Katika hili, Dr. Slaa anastahili sifa!

Katika hili, Dr. Slaa anastahili sifa!

Mkuu Sir H safi sana, historia yako na yangu vinafanana sana mpaka status ya elimu na miaka pia 18 years old, tushirikiane kwa pamoja kuwahamsha vijana wennzetu huku mashuleni ktk dafatari la kudumu ili tuondoe kwa pamoja huu utawala wa kidhalimu chini ya CCM.

Dr.Slaa tosha 2015.
 
Last edited by a moderator:
Dogo, Dr Slaa hana sifa kuongoza taifa la watu milioni 45. Kashindwa kusimamia familia yake atawezaje kutuongoza.
 
ni mazuzu kama wewe tu ndo wangemwamini.ushinde urais na wabunge wasiofika 30 wa kuchaguliwa hiyo serikali utaiendeshaje?unapeleka bajeti bungeni afu ndo kwa mtindo wetu ule wa kusema wanaoafiki waseme ndioooo......wasioafiki waseme siooooo....!kwa akili zetu za kibongo wapinzani huwa wanapinga tu jambo lolote la serikali hata kama ni zuri so hapo kama una akili kidogo tu unawezajua nini kingefuata!!!
 
Alikuwa hana sababu ya msingi ya kuwaambia watanzania kuwa ndiye mshindi wakati ukweli anaujua na alikuwa anaendekeza hasira za kabila lake. Idadi ya Wabunge wa CDM ndo kipimo tosha hata kwa mtoto mdogo kama wewe kuwa kura alizopata SLAA ndiyo ilikuwa stahiki yake na si vinginevyo. Hakuna mwananchi ambaye angemwaga damu wakati wengi wanajua walimpigia JK.

mkuu hili la kuendekeza hasira tena za kabila lake,hizi hoja zimekwisha pitwa na wakati maana Tanzania hatutazamani kwa ukabila,dini,ukanda,rangi wala chochote chenye kuleta ubaguzi wa namna yoyote hivyo kuendeleza hayo ni kuleta dhana nzima ya kibaguzi.
 
Dogo Sir H,

Kwanza hongera sana kwa kuonyesha weledi wako katika mambo makubwa ya nchi katika umri mdogo.

Pili ni watu wenye akili tamamu tu, kama wewe ndo wanaweza kuona ukweli huu mkuu.

Tatu, kuwa chachu ya mabadiliko kuwaelimisha vijana wenzako kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na 2015 wakaongee na kupaza sauti zao kwenye masanduku ya kura.

Nne, wewe ni mtanzania makini, jibidishe katika masomo ili muda mfupi ujao ulitumikie taifa lako zuri Tanzania linaloteketezwa na Manyang'au CCM kwa kuwadanganya watanzania kwa vipande vya kanga, Tshirt, kofia na pilau.

Hongera sana Mdogo wangu.
 
Last edited by a moderator:
As much as I would vote for Slaa if nominated by his party to contest for the presidency, CDM needs to review their nominations and strategies for 2015. It is more than M4C.
Practically the changes should start within the party before they embark on the bigger picture countrywide.
The party is slowly deteriorating and loose the fame it built itself over the years and the branch networks.
If CDM is to see itself in the leadership of this country, some issues needs to be addressed at the party leadership level.
I would support them better if they change the top layer leadership positions and the current leaders take advisory and advocating role for M4C.
I still think CDM can do better with the time they have to get to 2015.
My take
 
mimi nadhani utoto wako na kutofuatilia mambo kweli utakuwa umechangia kufikiri kama unavyofikiri.kwani kenya ODINGA alipata kura ngapi na KIbaki alipata ngapi?ni upi ulikuwa msimamo wa tume ya uchaguzi ya kenya kuhusu matokeo?ni upi ulikuwa msimamo wa waangalizi wa kumataifa kuhusu matokeo yale?ni upi ulikuwa msimamo wa mashirika ya kimataifa na mataifa mbalimbali juu ya uchaguzi ule?je?unafahamu slaa alipata kura asilimia ngapi dhidi ya rais kipenzi cha watu Ndug.JAKAYA KIKWETE? JE?unafahamu nini ulikuwa msimamo wa tume ya uchaguzi tanzania na waangalizi mbalimbali wa uchaguzi?je?unadhani slaa alikuwa na haki ya kukataa matokeo;au kufanya hivyo ingekuwa ni kosa kisheria na madhara yote ambayo yangejitokeza ingekuwa ni matokeo ya kosa hilo?kama kufanya hivyo ingekuwa ni kosa;vipi umpongeze mtu kwa kutofanya kitu ambacho hata hivyo hakutakiwa akifanye?
Kikwete ni kipenzi chako wewe na unafaidika sana na dhuluma amazoifanyia nchi yetu. kumbuka wengi tunateseka na kufa kutokana na ufisadi uliokidhiri wa raisi huyu na seriakali yake DHAIFU. Siku moja Italia kama sii hapa huko mbele ya safari.
 
