Katoliki ni zaidi ya uijuavyo!

Katoliki ni zaidi ya uijuavyo!

yeya alikuw ana uhumihu gani wa kujiuliza km sio kutaka shawishi wananchi wajinga hivyo?Mbona hakusema wangeulizwa watz wengi wangesema nini?Acha porojo mkuu. mawazo ya mkubwa ni amri kwa wafuasi wake na wengin. Ngoja siku rais akuambie naomba mke wako halafu uniambie ni kuomba.
Du!
 
Ndilo dhehebu pekee ambalo ni dola kamili km lilivyo dola la Tz na mengineyo hapa duniani!

Ndilo dhehebu pekee lenye mfumo imara wa ukusanyaji taarifa zihusuzo dhehebu lao na madhehebu mengine!

Ndilo dhehebu pekee hapa duniani lenye ushawishi usiomithiliwa na jengine!

Ndilo dhehebu pekee lenye mfumo imara wa kiinterijensia na uigwao na mataifa mengi hapa duniani!

Ndilo dhehebu pekee viongozi wao wakuu wakihitaji kuongea na mkuu wa dola wa nchi husika kwa mda wautakao wao-huweza!

Ndilo dhehebu pekee lenye idadi kubwa ya wafuasi kuliko dhehebu lolote hapa duniani!

Kifupi,Katoliki ni zaidi ya dini!

Wewe ni mwongo na unashabikia usichokijua. Ulichokiandika hapa hakina tofauti na masimulizi ya Alfu-Lela Ulela.

Mosi, Ukatoliki siyo dhehebu pekee ambalo ni dola kamili. Kuna madola ya Kiislamu kama Saudi Arabia (Dola la Waislamu wa kisuni) na Iran (Dola la Waislamu wa kishia). Haya yote ni madola ya kidini yaliyonganishwa na uongozi wa kisiasa. Tofauti yao kidogo ni kwamba Serikali Kuu ya kanisa la Katoliki (The Holy See) ni mtu kisheria (Legal Personality) kwamba inaweza kusaini mikataba ya kimataifa na nchi nyingine bila kuihusisha Nchi ya Vatican. Mfano Mkataba wa Lateran wa mwaka 1929 wa kuanzisha nchi ya Vatican ulisainiwa baina ya Serikali ya Kanisa la Katoliki (The Holy See) na Nchi ya Italy.

Pili, Kanisa katoliki lina nguvu na linakusanya sana taarifa kuhusu raia wake na dunia nzima lakini ukweli ni kwamba Wakatoliki wanaweza wasiwe wa kwanza kwenye upelelezi japo wana nguvu kubwa sanaaaa. Hakuna dini na dhehebu lenye nguvu ya kepenyeza dini na madhehebu mengine kama WAYAHUDI (Nasema haipo na haitakuja tokea) Kinacholibeba kanisa la Katoliki ni uwepo wa Idadi kubwa ya Waumini duniani kote. Wapo waumini Bilioni moja na ushee, wapo karibia katika kila Bara na nchi, na kibaya zaidi ni kwamba kanisa lina Wasomi na watu wakubwa wenye ushawishi kutoka karibia kila Serikali hapa duniani.

Hapa naongelea watu wasomi na wenye ushawishi kama Mwalimj Nyerere, Raisi Mkapa, Raisi Mugabe, Raisi JF Kennedy, Raisi Joe Bidden, Raisi Nicolas Sarkozy na wengine wengi ni wakatoliki sugu na wana utii kwa Kanisa hivyo wakatoliki kwa aina hii ya watu ni lazima watakuwa mbele tu katika mambo mengi.

Lakini ukweli mchungu ni kwamba Wayahudi ni kakundi kadogo sana lakini shughuli yao dunia nzima tunaijua. Mfano mzuri tu Wamepenyeza na wamepunguza nguvu ya Uprotestanti huko Marekani haijapata tokea tangu Marekani ipate uhuru. Mwaka 1962 Myahudi Steven Engels alipewa ushindi na Mahakama ya Juu ya Marekani kuzuia kabisa wanafunzi kufanya maombi shuleni. Leo hii za media za Wayahudi huko Marekani zimefanikiwa sana kueneza Propaganda za Ndoa za Jinsia Moja hadi kupelekea kuruhusiwa kitu ambacho Waanglikani wa Wakatoliki wa Ulaya walishindwa kukfanya kabisa. Nguvu ya mashirika yao kama Anti-Defamation League na AIPAC siyo ya kawaida nchini Marekani. Ubaya zaidi ni kwamba Vyombo vyao vya habari na burudani vinaeneza Propaganda chafu na za kibaguzi dunia nzima.

