Katiba inasemaje kuhusu kuongozwa na Mabalozi wa CCM nchi nzima?

Unitman

JF-Expert Member
Jul 14, 2021
256
354
Habari za kazi ndugu wadau. Napenda kuuliza hivi Katiba ya Tanzania inasemaje kuhusu wajumbe wa nyumba kumi au mabalozi.

Maana wanateuliwa na CCM kuongoza wananchii. Balozi CCM, Mwenyekiti CCM, diwani CCM, mbunge CCM mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, wote CCM, mtendaji kata CCM, Katibu tarafa CCM, COVID 19 CCM ,SPIKA CCM.

Is there any real Man in Tanzania?
 
Habari za kazi ndugu wadau.Napenda kuuliza hivi katiba ya tanzania inasemaje kuhusu wajumbe wa nyumba kumi au mabarozi.
Maana wanateuliwa na CCM kuongoza wananchii.Barozi
ccm,mwenyekiti CCM,diwani ccm,mbunge CCM mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa,wote CCM,IGP cccm,mtendaji kata CCM, Katibu tarafa CCM,COVID 19 CCM ,SPIKA CCM,Mahakama CCM.
Is there any real Man in Tanzania??
Balozi wa nyumba 10 hana mamlaka yoyote kisheria , mimi sijawahi kuwaheshimu wala kuwatii , kwanza wananiogopa vibaya sana !
 
Tatizo ukienda Serikali ya Mtaa au Mtendaji Kata kwa haja ya kiofisi watakutaka upeleke barua ya mjumbe. Hata Polisi wanauliza mjumbe. Wala hawataki mjumbe wa Serikali ya Mtaa ambao wao ni wa Serikali.
Ni mabaki ya mfumo wa chama kimoja ambao unalazimishwa kuendelea kutumika.
 
Balozi wa nyumba 10 hana mamlaka yoyote kisheria , mimi sijawahi kuwaheshimu wala kuwatii , kwanza wananiogopa vibaya sana !
Wao wapo kwa ajili ya CCM. Wewe sio mwana CCM. Uwaheshimu usiwaheshimu inawahusu nini? After all jitahidi kumuheshimu kila mtu. Itakuletea faraja rohoni mwako.
 
Hakuna mtu analazimishwa kuhudumiwa na Mabalozi wa Nyumba kumi.

Hakuna Mahali balozi ameorodheshwa kwenye Pay-roll ya serikali.

Mabalozi wa Myumba 10 ni nguzo kuu ya CCM kuwafikia wanachama wao kwa Grass- Root.

Wakati vyama vingine vikiwa na ofisi zilizozungukwa na vichaka kwa kusahaulika.
IMG-20220829-WA0021.jpg
 
Hakuna mtu analazimishwa kuhudumiwa na Mabalozi wa Nyumba kumi.

Hakuna Mahali balozi ameorodheshwa kwenye Pay-roll ya serikali.

Mabalozi wa Myumba 10 ni nguzo kuu ya CCM kuwafikia wanachama wao kwa Grass- Root.

Wakati vyama vingine vikiwa na ofisi zilizozungukwa na vichaka kwa kusahaulika.View attachment 2412034
Mwanachama wa CCM
1664537002242.jpg
 
Serikali inaanzia kwe mwenyekiti wa mtaa/ kitongoji.

Balozi siyo kiongozi wa wananchi wote. Ni kiongizi wa chama.

Hata chama chako kinaruhusiwa kuwa na mabalozi nchi nzima

Kumbuka balozi huchaguliwa na wanachama wa chama husika tu.

Kama ulihusika kumchagua balozi wa CCM na wewe siyo mwana CCM nenda kadai kura yako.
 
Balozi wa ccm ni ccm tu ndio anapaswa kushughulika nao na si vinginevyo.
Mhesimu kama binadamu lakini siyo kiongozi wako isipokuwa kama wewe ni ccm.
 
Kwa ujumla CCM wamejikita sana na kwa jinsi hii hawawezi kuondoka madarakani kiraisi. Hata kama wananchi watawakataa wataendelea kutawala kidicteta tu. Watakachobadilisha ni maraisi tu lakini kwa CCM tusitegemee mabadiliko sana kwenye nchi yetu pendwa. Hata katiba mpya tunayotaka wao wana nguvu ya kuiunda ili iwasaidie wao kukaa madarakani. Kuhusu mabalozi wa nyumba kumi kumi ingelikuwa vizuri kama kwenye katiba mpya ingependekeza wawe chini ya serikali yaani chini ya mwenyekiti wa kijiji kwa ajili ya kuwaangalia watu na usalama wao wa kila chama na siyo kama ilivyo sasa wanaishia kufanya kazi za CCM tu
 
Back
Top Bottom