Katibu wa Bunge na Hesabu za Asilimia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu wa Bunge na Hesabu za Asilimia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Amanikwenu, Nov 13, 2010.

 1. A

  Amanikwenu Senior Member

  #1
  Nov 13, 2010
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jana (12/11/2010) wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi wa Spika, Katibu wa Bunge Dr. Thomas Kashililah alisema kuwa Anne Makinda alipata kura 265 kati ya kura 327 zilizopigwa. Aliutaja ushindi huu wa Anne Makinda kuwa ni asilimia 74.2 ya kura zote. Naona hapa Katibu wa Bunge aliteleza au alipigwa chenga kidogo na hesabu za asilimia. Kwa kura alizopata Anne Makinda ki-asilimia ni 81.04 na si asilimia 74.2 kama alivyoutangazia umma wa Watanzania na dunia. Vinginevyo atuambie kuwa kura alizopata mama Anne Makinda ni 242.5 na wala si 265. Mbaya zaidi vyombo vyetu vingi vya habari vimeendelea kutaja hizo asilimia 74.2 badala ya kugundua kwamba kuna kasoro katika kile alichokitangaza Katibu wa Bunge
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Amani kwako pia!
   
 3. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  hii do bongo bwana kanyaga twende:bolt:
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaai ukizoea kuchakachua mpaka calculator unashindwa kuitumia kabisa..hayo ndo madhara ya kuchakachua
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  nili hoji kuhusu suala hili jana katika thread moja iliyokuwa ikitutangazia live uchaguzi wa speaker.

  Huhitaji calculator kujua kuwa hesabu hazijakaa sawa kwa kutumia logic tu hata kama hesabu zinakupiga chenga. Ikiwa 53 ni 17% na 265 ni 74%, kura 9 ni 9% ya 327?

  aibu ni kuwa hakuna mwandishi aliyehoji hili jana kutwa nzima wakati ni kitu kilicho dhahiri kabisa.
   
 6. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kuna tofauti ya kura 22 ambazo ni za CUF, hii inawezekana CUF walimpigia Marando lakini wakaamua kuziondoa ili kuchonganisha upinzani
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kura zimetimia kwa mgawanyiko wa 265,53 na 9 na kufanya 327, asilimia ndo iligomba.

  au unataka kusema asilimia ndo correct na kura ndo zimekosewa?
   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Watanzania hatuko makini na ndio maana tunaibiwa kirahisi.

  Nimeshangazwa na magazeti yote kurudia asilimia ambayo ina makosa. Yaani vyombo vyetu ni kama kasuku, vinaimba tu kile walichoambiwa au ndio dunia ya copy and paste? Hata yule mwandishi wa Reuters naye kachemsha.

  Na wale wabunge walioenda kusimamia kuhesabu kura, walikuwa wanasimamia nini?
   
 9. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  CCM: 265/327=81%
  CHADEMA:53/327=16%
  CHAKACHUA FORUM: 9/327= 3%

  UKIZOEA KULA NYAMA YA MTU UTAENDELEA KULA HADI MWISHO:By Mwl.Nyerere. CCM wamezoea vya kunyonga AIBU YAO AIBU YETU???? AIBU YAOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
   
 10. c

  chidide Member

  #10
  Nov 13, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa la waandishi wa habari wa Tanzania ni kufanya utafiti b4 hawajaandika. Ndio maana wamekuwa wanatoa habari ambazo sometimes ni only 10% correct. Hatari iliyopo ni kuwa wanamisslead waTZ sana
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Tanzania kila kitu kinawezekana. Hata bunge lililopita walichakachua mswada wa sheria za matumizi katika uchaguzi na wote wakakubali chenga hilo kasoro Dr Slaa.
  Hii inahitaji umakini.
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Nov 13, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Gregory Teu alikuwa mbali naye?
   
 13. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #13
  Nov 13, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Du! JF Wakati mwingine Mnanishangaza.

  Mmefanya consideration ya kura zilizoharibika?
   
 14. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #14
  Nov 13, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,322
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  Ahsante niliona hiyo pia jana pale katibu wa Bunge alipotangaza matokeo.
  Anne kura (265 x 100)/ 327=81.03%
  Marando (53 x 100)/327=16.2%
  Zilizoharibika (9 x 100 )/327=2.8%
   
 15. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #15
  Nov 13, 2010
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ukosefu wa umakini ni tatizo kubwa katika nchi hii, pengine kuliko hata ufisadi!
   
