Waombaji/wanamaombi tuombee nchi yetu

Waombaji/wanamaombi tuombee nchi yetu

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
3,341
Reaction score
3,822
1.AMANI YA NCHI YETU
2.UMOJA WA KITAIFA
3.TUOMBE KWA AJILI YA VIONGOZI WETU
4.UCHUMI WA TAIFA
5.UTAWALA WA HAKI NA SHERIA

Chochote Mungu atakachokuongoza kuomba KWA AJILI ya NCHI yetu omba mana kikubwa zaidi amani ,mana pasipo kuwa na amani ujue Mungu hatakuwepo ambao hakuna amani,tuombe Imani idumu.
Mungu WETU ni WA amani anapenda amani ,amani ilipo ndipo alipo.

UMOJA Mungu WETU anapenda UMOJA na upatanishi ,yeye Mungu ni WA UMOJA na Roho,mwana,Mungu BABA

Mungu WETU ni Mungu WA HAKI tuombe KWA AJILI ya utawala WA HAKI na SHERIA.

UCHUMI nchi hii ni yetu yuipende tuombee mema tuombe Mungu atuepushe mbali na umasikini,njaa na magonjwa,na majanga ya asili,mafuriko ,ukame,n.k

Tanzani nchi yangu nakupenda nakuombea mema KWA Mungu,Mungu atuepushe na mabaya.
 
1 Wakorintho 14:33 — "Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani." (Kuhakikisha kuwa fujo hazitoki kwa Mungu

2 Wakorintho 13:11 — "... mwe na amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi." (Kuwepo kwa amani kati yenu kunamfanya Mungu akae nanyi).
 
mnasikia utabiri wa habari ya MVUA KUBWA YA ELNINO ambayo huwa ina ambatana na NJAA na kushusha shughuli za kiuchumi...

kuna mafunuo ambapo mtumishi alifunuliwa katika NDOTO mwezi huu wa nane mwishoni mwaka huu 2026
1.MVUA KUBWA WATU WAKAJIFUNGIA NDANI WASIWEZE KUTOKA NJE ilianza ASUBUHI mpaka mvjana
2.ILIPOFIKA MCHANA kuelekea jioni ikabadilika ikawa MVUA KUBWA YA MAWE watu waliendelea kusali ndani bila kutoka nje,ikanyesha siku kucha
3.KULIPOPAMBAZUKA ikaanza kunyesha MVUA YA DHAHABU dhahabu zilianguka kutoka mbinguni zikapatapakaa juu ya uso wote wa nchi watu waliokuwa wamejificha ndani wakati mvua zikinyesha wote wakatoka nje na kuanza kukusanya dhahabu kwa wingi na kuhifadhi hazina ya kutosha ndani ya nyumba zao kila mmoja .
 
1.AMANI YA NCHI YETU
2.UMOJA WA KITAIFA
3.TUOMBE KWA AJILI YA VIONGOZI WETU
4.UCHUMI WA TAIFA
5.UTAWALA WA HAKI NA SHERIA

Chochote Mungu atakachokuongoza kuomba KWA AJILI ya NCHI yetu omba mana kikubwa zaidi amani ,mana pasipo kuwa na amani ujue Mungu hatakuwepo ambao hakuna amani,tuombe Imani idumu.
Mungu WETU ni WA amani anapenda amani ,amani ilipo ndipo alipo.

UMOJA Mungu WETU anapenda UMOJA na upatanishi ,yeye Mungu ni WA UMOJA na Roho,mwana,Mungu BABA

Mungu WETU ni Mungu WA HAKI tuombe KWA AJILI ya utawala WA HAKI na SHERIA.

UCHUMI nchi hii ni yetu yuipende tuombee mema tuombe Mungu atuepushe mbali na umasikini,njaa na magonjwa,na majanga ya asili,mafuriko ,ukame,n.k

Tanzani nchi yangu nakupenda nakuombea mema KWA Mungu,Mungu atuepushe na mabaya.
Kwani siku zote tulikuwa hatuombi?
 
1. Mvua Kubwa ya Asubuhi (Kujifungia Ndani)
    • Maana: Kipindi cha kwanza kinawakilisha majaribu, dhoruba za maisha, au vizuizi vinavyowashtua watu ghafla ("asubuhi").
    • Ujumbe: Kujifungia ndani kunamaanisha umuhimu wa kukimbilia mahali salama kiroho (kama vile maombi au siri ya uwepo wa Mungu) wakati wa dhoruba, badala ya kupambana nayo kwa nguvu za kibinadamu.

2. Mvua ya Mawe ya Mchana na Usiku (Kuzama Kwenye Maombi)
    • Maana: Katika maandiko, mvua ya mawe mara nyingi inaashiria hukumu ya Mungu dhidi ya uovu au utakaso mzito unaotikisa kila kitu.
    • Ujumbe: Hatua ya watu kuendelea kusali ndani bila kutoka nje inaonyesha ustahimilivu, imani, na toba. Ni ukumbusho kuwa wakati wa dhoruba kali zaidi, silaha pekee ya muumini ni kudumu katika maombi na kukaa ndani ya "safina" ya kiroho.

3. Mvua ya Dhahabu ya Alfajiri (Urejesho na Hazina)
    • Maana: Alfajiri inawakilisha mwanzo mpya baada ya usiku mrefu wa mateso. Dhahabu inasimamia utukufu wa Mungu, utakaso, na baraka zisizo na kifani (Siri za Ufalme wa Mungu).
    • Ujumbe: Wale waliovumilia dhoruba bila kukata tamaa ndio wanaokwenda kurithi utajiri wa kiroho na kimwili. Ni ishara ya thawabu kubwa na urejesho wa kila kitu kilichopotea wakati wa majaribu.
 
Back
Top Bottom