!

Ina kipindupindu!! yaani inaharisha!

pengine inaugua pepopunda na dondakoo. Kazi kweli kweli. Serikali ya Kimagamba! Baadaye tutamsikia mwehu mwingine akimwaga mapovu mengine kuhusu swala hili hili la Dc Kimolo.
 
Kandoro ni gamba! Arudishe lile shangingi la million 250 alilonunua kwa millioni mbili.

lile gari hajalinunua, taarifa zilizozagaa hapa JF, zilisaidia kuliokoa. hadi leo ukienda parking y magari ya mkuu wa mkoa wa mwanza utalikuta toyota vx lipo. na hutumika maalumu kwa misafara ya mawaziri wanaotembelea mwanza
 
Too low for an Rc. Kakurupuka kutoa tamko, angemuachia jukumu hilo mteuzi wao ( yy Kandoro na Kimolo)
 
ni heri hata angesema ni mbadhirifu japo lazima ufafanuz uwepo
 
Huyu naye ni kiongozi au kiungozi,I think his thinking and reasoning capacity has ceased.
 
Namshangaa Kandoro. DC ktk maelezo yake hajamtaja popote. DC alilia na waziri juu ya kahawa.sasa kiherehere kimetoka wapi kandoro?
 
Hivi Wasambaa na Wakwere wanatofautiana sana? Niliwahi kuwa na Boss wa Kisambaa akimshughulikia mtu kinidhamu anakuwa anapitapita kwenye ofisi za watu kuwauma sikio. Utasikia anajisemea tayari kimemwakia! Inawezekana na huyu Mkwe.re yuko hivyo, kabla hajafanya lolote taarifa ziko kwenye gahawa!
 
Msimtukane baba mkwe wangu nimemmega sana mwanae wakati tunasoma Jitegemee 2007-2009.
Kwahiyo kama mtu aliwahi kummega mama yako aje kujitangazia hapa kama ni babako wa kambo?angalia wasije wakajitokeza baba zako wa kambo wengi humu!!!!ujaribu kuchangia vitu vinavyohusiana
 
...tutajuaje kama naye atapewa kazi nyingone ya kuwa mgeni cDm, na kuiharibu kabisa ikiwezekana.
 
Kimolo amemruka Kandoro taarifa ya habari TBC, what a shame kwa mkuu wa mkoa kujadili mambo yasiyosaidia maendeleo
 
Huyu Kandoro ni tatizo sana. Mbona hoja zake huwa hazina msingi? Huyo DC ni wa kupongezwa sana.

Huyo DC aliyejiuzulu sio kilaza; Gabriel Kimolo ni msomi mzuri kuliko huyo Kandoro na nadhani amesoma alama za nyakati na punde mtamsikia akiunguruma huko anakostahili!!
 
salam wana JF. nimemsikiliza RC kandoro akitoa maelezo dhidi ya hatua ya DC aliyeamua kuacha kazi kuwa amefanya hivyo kwa sababu anajua/ameambiwa kuwa hayupo katika orodha mpya. hivi huwa taarifa zinafika kwa wahusika kama wanateuliwa ? kwa mtazamo wangu,mimi naona Kandoro ameonyesha udhaifu kuonyesha kuwa ukiteuliwa unajua kabla, au kaonyesha ni jinsi gani siri zinavyotolewa na watumishi wa serikali. karibu utoe maoni yako

Kandoro ni Fisadi na nina imani ana mkono wake kwenye hili sakata la DC kujiuzulu .ukiangalia historia yake kila mkoa anakopelekwa huwa ni mzee wa migogoro na kule mwanza alikwapua land cruiser VX V8 aliyokuwa akitumia kama mkuu wa mkoa kwa bei ya shilingi milioni mbili tu.
Watu walipokomalia hadi humu JF ndio alirudisha na kuhamishiwa huko aliko.
Na hata alipokuwa Dsm ilikuwa migogoro tu.
Sasa anatwambia kwamba tayari ana orodha ya ma DC watakaoteuliwa na rais je ina maana yeye na rais wako karibu kiasi gani? Na kama ni hivyo mbona hakumpa uwaziri ili amsaidie kazi vizuri? Mimi nina imani kuwa kandoro naye ni MUST go KWA SABABU TAYARI NI GAMBA!
 
Kwenye news tbc usiku huu kandoro kasema kua ni dc ndie aliemjuza kua yeye dc kaambiwa kua kwenye list hayumo.
 
Hivi Wasambaa na Wakwere wanatofautiana sana? Niliwahi kuwa na Boss wa Kisambaa akimshughulikia mtu kinidhamu anakuwa anapitapita kwenye ofisi za watu kuwauma sikio. Utasikia anajisemea tayari kimemwakia! Inawezekana na huyu Mkwe.re yuko hivyo, kabla hajafanya lolote taarifa ziko kwenye gahawa!

.....Chijana, Tafazai sana Tiheshimiene! Boss wako sio Balozi wa Wasambaa wote...!!
 
Back
Top Bottom