Katibu Mkuu Umoja wa Posta Afrika (PAPU) awasili jijini Dodoma

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
KATIBU MKUU UMOJA WA POSTA AFRIKA (PAPU) AWASILI JIJINI DODOMA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU),Bwana Sifundo Chief Moyo amewasili jijini Dodoma akiambatana na msaidizi wake Bi Jessica Uwera Ssengooba kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya Siku Posta Duniani yatakayofanyika tarehe 9 Octoba, 2021.

Maadhimisho hayo yametanguliwa na wiki ya maadhimisho ambapo shuguli mbalimbali zinafanyika kuanzia tarehe 6-9 Oktoba ,2021 na siku ya hitimisho ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Isdor Mpango.

Katika ziara yake leo tarehe 7 Oktoba 2021 Ndg. Moyo amepata nafasi ya kumtembelea ofisini kwake jijini Dodoma Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo na kufanya mazungumzo naye, pia ametembelea vituo vya Huduma Pamoja (One Stop Center) katika ofisi za Shirika hilo, jijini Dodoma.

Akiwa ofisini hapo, ameeleza kuwa, Posta kwa sasa inaendelea kuboresha huduma zake na amempongeza Mwana Mbodo kwa juhudi anazoendelea kuzifanya katika kufanya magezi makubwa hasa yale yanayolifanya Shirika la POsta kuwa la Kidijitali. Ameongeza kuwa Shirika hilo linajiweka katika hatua nzuri kwani dunia imebadilika na mahitaji ya watu yanabadilika kulingana na mazingira

Aidha, Ndg. Moyo ameihakikishia Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Posta kuwa litaendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha katika kuifanya Sekta ya Posta kuwa ya kidijitali na yenye manufaa kwa jamii.

Naye Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Mbodo ameeleza kuwa Shirika hilo kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania linaendelea na mikakati yake ya kulifanya Shirika kuwa la kisasa zaidi kulingana na mahitaji ya wananchi wake, kwani tayari Serikali imeshawapatia zaidi ya Bilioni 7 kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Shirika.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu PAPU akiwa na msaidizi wake Jessica Ssengooba wameweza kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya watoa huduma likiwemo la Shirika la Posta na kupata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Shirika hilo kwenye maonesho yanayoendelea katika ukumbi wa Jakaya kikwete, jijini Dodoma

Pia Katibu Mkuu huyo ameweza kushuhudia magari mapya yaliyonunuliwa na yatakabidhiwa kwa Shirika na mgeni Rasmi katika kilele cha siku ya Posta Dunia Oktoba 9,2021 Mheshimiwa Philip Isdor Mpango,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika ziara hiyo Kaimu Postamasta Mkuu aliambatana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Elia Madulesi, ambapo Viongozi wa PAPU waliambatana na Mkurugenzi wa Mawasiliano katika ofisi ya Katibu Mkuu wa PAPU Bwana Amadou Bello.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania
7 Octoba, 2021

IMG-20211007-WA1004.jpg

IMG-20211007-WA1001.jpg

IMG-20211007-WA1009.jpg
 
IMG-20211007-WA0140.jpg

IMG-20211007-WA0141.jpg
 
Back
Top Bottom