Katika hili, namwamini Shetani

Nadhan hapa hoja hasa si kwamba mungu alidanganya bali ni kwamba story hii ya adam na eva na tunda la kati...si ya kweli. Ni ngano za kale zisizokuwa na ushahid nje ya imani. Ukiondoa imani...dhana ya kula tunda haiwezi kujisimamia..aka kujitegemea kama matter of fact.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hakika acheni Mungu aitwe Mungu.Tunakifanyia kufuru ya level hii Kitu Chenye nguvu za kutuzima Kama kibatari katikati ya upepo wa bahari lakini bado uko hai unavuta pumzi yake.Kweli Mungu anatupenda saaaana,ingekuwa ndo Mimi Nina nguvu hizo wewe nakuhakikishia sahivi ungekuwa ulishalala mautini.Hivi ukijiuliza kusema akisema apige akuue atakuwa Na hasara gani hakuna!!!lakini bado anakuach yamkini unamkashifu yeye Mungu ambaye akisema akikuwekea mkono tu unanyauka unaacha kumchafua huku unapotea kweny ramani.Unamsifia adui yake Na bado anakuachia Na pumzi yake kesho tena uamke asubuhi afu unaamka unakuja kumdhalilisha tena .Aisee acheni Mungu aitwe Mungu maana Nami Nina ya kwangu Ila ananivumilia.Hakika hakuna aliye Kama wewe Mungu wa Israel.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungezaliwa kwenye pagoda na ukawa na ma monk sidhani km ungesema haya,hizi imani ni kurithishwa kutoka na jamii ulipozaliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shetani hakuna na ukitafakari Hilo hayo maswali yako unakuwa umeyapatia majibu

Bila hivyo utaumiza kichwa chako bure na usipate majibu milele
 
Ok mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenena Vyema Mkuu
Ila shida ni moja tu umefanya hukumu jambo usilolielewa wala kulijua

Jifunze kwa mfano huu hapa
Ulipokuwa mtoto kuna mambo wazazi walikukatazia huenda ukifanya ama kujihusisha nayo uliadhibiwa kabisa na kwa uhalisia ulikuwa unaona kabisaa unaonewa na wazazi wako, lakini ulipokuwa mtu mzima ikawa ni tofauti unatambua na kuelewa yakuwa kumbe wazazi walikuwa sawa ila tofauti ni kwamba uelewa ulikuwa nao mdogo wakati ule tofauti sasa umekuwa mtu mzima.

Tuangalie Tena mfano wa pili
Ulipokuwa hujui kiingereza haswa wakati wa utotoni basi ukiona maandishi ya kiingereza ama ukiangalia filamu za kiingereza na watu wakiwa wanaozungumza basi naamini ulikuwa unaona kama madudu tu fulani nadhani kiutoto utoto ukijaribu kugeza kama unaongea kiingereza unaweza cheka zile pumba tulivyokuwa tunaigiza, lakini kwasasa umetambua na kuelewa kiingereza unashangaa kabisa sijui yale madudu ulikuwa unayatoa wapi wakati ule, ni kwamba sasa uelewa umekuwa mkubwa tofauti na zamani.

Chukua tafakri hii hapa
Unapokuwa vitani huwezi shinda vita usipojua udhaifu wa adui yako, itakuwa ni kupoteza mda tu, mfano mzuri hapo nyuma wanajeshi wetu walivamiwa huko congo wakiwa wamepumzika kambini hakuna aliyepona adui alitafuta udhaifu ambao ulipelekea ushindi wake, hata akafanikiwa kuwapoteza wanajeshi wetu RIP Makomandoo Wa TZ

Sasa nakuja kwako umeamua kwa makusudi kabisa kujipa ukomo wa fikra zako umekuwa kama mtoto aliyetoka kuangalia movie ya the hulk naye anaamini anauwezo wa the hulk kitu ambacho mtu mzima asingeweza kuamini
Kwa lugha rahisi ni kwamba upo chekechea broo umevamia elimu ya chuo kikuuu unaweza kupote kabisaaa

Kumbuka unaambiwa Biblia ni kama msitu mnene si wote waingia wanaweza kutoka salama wasipokuwa na msaada fulani,

Maswali ya kujiuliza Ulilijua Lengo la Mungu Kumuweka Adam na Eva Eden?
JIfunze kujifunza mkuu maarifa hayaji kwa kukurupika kama hivyo bali huja kwa kuweka bidii katika kuyatafuta
 
Kwani hii misiba inayotokea kila siku huioni???
 