Wakatoliki na Ujanja wao wote walishindwa kabisa kuiangusha nguvu ya Kanisa la Orthodox la Ulaya Mashariki chini ya Ufalme wa Urusi. Hii ilipelekea Wakatoliki kujaribu kuwavuta warusi lakini kila walipojaribu kutuma mapadri na majesuit walikuta wanauawa, hadi waliposhindwa kabisa wakaamua kumtungia Propaganda za Uongo Mfalme wa Urusi na kuunza kumuita Ivan The Terrible kwamba ni muuaji sana.

Wakati wa Vita za Kidini (Crusades) kule Mashariki ya kati mnamo karne ya 11 na 12, Papa Urban alijaribu kuwavuta Warusi wajiunge na wenzao wa Uingereza, Hispania,Italia na Ufaranaa lakini ilishindikana na walijaribu fitna zote wakashindwa. Lakini mwaka 1917 kakundi kadogo kabisa kakiongozwa na Myahudi Vladmir Lenin na wenzake walifanya kitu ambacho hakuna taifa liliwahi kuweza. Walipindua Ufalme wa Urusi na Kuvunja mgongo wa Kanisa la Orthodox ambapo limeanza kurudi Kwenye ushawishi miaka ya 1990 baada ya Ukomunisti kufa na Urusi ya Kisovyeti kuanguka (Pitia tena historia)

Mwaka 1919 Wayahudi waliweza Kuharibu kabisa Dola la Kiislamu la Uturuki (Ottoman Empire) na kuligawa vipande vipande chini ya Mkataba wa siri wa Sykes-Pikot wa 1916 na kuyafanya baadhi ya majimbo yake kama Palestina yawe chini ya Ufalme wa Uingereza. Kumbuka hao Wakatoliki walishindwa kabisa kpigana na Waturuki kwa miaka mingi na kuna kipindi ilibakia kidogo tu wasingekuwepo leo hii kama tu Waturuki wangefanikiwa kuipiga Italia mwaka 1480.

Tatu, hujatutajia nchi ambazo zimeiga huo mfumo imara wa Kanisa la Kikatoliki. Ili kufanya hoja yako iwe na uzito ni vema ukaweka na ushahidi wa hayo madai yako.

Nne, Kuhusu kuongea na viongozi wa nchi kwa muda watakao hicho ni kitu cha kawaida sana kwasababu Kanisa la katoliki mbali na kuendesha shughuli za kidini pia linaendesha Shughuli za Kijamii,kisiasa na kiuchumi. Hivyo kupitia mashirika yao mengi ya kanisa kama CARITAS FOUNDATION, JESUIT FATHERS, CONSOLATA na mengineyo wamekuwa wabia wakubwa wa maendeleo kwenye nchi nyingi duniani, hivyo basi kama ambavyo Raisi Kenyatta anaweza kuongea na wawekezaji kuhusu Elimu vivyo hivyo ataongea na Wakatoliki kuhusu Elimu kwa muda wanaotaka kwasababu tu ya mchango wao kwenye Uchumi wa nchi husika na mara nyingine inaweza isiwe sababu ya dini mfano kwenye nchi za Kiislamu hawawezi kabisa kucheza karata ya dini bali karata ya Siasa au Uchumi.

Upande wa pili wa Shilingi kwenye nchi za Kiislamu au Kihindu viongozi wa dini wanaweza kuongea na viongozi wa nchi muda wowote watakao kwasababu wao ni wadau wakubwa wa maendeleo ya nchi husika. Hebu jiulize leo ni kiongozi gani wa nchi anaweza kukataa kufanya mazungumzo na Sheikh Mkuu wa Waislamu hapa Duniani Ahmed Muhammed Ahmed El-Tayeb (The Grand Imam of Al-Hazar) ?? Hasahasa ukiangalia mchango wa dhehebu la Wasuni kwenye uchumi wa nchi mbali hapa duniani ???

Kibaya zaidi umesahau nchi kama Marekani viongozi wa Kilokole kama Marehemu Mchungaji Billy Graham walikuwa wanaenda hadi Ikulu kufanya maombi na kuhudhuria vikao vya Baraza la Mawaziri tena kibaya zaidi mwaka huu Raisi Donald Trump amefululiza kutembelewa na wachungaji wakubwa kama Dr.Franklin Jentezen na Dr.Robert Morris ambao wamechaguliwa kuwa moja kati ya washauri wa karibu wa Raisi Trump hivyo huzungumza na viongozi muda wowote watakao.

