Katika hili, Dr. Slaa anastahili sifa!

Alikuwa hana sababu ya msingi ya kuwaambia watanzania kuwa ndiye mshindi wakati ukweli anaujua na alikuwa anaendekeza hasira za kabila lake. Idadi ya Wabunge wa CDM ndo kipimo tosha hata kwa mtoto mdogo kama wewe kuwa kura alizopata SLAA ndiyo ilikuwa stahiki yake na si vinginevyo. Hakuna mwananchi ambaye angemwaga damu wakati wengi wanajua walimpigia JK.

uliza uambiwe yaliyofanyika ikulu pale usiku kucha usikulupuke kuandika inaoneka ukujua kilichokuwa kikiendelea
 
Siku za mwizi ni arobaini,wakati umefika kuwaonyesha ccm kuwa hata watoto wa shule za msingi na sekondari wamegundua kuwa ccm ni wezi.Cha moto kukiona 2015. Kitaeleka tu
 
Ni kweli sifa mojawapo ya kiongozi bora ni kuwa na busara hata hivyo hakuna busara inayoruhusu kukubali kuporwa haki.

Kunawakati unatakiwa ku give up kwa manufaa fulani....kama slaa alvyofanya, si vizuri kuruhusu damu kumwagika katika mazingira ambayo yanaweza kuepukika

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
watanzania hawatakaa wapigane hadi amani ya nchi kutoweka kisa siasa. Hili nina hakika nalo. Watapigana kwa masuala ya kidini (tuepushie) na rasilimali na kugombea rasilimali. Hili hata cdm wanalijua
 
hivi inakuwaje dogo kama huyu anamzidi akili libaba kama nchemba?nimeamini kuna shahada za kufoji
 
Ulivyopangilia hoja umethibitisha kwamba wewe si wa sekondari za kata a.k.a saint kayumba. Kama nimekosea dogo H ataniambia. Ki ukweli dakt Slaa sio tu anastahili sifa bali Anastahili heshima.Dakt ni msumari wa moto kwenye masaburi ya magamba

bro,nimesoma saint kayumba mwanzo mwisho na hadi kidato cha tano bado nipo saint kayumba Geita!
 
Mungu aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu ili apate kujitukuza katika Israeli.Mungu anaenda kuiaibisha ccm 2015;na kujitukuza kwa wanyonge na wadhaifu kupitia CHADEMA 2015.Ni dhahiri kuwa alishinda na hilo linajulikana kwa ccm,ila Mungu alikuwa bado anakusanya hasira ili kufuta historia ya ccm Tanzania 2015.
 
Huyu mtu haihitaji kusifiwa bali kutumainiwa.Ni bidhaa adimu katika ulimwengu wa sasa ambae anaweza kututoa katika umaskini huu.
Leo nimevuta fikra sana na hatima yake nimeona Slaa anastahili sifa na ikiwezekana anafaa kuwa rais wa nchi yetu.

Kikubwa zaidi kilichonifanya niseme hivi ni baada ya kukumbuka majirani zetu Kenya mwaka 2008 nikiwa kidato cha kwanza.Katika uchaguzi uliofanyika mwaka huo, Kibaki Mwai ndo alitangazwa mshindi dhidi ya Odinga Raila. Kutokana na madai ya kuwa Mwai hakushinda kwa uhalali, Odinga aliwaambia wafuasi wake kuwa yeye ndiye alikuwa mshindi na badala yake wananchi walimwaga damu.

Pia kumbukumbu yangu ikanijia kufikiri tukio jingine hapa kwetu Z'bar. Sharif Hamad alidai kuwa ktk uchaguzi uliofanyika mwaka 2000, yeye ndo alikuwa mshindi na hatimaye wazanzibar walimwaga damu isivyo kifani.

Ninachotaka kukizungumzia hapa ni kwamba,kiongozi anaweza akawa msomi,mwenye lundo la shahada na hata masters lakini bila kuwa na hekima na busara,huyo mtu hafai.Kiongozi anayekuwa hana huruma na roho za binadamu ama analazimisha siasa hadi kwenye uhai,huyo hafai.

Kwanini nimesema Dr Slaa anafaa kusifiwa?

Katika uchaguzi huu uliofanyika mwaka 2010 nikiwa kidato cha tatu umenifanya nimpende Slaa na kummwagia sifa kemkem japo bado nipo mwanafunzi na sijaijua vizuri siasa lakini kwa hili imenibidi leo nivunje ukimya. Tuhuma nyingi zilionekana kuwa Slaa alikuwa na kura nyingi katika majimbo mengi na hivyo angeamua kuwaambia mashabiki wake kuwa yeye ndo alistahili ushindi, sidhani kama vita vingekosekana kama kenya na Z'bar.

Mwenyezi Mungu amjalie 2015 aweze kuichukua nchi maana hata mimi nitakuwa ndiyo kwanza nimemaliza kidato cha sita hivyo nitakuwa na muda kumpigia debe. Dr Slaa ana uamuzi mzur wenye hekima na busara.Nampenda sana Slaa.
 
kwa swali moja ni kuwa kura za Slaa hazijulikani na wala za JK hazijulikani sio tume ya uchaguzi wala kwene vyama vyao wala kwa msajili wa vyama mfano niambie matokeo ya urais jimboni kwako Jk alipata ngapi?
sasa siwezi kukumbuka kichwani.ukitaka undani wa data hizi nenda ofisi za tume ya uchaguzi.iko pale posta ukifika ulizia tu utaoneshwa.
 
Nidyo maana watu mnafeli mtihani.

Hukuombwa matokeo ya URAIS wa Tanzania mwaka 2010 kwa ujumla. Amekuomba matokeo ya Urais wa Tanzania mwaka 2010 kwa KILA JIMBO. Wewe unatoa ya jumla, sijui huwa mnawahi nini kujibu bila kusoma?

Ni heri wala usingelijibu kabisa kuliko kuweka jibu ya swali ambalo hujaulizwa.

Faida ya Baiskeli ni nini? Jibu: "Spoko za Baiskeli ni nzuri sana kwa kufanyia mishikaki."
tembelea ofisi za tume ya uchaguzi uwaombe makabrasha ukatoe copy.
 
Back
Top Bottom