Nimejaribu kuuelewa mfano wako mkuu mtoto kaambiwa ukiweka sukari kwenye chai ntakuchapa lakini akaja shetani akasema ukiweka sukari kwenye chai hakika chai itakuwa tamu.ni kweli mtoto baada ya kuweka sukari kwenye chai ikawa tamu lakini adhabu ya kuchapwa na mzazi inakuja kwa sabab mtoto aliambiwa akiweka sukari kwenye chai atachapwa.big up bwana big IQ kwa upande wangu nimekuelewa sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama huwaga husomi umejuaje kama anaanza na hayo maneno mkuu?[emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
rubbish

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitabu chenu kinasemaje kuhusu hii mada?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na ni kweli walipokula lile tunda hawakufa kama Mungu alivyosema, kwa hiyo tunaona Mungu alidanganya na shetani aliwaambia kweli kwani walipokula tu hilo tunda wakajua mema na mabaya.kama shetani alivyowaambia.
[emoji115]HAPO MUNGU ALIMAANISHA KUFA SIO KWA MAANA KULA TUNDA KAMA SUMU NA KUFA HAPO HAPO UKILA. YEYE ALIMAANISHA UKIMTII MAAGIZO YAKE USIFANYE KILE ALICHOKUAMBIA USIFANYE. ALIKUWA NA MAANA WANGEISHI MILELE BILA KUONJA MAUTI. ONA SASA BAADA YA KULA TUNDA KIFO KIKAINGIA DUNIANI. NA BAADA YA KUJUA MABAYA NA MEMA ONA SASA KILA AINA YA TABU IKAINGIA DUNIANI,NJAA,VITA,MAGONJWA. BILA KULA LILE TUNDA KUSINGEKUWA NA KIFIO. BILA KULA LILE TUNDA DUNIA INGEKUWA MAHALA PA FURAHA TU,BILA TABU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hayo mema na mabaya ndio yepi?
Hi scenario kwangu inatia ukakasi kupitiliza.
Ila warumi una mantiki ktk hili.
 
Mti wa kujua mema na mabaya ukila utajua mema na mabaya sio utakufa
 
Sema biblia inachanganya sana. Kwa mfano navyoelewa mimi dhambi/kosa la kwanza kabisa duniani ilikuwa/lilikuwa ni usile tunda la mtu wa katikati. Na adhabu yake kama mtu akila ilikuwa wazi kabisa kwamba ni kifo.
Kwa mujibu wa maandiko Evah/Hawa alikula na hakufa. Kisha akampa na Mumewe Adam nae akala hakufa! Sasa kituko kiko hapa, Mungu badala ya kutoa adhabu ya kifo akaibadili na kuwa hii inayotutesa sasa. Kwa Mwanamume ikawa utakuala kwa jasho. Mungu alisema hivi. Ardhi imelaaniwa, Adam utakula kwa jasho. Na wewe hawa utazaa kwa uchungu.

Hii manake nini? Maanake ni kwamba kama ingetokea Hawa asingekula tunda lile basi ikifika wakati wa kujifungua asingesikia uchungu huu wanaopata mama zetu na wake zetu wakati wanapotuzalia watoto. Wangekuwa wakijifungua huku wakiwa na matabasamu midomoni mwao huku wakipiga story na kucheka.

Yote kwa yote nabaki kuwa na imani kuwa kuna chanzo cha huu ulimwengu. Nacho ndio hiki tunachokiita MUNGU. ila haya yaliyoandikwa kwenye biblia kidogo yanatia ukakasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe Mungu wa waisrael , mimi namsubiri Mungu wa wamakonde
 
Utii??kwanini unatii?kitu alichosema shetani ni kwamba ukila tunda la mti wa kati utafahamu mema na mabaya hapo utaweza kutii ukiwa na reasons,see??!shetani alicho ki implement kwa binadamu ni ile reasoning capability.turudi kwenye mfano wa sukari na mtoto,umesema huenda baba alimkataza mtoto kwasababu labda mtoto ana kisukari,lakini jee baba alimwambia mtoto sababu ya kumkataza asiweke sukari?kwanini ali jump kwenye adhabu tuu kwamba nitakuchapa?kwanini mungu alificha kwamba ukila tunda la mti wa kati utajua mema na mabaya?je mungu hajui mema na mabaya?kama anajua mema na mabaya kwanini alimuumba mtu asiyejua mema na mabaya na alafu aseme ni mfano wao?mimi ninaamini kila mtu ana akili yake na maamuzi yanatofautiana kati ya mtu na mtu,si ajabu wewe kwa utii wako uliouonyesha hapa usingekula lile tunda,sasa mbona unazaa kwa uchungu,unatafuta kwa jasho na hakika utakufa.yanakuhusu nini hayo ewe mtiifu?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…