ufisadi mkubwa kwenye nchi hii ulifanyika kipindi cha mkapa.alivyo ingia kikwete akaachia watu uhuru wa hali ya juu,ndo mimi na wewe tukajua kwamba kumbe kuna ufisadi.kuhusu kuwa kikwete ni kipenzi cha nani wewe angalia matokeo ya uchaguzi mwaka 2005 na 2010 utajua ni kipenzi cha nani.tutumie facts bwana tuache chuki binafsi.au huamini matokeo ya demokrasia?
 
Wewezo wako wa kufikili ni mdogo sana wewe

Alikuwa hana sababu ya msingi ya kuwaambia watanzania kuwa ndiye mshindi wakati ukweli anaujua na alikuwa anaendekeza hasira za kabila lake. Idadi ya Wabunge wa CDM ndo kipimo tosha hata kwa mtoto mdogo kama wewe kuwa kura alizopata SLAA ndiyo ilikuwa stahiki yake na si vinginevyo. Hakuna mwananchi ambaye angemwaga damu wakati wengi wanajua walimpigia JK.
 
Alikuwa hana sababu ya msingi ya kuwaambia watanzania kuwa ndiye mshindi wakati ukweli anaujua na alikuwa anaendekeza hasira za kabila lake. Idadi ya Wabunge wa CDM ndo kipimo tosha hata kwa mtoto mdogo kama wewe kuwa kura alizopata SLAA ndiyo ilikuwa stahiki yake na si vinginevyo. Hakuna mwananchi ambaye angemwaga damu wakati wengi wanajua walimpigia JK.
mkuu unajuaje hakuna ambaye angemwaga damu?.pia acha element za ukabila!
 
Watu wenye uwezo wa kuongoza hawapendi uongozi,wale wasio na uwezo wanapenda uongozi! Dr slaa yuko wapi?
 
Wapo wananchi wengi tu walioipigia kura CHADEMA na kumpatia ushindi Dkt. Slaa na hata wengine wachache ambao hawakumpigia kura, na wengine wengi tu ambao hawakupiga kura, wanajua uwezo wa Dkt. Slaa ambao unasababishwa na composition ya vitu vingi, ulitunusuru Watanzania kuchukua njia ya Ivory Coast, katika kusimamia haki na uwajibikaji, kutokana na watawala kuamua kwa makusudi kutoheshimu sanduku la kura.

Hata wao wanajua, Slaa alitosha na kuvuka uwezo wao kwa mbali. Hongera kamanda 'mdogo' kwa kufuatilia siasa za nchi yako. Siasa ni maisha ya mwanadamu. Unayo haki na wajibu wa kujua mwelekeo wa nchi yako. Keep it up. Kila la heri kwenye masomo yako. Fanya jitihada za kutosha na kujifunza na kupata maarifa, lakini usisahau, siasa ni maisha yako, mimi, yule, wale na sisi sote.
 
mimi nadhani utoto wako na kutofuatilia mambo kweli utakuwa umechangia kufikiri kama unavyofikiri.kwani kenya ODINGA alipata kura ngapi na KIbaki alipata ngapi?ni upi ulikuwa msimamo wa tume ya uchaguzi ya kenya kuhusu matokeo?ni upi ulikuwa msimamo wa waangalizi wa kumataifa kuhusu matokeo yale?ni upi ulikuwa msimamo wa mashirika ya kimataifa na mataifa mbalimbali juu ya uchaguzi ule?je?unafahamu slaa alipata kura asilimia ngapi dhidi ya rais kipenzi cha watu Ndug.JAKAYA KIKWETE? JE?unafahamu nini ulikuwa msimamo wa tume ya uchaguzi tanzania na waangalizi mbalimbali wa uchaguzi?je?unadhani slaa alikuwa na haki ya kukataa matokeo;au kufanya hivyo ingekuwa ni kosa kisheria na madhara yote ambayo yangejitokeza ingekuwa ni matokeo ya kosa hilo?kama kufanya hivyo ingekuwa ni kosa;vipi umpongeze mtu kwa kutofanya kitu ambacho hata hivyo hakutakiwa akifanye?

Wewe vipi?wala usimwonee kwa udogo wake unaweza kuwa mkubwa lakini huna cha maana.Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya SAMWEL KIVUITU alikiri kushinikizwa kumtangaza Kibaki kama mshindi.Wakaguzi wa nje waliwaganyika wengi walisema ODINGA alishinda.Acha kutoa maoni kwa hisia za ukada!!
 
Back
Top Bottom