Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani aandika barua ya Kujiuzulu. Lugola na Andengenye wakalia kuti kavu, Rais Magufuli asema hawafai

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Messages
527
Points
1,000

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2018
527 1,000
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani Aandika barua ya Kujiuzulu.

Rais Magufuli akiwa anahutubia wakati wa ufunguzi wa nyumba za Askari Magereza, amesema kwamba..

Nampongeza sana Meja Jenerali, Kingu ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kuwajibika kwamba ametambua. Na nimamuheshimu na nitaendela kumuheshimu

Lugola nampenda sana ni mwanafunzi wangu nilimfundisha Sekondari, hapa umenisifia kwelikweli nakushukuru lakini kwenye hili hapana. Nilijua nisingemkuta hapa, Kamishna Andengenye ni mchapakazi nilitegemea hapa asiwepo hatuwezi tukaendesha nchi kwa misingi ya ajabu.

"Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani nampenda sana lakini kwenye hili la kwenda nje ya nchi unasaini fedha ambazo hazijapitishwa hata na Bunge hapana".


Lugola Andengenye.JPG

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akijadiliana mambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola.
 

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Messages
16,634
Points
2,000

figganigga

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2010
16,634 2,000
Wakuu,

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji, Thobias Andengenye Wametumbuliwa muda huu. Huku Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Meja Jenerali Jacob Kingu akiandika Barua ya Kujiuzulu.

Wanakabiriwa na tuhuma za kusaini mkataba nje ya Nchi huko Romania. Mkataba ambao haujapitishwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge

“Ninashangaa kuwaona Kangi Lugola na Kamishana Jenerali bado mko hapa sitaki kuwa mnafiki mtu anasaini zaidi ya Sh trilioni moja wakati sheria zote zinajulikana mwenye mamlaka ya kukopa fedha kwaajili ya Tanzania ni Wizara ya Fedha peke yake ikiwa hivyo kila mtu atakuwa anakopa hata mimi nitakopa sasa mimi nitaendelea kuwapenda lakini kwenye position hii no,” Kasema Magufuli

Stay tuned
1579771531532.png
1579771665534.png
 

Echililo

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2016
Messages
597
Points
1,000

Echililo

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2016
597 1,000
Rais Magufuli amethibitisha kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amejiuzulu nafasi yake.

“Kangi Lugola nakupenda sana na hapa umenisifia kwelikweli nakushukuru lakini kwenye hili hapana, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani nampenda sana lakini kwenye hili la kwenda Nje ya Nchi unasaini fedha ambazo hazijapitishwa hata na Bunge hapana”

"Ninajua Waziri wa Mambo ya Ndani hayupo hapa ameshaandika barua ya kujiuzulu na mimi nimeshamkubalia"

Pia Dkt.John Pombe Magufuli amemuondoa kwenye nafasi yake Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Tanzania, Thobias Andengenye kutokana kwenda ulaya kusaini mdaradi ambao haujapitishwa na bunge.
 

mswati52

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2019
Messages
327
Points
500

mswati52

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2019
327 500

Siwamilele

Member
Joined
Oct 22, 2019
Messages
53
Points
150

Siwamilele

Member
Joined Oct 22, 2019
53 150

Forum statistics

Threads 1,390,620
Members 528,218
Posts 34,056,622
Top