vukani
JF-Expert Member
- Dec 30, 2009
- 245
- 165
Nimewaza haya nikiwa nje ya Dini kabisa. Hapa nilikuwa naliangalia jambo hili Kisayansi, kwa hiyo kama ukihusisha Dini yako na jambo hili, utatoka nje ya mada.
Nilikuwa najiuliza tu kwamba, sisi wote tulitoka kwa wazazi. Baba alitoa mbegu, ambazo kwa sehemu kubwa ni protini (chakula alacho). Kwa kufanya tendo la ndoa mara moja mwanamme hutoa cc 5 za manii (ujazo wa kijiko kimoja cha chai). Kila cc moja ina mbegu zipatazo milioni 120. Hivyo, cc 5 za manii, zina mbegu zipatazo milioni 600. Kati ya hizi, ni mbegu moja tu inayotakiwa kurutubisha yai ili azaliwe mtoto, ni ajabu eh!
Mbegu moja kati ya mbegu milioni 600. Ni uwiano mbaya sana kama siyo kituko. Yaani hii ni bahati sana, kati ya watu milioni 600 aliowatoa baba ukabahatika wewe peke yako. Mama naye alitoa yai. Kila mwezi hutoa yai moja ambalo likirutubishwa anazaliwa mtoto. Kila mwezi, mwanamke hutoa yai moja, kwa mwaka mmoja hutoa mayai 12. kati ya haya ni mangapi hurutubishwa? Kumbuka, mbegu na yai vilitokana na vyakula ambavyo vilioteshwa au kupandwa kwenye udongo wenye rutuba (mbolea) na maji. Maji na mbolea vilitoka wapi? Ni mzunguko usio na mwisho wala mwanzo ..