Rais Samia: Mfumo wa Posta ubadilike kuendana na Mahitaji ya sasa ya soko

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki ufunguzi wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Arusha, leo Septemba 2, 2023.


View: https://www.youtube.com/live/MSIbItMgQvo?si=ogAiZuUyEEvUzqqK

===
Rais Samia amesema huu ni mradi wa ubia uliogharamiwa na umoja wa Posta Afrika kwa 60% na Tanzania kupitia TCRA kwa 40%.

Mwaka 1874 ulianzishwa umoja wa Posta Duniani, na baada ya kuanzishwa kwa AU, wakuu wa nchi za Afrika wakaona waanzishe pia umoja wa Posta Afrika.

Mifumo ya mawasiliano inachukua sura mpya ya kidigitali, mfumo wa posta nao hauwezi kubaki kama ulivyopita, lazima ubadilike kuendana na mahitaji ya soko.

Serikali imechukua hatua za kupitia sera ya Taifa ya Posta, kuweka mfumo wa anuani za makazi, kuanzisha vituo vya kutoa huduma kwa pamoja (Makao ya ajira, Uhamiaji, NIDA, BRELA, TRA na RITA). Hili limesaidia Serikali kupunguza gharama.

Umoja wa Posta Afrika unaweza kuleta mabadiliko makubwa ya kidigitali katika bara la Afrika.
 
Mwendelezo ni ule ule wa zinduzi bwawa la nyerere hatujui lini litaanza uzalishaji!
 
Kizimkazi hiki Cha kupiga misele kiko damuni tu. Tanganyika haina petroleum n diesel ⛽.wala sioni akitatua
 
Back
Top Bottom