Leo nimevuta fikra sana na hatima yake nimeona Slaa anastahili sifa na ikiwezekana anafaa kuwa rais wa nchi yetu.
Kikubwa zaidi kilichonifanya niseme hivi ni baada ya kukumbuka majirani zetu Kenya mwaka 2008 nikiwa kidato cha kwanza.Katika uchaguzi uliofanyika mwaka huo, Kibaki Mwai ndo alitangazwa mshindi dhidi ya Odinga Raila. Kutokana na madai ya kuwa Mwai hakushinda kwa uhalali, Odinga aliwaambia wafuasi wake kuwa yeye ndiye alikuwa mshindi na badala yake wananchi walimwaga damu.
Pia kumbukumbu yangu ikanijia kufikiri tukio jingine hapa kwetu Z'bar. Sharif Hamad alidai kuwa ktk uchaguzi uliofanyika mwaka 2000, yeye ndo alikuwa mshindi na hatimaye wazanzibar walimwaga damu isivyo kifani.
Ninachotaka kukizungumzia hapa ni kwamba,kiongozi anaweza akawa msomi,mwenye lundo la shahada na hata masters lakini bila kuwa na hekima na busara,huyo mtu hafai.Kiongozi anayekuwa hana huruma na roho za binadamu ama analazimisha siasa hadi kwenye uhai,huyo hafai.
Kwanini nimesema Dr Slaa anafaa kusifiwa?
Katika uchaguzi huu uliofanyika mwaka 2010 nikiwa kidato cha tatu umenifanya nimpende Slaa na kummwagia sifa kemkem japo bado nipo mwanafunzi na sijaijua vizuri siasa lakini kwa hili imenibidi leo nivunje ukimya. Tuhuma nyingi zilionekana kuwa Slaa alikuwa na kura nyingi katika majimbo mengi na hivyo angeamua kuwaambia mashabiki wake kuwa yeye ndo alistahili ushindi, sidhani kama vita vingekosekana kama kenya na Z'bar.
Mwenyezi Mungu amjalie 2015 aweze kuichukua nchi maana hata mimi nitakuwa ndiyo kwanza nimemaliza kidato cha sita hivyo nitakuwa na muda kumpigia debe. Dr Slaa ana uamuzi mzur wenye hekima na busara.Nampenda sana Slaa.