Matokeo ya kura ya Urais yaliyotangazwa na NEC 2010
05/11/2010
26 Comments
Baada ya siku tano za kusubiri matokeo ya kura zilizopigwa na wananchi siku ya Jumapili, Oktoba 31, 2010 ili kumpata mtu atakayekimiliki kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha kuanzia Novemba 2010 hadi Oktoba 2015, hatimaye matokeo hayo yametolewa na Tume ya Uchaguzi Tanzania, NEC, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar Es Salaam. Maelezo kwa ufupi yalikuwa ni kwa vielelezo vifuatavyo:
- Watu waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 20,137,303 (idadi hiyo ilipungua hadi Milioni 19 kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za vifo, safari, kupoteza shahada, nk).
- Watu waliopiga kura walikuwa 8,626,283 sawa na asilimia 42.84% (ya wote waliojiandikisha)
- Kura zilizoharibika ni 227,889 ambazo ni asilimia 2.64% ya kura zote zilizopigwa.
- Kura halali zilikuwa 8,393,394 yaani asilimia 97.36% ya kura zote zilizopigwa.

Matokeo kwa mlinganyo wa kura kwa vyama na wagombezi wake ni kama ifuatavyo:
- Dovutwa Yahmi Nassoro/UPDP kura 13,176 = 0.15%
- Mgahywa Muttamwega Bhatt/TLP kura 17,482 = 0.20%
- Rungwe Hashim Spunga/NCCR-Mageuzi kura 26,388 = 0.31%
- Kuga Peter Mziray/APPT Maendeleo kura 96,933 = 1.12%
- Lipumba Ibrahim Haruna/CUF kura 695,667 = 8.06%
- Slaa Willibrod Peter/CHADEMA kura 2,271,941 = 26.34%
- Kikwete Jakaya Mrisho/CCM kura 5,276,827= 61.17%
Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete
ataapishwa rasmi kesho Jumamosi 6 Novemba 2010 kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hafla hiyo itafanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam. Kikwete anaishika nafasi hii kwa mara ya pili na ya mwisho kwa mujibu wa maelekezo ya katiba ya sasa ya Tanzania.
Kwa taarifa zaidi, maswali, ushauri, mapendekezo, dukuduku nk, tafadhali wasiliana na
NEC.go.tz
Source:
Matokeo ya kura ya Urais yaliyotangazwa na NEC 2010 - wavuti.com