NB: Wakatoliki ni dhehebu kubwa sana duniani lenye ushawishi mkubwa mno, lakini Serikali yake bado kuna sehemu huo ushawishi wao hauwezi kufanya kazi kirahisi au kufanikiwa hata kidogo. Kama nguvu hizo wanazo (Omnipotent) nakuhakikishia dunia yetu ingekuwa haina maendeleo kabisa kwasababu Kanisa la Roma lilivyoshika dunia tokea Karne ya 4 hadi ya 17 kulikuwa na kipindi kigumu chenye mateso kwa binadamu haijawahi tokea. (The Dark Ages)

Walificha Biblia na walikataa mtu asifikirie kabisa kwa kumnyima elimu kwa maksudi. Wanasayansi walioamua kufikiria nje ya boksi kama Galileo Galilei waliuawa na kanisa kisa tu kusema dunia yetu ni Mviringo.

Kanisa lilitawala Ulaya yote kimabavu lakini mwishoni likashindwa kuendeleza hiyo nguvu na mambo yakaliyokea puani. Upande wa pili pamoja na nguvu zao zote walishindwa kabisa kushinda vita za kidini dhidi ya Waislamu kule Yerusalem mnamo karne ya 12 ambapo walitamani sana Vatican ingekuwa Yerusalemu.

Mwaka 1648 (Peace of Westphalia) Kanisa na ushawishi wake lilishindwa tena kuhadaa uhuru wa mataifa na kukubali kwamba nchi zinazotaka kujitoa Rumi zitoke tu kwasababu Ulaya yote ilipigana Vita ya miaka thelathini (Thirty Years War) ya kidini kisa tu Warumi walitaka kutawala mataifa yote kidini na kimabavu.

Intelijensia Imara ya Kanisa Katoliki ilishindwa kabisa kumzuia Napoleon Bournaparte kumfunga Gerezani Papa Pius wa VII hadi mwaka 1809 hadi 1812. Hivyo wako Imara lakini lazima uje kwamba mwanadamu atabakia kuwa mwanadamu mwenye udhaifu tu.

Haya tena sasa,
Hao Wakatoliki walishindwa kabisa kuwazima Waprotestanti Chini ya Martin Luther, Walishindwa kabisa kuwazima waanglikani nchini Uingereza mwaka 1601, hebu tafuta kitabu kiitwacho (THE PROTESTANS: RADICALS WHO CHANGED THE WORLD) ndiyo utaelewa jinsi gani Wakatoliki walijaribu kuua maelfu ya Waprotestanti lakini kumbe ndiyo wanaendelea kwachochoea.

Tena walishindwa kabisa kuzima uhuru wa mawazo wa Karne ya 18 na 19 (Age of Enlightenment), japo wao hawakupenda na hawapendi binadamu awe huru kifikra kwasababu Kama watawala wengine tu hapa duniani wanadamu wanapokuwa huru sana kifikra siku zote ni lazima inawaletea sana matatizo watawala wa Kikatoliki tokea siku za Martin Luther, Niccolo Machiavelli, Adam Weishapt, Oliver Cromwell, Napoleon Bournaparte, George Washington, Voltaire, Baron Montesquieu, John Locke na Hugo Grotius.

Ushahidi wa hili hebu angalia hii ndoa ovu baina ya Serikali ya Tanzania na Kanisa Katoliki inavyoumiza na kudumaza maendeleo ya Watanzania. Watanzania tukiwa gizani maswali yatapungua na hasa yale yanayohusu maslahi ya moja kwa moja ya Kanisa la Katoliki.

Hilo la mwisho hujakosea kabisa Ukatoliki ni zaidi ya dini: Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki ametangaza wazi kabisa kuwa hataki hata kusikia Uwepo wa mabadiliko ya Katiba, Haki za Binadamu, Uhuru wa vyombo vya habari, Uwazi na Uwajibikaji wa viongozi mbele ya Ummah. Amini Amini haya atayatolea Waraka Maalum na waumini wote watatii kwa kusema “HUU NI USEMI WA MUNGU” hii haitajalisha kama wako CHADEMA, ACT, NCCR, TLP au CUF.

Teh teh teh teh....
Kwa akili kama zako mtoa mada maendeleo hapa nchini Sahau kabisa.

CC: Consigliere, Gentries
 
Katoliki hawako kidini, wao no mafia! Ila kwa sasa influence yao imebaki Africa tu zaidi na south America _ Europe na Asia wako taabani
 
Hata free masons kwenye dhehebu hili hawajiendekezi wanajua muziki wake
 
Ila hakuna dhehebu linaloitunza amani duniani kama wakatoliki
Na siku wakiamua dunia isiwe na amani dunia yote itakuwa moto kwa kuwa wako kila mahali duniani
 
Na siku Papa akiamua kutembelea korea ya kaskazini dunia itasimama
 
Hata huyo Kim utashangaa akimpigia magoti Papa na kubusu Pete yake!
Hii ni salamu kwa Papa yeyote goti ni heshima ile pete ndio salamu ya askofu ni lazima uibusu
Kama Yuda alivyombusu Yesu wakati anamsaliti ni salamu tu ya kawaida hiyo
 
Ndilo dhehebu pekee ambalo ni dola kamili km lilivyo dola la Tz na mengineyo hapa duniani!

