Katuni ya Masoud Kipanya ina maana gani?

Katuni ya Masoud Kipanya ina maana gani?

Anataka wamfutie usajiri?. Sisi WaTz bado sana. Ni underdog tu kwa serikali. Bado tu wafu
 
Sasa mbona wamemfunga mnyororo ina maana tawi likikatika watamdaka?

ukiangalia vizuri wanaenda wote, usisahau overweight ya upande wa kulia ni lazima mti wote uende …
 
wasaidizi wake chini ya wasiojulikana wanafikiri wanajenga, kumbe wanamuangusha na mwisho wa yote kumbe na wao wanaenda kuanguka.
 
Ninavyoona ni kama watadondoka wote kwasababu mwenye kilemba chekundu ni mzito kuliko aliyevaa mask.
Kuna sehemu nimekutana na ki-picha hiki, eti "ABDUL" anatengeneza anguko la "MAMA YAKE", na anguko lake mwenyewe!
 
Tafakuri

- Kinyago cheusi ni watu wasiojulikana

- kukata kwa msumeno ni mambo mabaya ya utekaji na manyanyaso yanayoendelea

- Kukata katikati ya mguu wake maana yake ata mti ukidondoka uyo mtu yeye bado ana nafasi ya kujiokoa ila uyo mama apo lazima adondoke.

- Mnyororo maana yake hao wasiojulikana wanaongozwa au wanaamrishwa na uyo mama
 
Mwanzoni nilidhan anayekata tawi (mwenye kijamii) anaakili. Anataka kukata then aondoe mguu mmoja huku alipokata ili amuache huyo mama akidondoka mwenyewe. Cha ajabu naye amejifunga mnyororo. Hiyo wanakwenda wote. İnnalilahi
[emoji23][emoji23]
 
Kwa nilivyoelewa Inamaanisha ukivaa mask upande juu ya mti na msumeno ukate matawi
 
1. Yule mtu anayekata Mti huku amejifunika Usoni = Wasiojurikana.
2. Amevaa Sweta la Kijani sio Kwa bahati mbaya, means Wasiojurikana ni miongoni mwa Wana CCM.
3.Mwanamama amesimama kwenye Tawi la Mti linalokatwa, ameangalia Upande mwingine, na Mtu anayekata Tawi ametizama upande mwingine, ukiangalia Picha inaonyesha Mama hajui kama Tawi la Mti linakatwa, na Tawi likikatika wote wataanguka Shimoni Kwa sababu wamefungwa na Cheni Moja.
 
Mkataji anao uwezekano wa kupona lakini huyo mama ndio basi tena. Elewa neno basi tena
 
Back
Top Bottom