Rais Magufuli amethibitisha kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amejiuzulu nafasi yake.
“Kangi Lugola nakupenda sana na hapa umenisifia kwelikweli nakushukuru lakini kwenye hili hapana, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani nampenda sana lakini kwenye hili la kwenda Nje ya Nchi unasaini fedha ambazo hazijapitishwa hata na Bunge hapana”
"Ninajua Waziri wa Mambo ya Ndani hayupo hapa ameshaandika barua ya kujiuzulu na mimi nimeshamkubalia"
Pia Dkt.John Pombe Magufuli amemuondoa kwenye nafasi yake Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Tanzania, Thobias Andengenye kutokana kwenda ulaya kusaini mdaradi ambao haujapitishwa na bunge.