Ndilo dhehebu pekee lenye mfumo imara wa ukusanyaji taarifa zihusuzo dhehebu lao na madhehebu mengine!

Ndilo dhehebu pekee hapa duniani lenye ushawishi usiomithiliwa na jengine!

Ndilo dhehebu pekee lenye mfumo imara wa kiinterijensia na uigwao na mataifa mengi hapa duniani!

Ndilo dhehebu pekee viongozi wao wakuu wakihitaji kuongea na mkuu wa dola wa nchi husika kwa mda wautakao wao-huweza!

Ndilo dhehebu pekee lenye idadi kubwa ya wafuasi kuliko dhehebu lolote hapa duniani!

Kifupi,Katoliki ni zaidi ya dini!
Ndilo dhehebu pekee lililobaki likiabudu sanamu kwa kulipigia magoti....
 
Umekariri porojo za sunday school, kanisa katoliki lilishiriki mauwaji ya kimbari Rwanda mwaka 1994, usisahau kuijumuisha na sifa hii ya kanisa katoliki.
Unachoshindwa kujua ni kwamba vita haiangalii sura au wewe ni nani ni kujitetea tu halafu vita ya rwanda ilikuwa ya kikabila ni vita ambayo haimwachi mtu salama
 
Wewe ni mwongo na unashabikia usichokijua. Ulichokiandika hapa hakina tofauti na masimulizi ya Alfu-Lela Ulela.

Mosi, Ukatoliki siyo dhehebu pekee ambalo ni dola kamili. Kuna madola ya Kiislamu kama Saudi Arabia (Dola la Waislamu wa kisuni) na Iran (Dola la Waislamu wa kishia). Haya yote ni madola ya kidini yaliyonganishwa na uongozi wa kisiasa. Tofauti yao kidogo ni kwamba Serikali Kuu ya kanisa la Katoliki (The Holy See) ni mtu kisheria (Legal Personality) kwamba inaweza kusaini mikataba ya kimataifa na nchi nyingine bila kuihusisha Nchi ya Vatican.

Pili, Kanisa katoliki lina nguvu na linakusanya sana taarifa kuhusu raia wake na dunia nzima lakini ukw.
Unajitekenya na kucheka!
 
ni kanisa la amani bwana, usilifanye lionekane ni kanisa la hila!!
Maana vitisho vyako ni as if siyo Janisa la Yesu aliyefundisha Rehema!
Hajafundisha rehema.....yeye mwenyewe alitaka rehema.....
 
Ndilo dhehebu pekee ambalo ni dola kamili km lilivyo dola la Tz na mengineyo hapa duniani!

Ndilo dhehebu pekee lenye mfumo imara wa ukusanyaji taarifa zihusuzo dhehebu lao na madhehebu mengine!

Ndilo dhehebu pekee hapa duniani lenye ushawishi usiomithiliwa na jengine!

Ndilo dhehebu pekee lenye mfumo imara wa kiinterijensia na uigwao na mataifa mengi hapa duniani!

Ndilo dhehebu pekee viongozi wao wakuu wakihitaji kuongea na mkuu wa dola wa nchi husika kwa mda wautakao wao-huweza!

Ndilo dhehebu pekee lenye idadi kubwa ya wafuasi kuliko dhehebu lolote hapa duniani!

Kifupi,Katoliki ni zaidi ya dini!
Taasisi kongwe kuliko zote duniani. The oldest organized organization in the world
 
Kuhudhuira ibada sio kuwa unaifahamu vizuri historia ya Katoliki. Ok, kama unawafahamu wakatoliki nijibie maswali haya saba tu.
  1. Papa wa Tatu wa kanisa katoliki aliitwa nani na alikuwa na sifa gani za kipekee/
  2. Hadi sasa kanisa katoliki lishatangaza Idadi) watakatifu wangapi katika historia yake?
  3. Ni mapapa wangapi wa kanisa katoliki ambao hawajawahi kuitwa watakatifu?
  4. kanisa katoliki lina mashirika mangapi ya kitume?
  5. Ni makadinali wangapi walishiriki kwenye mchakato wakumpata Papa wa sasa (papa Francis)
  6. Ni nchi zipi duniani ambapo papa hajawahi kuwa na balozi wake? (hakuna balozi anaemuwakilisha)
  7. mabadiliko ya hivi karibuni ya kanuni za ibada yalisababishwa au kuletwa kwa sabahu zipi?

halafu basi kwa vile umeng'ang'ania ushiriki wa kanisa kule rwanda basi tuletee hoja yako hapa. uweke na ushahidi zisiwe hisia zako potofu tu.
Hapa hajitokezi kabisa
 
Back
Top Bottom