 16. s

  shostsm New Member

  #16
  Nov 13, 2010
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa watu wamezoea kuchakachua, ni aibu kubwa kwa watu wa ngazi nzito kama ile kukosea namna hii. Nafikiri Mungu ameamua kuwaumbua na kuweka makosa yao peupe. Something very serious is hidden behind this!!
  Hata matokeo ya kura za Uraisi hesabu zake hazieleweki. Ukijumlisha kura walizopata wagombea pamoja na zilizoharibika unapata waliopiga kura ni 8,626,303 lakini tume ya uchaguzi ilitangaza kuwa waliopiga kura ni 8,626,283. Hapo kuna tofauti ya kura 20, kuthibitisha kuwa matokeo hayo ni ya kupikwa au KUCHAKACHULIWA.
  Mwenyekiti wa NEC alianza kwa kutoa takwimu zifuatazo:
  Waliojiandikisha: 20,137,303
  Waliopiga kura: 8,626,283 sawa 42.64% (ukifanya hesabu utapata 42.84%)
  Kura zilizoharibika: 227,889
  Kura halali zilzopigwa: 8,398,394

  KUGA PETER MZIRAY
  APPT - MAENDELEO
  96,933
  1.12%
  KIKWETE JAKAYA MRISHO
  CCM
  5,276,827
  61.17%
  SLAA WILLIBROD PETER
  CHADEMA
  2,271,941
  26.34%
  LIPUMBA IBRAHIM HARUNA
  CUF
  695,667
  8.06%
  RUNGWE HASHIM SPUNDA
  NCCR-MAGEUZI
  26,388
  0.31%
  MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT
  TLP
  17,482
  0.20%
  DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA
  UPDP
  13,176
  0.15%
  SPOILT VOTES

  227,889
  2.64%
  TOTALS

  8,626,303
  100.00%


  Hii ni sehemu tu ya kasoro kibao zilizojitokeza kwenye mchakato mzima wa uchaguzi. Hivi NEC watatueleza nini? Wanadai eti wanatumia teknolojia mpya ya computer!!! Computer gani hizi haziwezi hata kufanya hesabu za kujumlisha na kutafuta asilimia. Mbona hata mtoto wa darasa la nne angeweza kujumlisha na kutoa majibu sahihi tena kwa kichwa bila hata msaada wa calculator?

  NEC bila hata aibu wanadiriki kutamka hadharani eti kwamba wataalam wa kutumia kompyuta ni wachache nchi hii. Nakubali nchi hii ina wataalam wachache katika maeneo mengi lakini hatujafikia kukosa watu wa kufanya entries za kitoto kama hizo kwenye computer au kushindwa kufanya hesabu hizo za kujumlisha.
   
 17. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #17
  Nov 13, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nimeamini hakuna kinacho shindikana katika nchi hii.
   
 18. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #18
  Nov 13, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mnawaonea! Mdahalo bubu wa JK alikiri kwamba hakupenda hesabu shuleni (sijui alifauluje uchumi). Mnategemeaje wajue hesabu wakati hazifundishwi tena mashuleni tz? Halafu zoezi lile la uchaguzi bungeni halikufadiliwa na wawekezaji, Tena kanuni za bunge haziruhusu consultants waingie ukumbi wa bunge.

  Msiwaonee kabisa!
   
 19. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #19
  Nov 13, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Ni hatari sana sana. Matokeo ya urais yalikosewa, tukanyamaza. Matokeo ya uspika yamekosewa tumenyamaza. Mungu atuepushie uozo huu
   
 20. A

  Amanikwenu Senior Member

  #20
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hali ya ukosefu wa umakini hapa nchini inasikitisha sana. Ni aibu sana kuona kuwa Katibu wa Bunge tena mwenye PhD anafanya makosa kama hayo na bado amekaa kimya bila kufanya masahihisho na kuuomba radhi umma wa Watanzania na Wabunge.

  Kwa upande mwingine kama mchangiaji mmoja alivyosema kuhusu uidhaifu wetu katika Hisabati hali inasikitisha sana. Ukiangalia takwimu zinaonyesha kuwa wastani wa asilimia 82.8 ya watoto wetu wanaofanya mtihani wa kumaliza darasa la saba hufeli somo la Hisabati lakini karibu asilimia 40 huchaguliwa kuendelea na masomo ya Sekondari. Hatujui matokeo ya mwaka huu yatakuaje. Kwa ngazi ya kidato cha nne hali nayo ni mbaya sana tu, kwani zaidi ya asilimia 75 ya wanafunzi wanaofanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne hupata F katika Hisabati.
   
Loading...