Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aandika barua ya kujiuzulu

Soma hapa!
182E609F-B1F1-4517-A006-96F1DF8A0E4C.jpeg
 
Ikiwezekana wajiudhuru wote kabisa, ili kuleta ahueni kwa nchi na wananchi wake wenye mapenzi mema na nchi hii.
Wakati uvumi wa uteuzi wa Paul Makonda kwa nafasi ya Katibu Mwenezi wa chama chao uliposambaa, nilitoa comment humuhumu JF kwamba "Naomba Mungu habari hiyo iwe ya kweli ili kuharakisha Anguko," na kweli sasa yameanza kutimia. " Wajenzi wa Mnara wa Babeli hawaongei tena lugha moja kwa sasa."

 
Kama kweli Chongolo amesingiziwa hayo mambo na ameamua kujiuzulu kwa sababu hiyo, anastahili pongezi.

Wasiwasi wangu isijekuwa kama yale ya Ndugai, unalazimishwa kuandika barua ya kujiuzulu kisha unaiweka kama vile umeamua kujiuzulu kwa maamuzi yako binafsi.

Chongolo kama kweli ungekuwa hauhusiki na hayo mambo unayodai kuchafuliwa nayo, kwanini usikitake chama chako kufanya uchunguzi ili kujiridhisha kama tuhuma dhidi yako ni za kweli au hapana?

Unatulazimisha tuamini tu kwamba umeamua kuitoa sadaka kazi kwa sababu ya tuhuma za uongo?!

Not me.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom