Tanzania imetumia Hekta Milioni 10.8 tu kati Milioni 44 za ardhi inayofaa kwa Kilimo hadi sasa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Akizungumza na Vyombo vya Habari, Msemaji Mkuu wa Serikali amesema Tanzania ina hekta Milioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo na kati yake ni hekta Milioni 10.8 ndizo zinalimwa na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutambua kuwa kilimo ndicho kinaajiri zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania kuanzia msimu huu imeanza kutoa pembejeo za ruzuku. Imetenga shilingi Bilioni 150 kwa ajili hiyo.

Usambazaji pembejeo za ruzuku hasa Mbolea unaendelea nchi nzima kwa bei ya chini ya nusu ya bei ya mwaka jana, yaani kati ya shilingi 40,000 na shilingi 70,000 kwa mfuko mmoja wa kilo 50.

Mwaka 2023 mbolea ziliuzwa hadi zaidi ya shilingi 150,000 kwa mfuko mmoja katika baadhi ya maeneo

Msigwa amesema "Nafurahi kuwajulisha kuwa wakulima nchini kote wanaendelea kunufaika na mbolea ya ruzuku, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imesajili wazalishaji wa mbolea 3, wasambazaji wa mbolea 31 na mawakala 3,103 katika mikoa yote nchini."

"Kwenye vitabu vyetu vya wakulima waliosajili kwa ajili ya kupata mbolea ni 3,264,440 na kupitia mfumo wetu wa kidigitali tumesajili wakulima 2,793,469."

"Hadi tarehe 09 Januari, 2023 wakulima wamesambaziwa mbolea ya ruzuku tani 194,259 yenye thamani ya shilingi Bilioni 208.6 ambapo idadi ya wakulima walionufaika ni 560,451 ambao ni sawa na asilimia 20 ya wakulima waliosajiliwa nchi nzima."

Zoezi la usambazaji wa mbolea hizi linaendelea na hivi sasa kwa wale wakulima wenzangu na mimi huu ndio muda wa mbolea za kukuzia baada ya wengi kuwa wamekamilisha kupanda kwani kalenda ya kilimo inaelekeza kuwa tarehe 15 ndio mwisho wa kupanda zao la mahindi.

"Naomba kuchukua fursa hii kurudia kuwapongeza wakulima wote nchi kwa kuungana na Serikali ya awamu ya sita katika kuharakisha mageuzi ya kilimo. Kuongeza bajeti ya kilimo kutoka shilingi Bilioni 254 hadi Bilioni 954 sio jambo dogo na halikuwa kutokea wakati wowote katika historia ya nchi yetu. Hii yote ni dhamira njema ya Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyeamua kuwagusa Watanzania wote kupitia kilimo."

Upande wa Taarifa za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)

NBS imetabiri kupungua kwa mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji baridi, kutoka asilimia 9.7, kufikia Machi mwaka huu. <b><i>Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, leo 18 Januari 2023, Dk. Albina Chuwa, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, amedai tofauti na ilivyokuwa Desemba mwaka jana, katika kipindi cha robo mwaka ya kwanza ya 2023 (Januari hadi Machi), mfumuko huo, utapungua hadi kufikia 8.4 asilimia.

Dk. Chuwa alitoa kauli hiyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari, katika kilichoitwa, “kikao kazi cha idara yake.”

Alisema, bei hizo zitapungua kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali kudhibiti mfumuko wake, ikiwemo kuimarisha sekta ya kilimo kwa kuongeza bajeti na kutoa ruzuku kwenye mafuta na mbolea.

Akijibu baadhi ya maswali ya waandishi waliotaka kufahamu vigezo vinavyotumika kupima mfumuko huo wa bei, Dk. Chuwa alisema, tofauti zinatokana na taratibu zinazopima viashiria hivyo.

Alisema, tofauti hiyo inatokana na NBS kufanya takwimu zake kwa kuangalia bei za bidhaa za nchi nzima kisha hutoa wastani wa mfumuko wa bei kitaifa.</p>
<p>Baadhi ya waandishi walitaka kufahamu vigezo vinavyotumniwa na taasisi hiyo, kufuatia madai kuwa ripoti ya NBS mara nyingi huonyesha tofauti na uhalisia.

Baadhi ya mifano iliyotolewa, ni kwamba wakati NBS wanasema mfumuko wa bei kitaifa umepungua, bei za bidhaa hasa vyakula, zinaonekana kuwa juu nchi mzima.

Ametolea mfano wa bei ya mchele nchini ambapo katika baadhi ya mikoa, huuzwa kati ya Sh. 2,500 na 3,000; na au hadi 3,500, lakini wastani wake kitaifa ni 2,500 kwa kilo.

"Bei ya michele tunapima wastani wake kwa kilo ya kwa nchi, tunachukua wastani wa bei za mikoa yote ya Tanzania Bara, kisha tunafanya wastani wa bei kwa nchi. Hapo utakuta ile bei ya Sh. 3,000 na 2,000 wastani wake inakuwa Sh. 2,500" ameeleza

Akizungumzia ustahamilivu wa mfumuko wa bei, Dk. Chuwa alisema, mfumuko huo uko stahimilivu, kwa kuwa bado umebaki kwenye tarakimu moja ambapo kwa mwaka 2022 ulikuwa 4.3 asilimia.

Katika hatua nyingine, Dk. Chuwa amezungumzia fahirisi ya bei za bidhaa, akisema kati ya Sh. 100 ya mwananchi, asilimia 28.2 hutumika kwa bidhaa za vyakula na vinywaji, wakati asilimia 15 zinakwenda kwenye nishati ikiwemo umeme, gesi na mafuta.

Amesema, asilimia 14 kati ya Sh. 100 ya mwananchi inakwenda katika usafiri.

Alisema, pamoja na kuonekana bei za bidhaa hasa vyakula kuonekana kupanda mtaani mwezi Desemba 2022, lakini mfumuko wa bei kitaifa ulishuka hadi kufikia asilimia 4.8, kutoka asilimia 4.9, iliyokuwa Novemba.

Aliongeza, “tumepima viwango hivyo kwa kuangalia mapato na matukizi ya kaya. Serikali imejipanga kupungua gharama za uzalishaji mazao ya kilimo, ili kuongeza kipato cha mwananchi kwa kuwa tunafahamu kilimo ni nguvu kazi ya taifa."

Kwa mujibu wa Dk. Chuwa, mfumuko wa bei kitaifa kwa Desemba ulipungua kutokana na kushuka kwa bei ya bidhaa zisizokuwa za vyakula, ikiwemo dizeli na petroli.

Alisema, bei ya saruji ilipungua kutoka asilimia 3.2 hadi 2.5, gesi ya kupikia (asilimia 13.8 hadi 11.8). Hata hivyo, Dk. Chuwa amesema, serikali iko katika maandalizi ya mwisho ya kufanya utafiti wa hali ya umasikini nchini kwa mwaka wa 2023/2024. “…tunategemea kufanya utafuti kwenye mapato na matumizi ya kaya, ambayo itatupa hali ya umasikini. Tuko kwenye maandalizi ya mwisho ya kufanya hivyo," alieleza.

Mtakwimu huyo wa serikali amesema, utafiti wa mwisho wa hali ya umasikini ulifanyika mwaka 2017/18, ambapo ulionyesha asilimia 28.2 ya wananchi, wanaishi chini ya mstari wa umasikini

Lakini wakati serikali ya Tanzania, ikieleza kuwa mfumuko wa bei unatarajiwa kuhuka kufikia Machi mwaka huu, Benki ya Dunia (WB), inaendelea kusisitiza kuwa “dunia iko karibu na mdororo wa uchumi.”

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Washington DC, nchini Marekani, Rais wa WB, David Malpass amesema, baadhi ya nchi tayari zimepandisha viwango vyao vya riba na huenda sasa zinafikia hatua ambayo hazihitaji kuongeza.

Kwa mujibu wa benki hiyo, mfumuko wa bei ulimwenguni utazidi kuongezeka, huku ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2023 ukishuka kutoka asilimia 3 hadi 1.9 asilimia.

Kuhusu pato la Taifa (GDP), Dk. Chuwa amesema, matokeo ya ukuaji wake ni asilimia 5.3, kutokana na majanga yanayoendelea kutokea duniani, hususan athari za vita kati ya Urusi na Ukraine.

"Matokeo tuliyofanya yalituonyesha GDP itakuwa kwa asilimia 5.3 katika robo ya mwaka, lakini tuna sera ya kufanya marejeo kulingana na global crisis ambapo tumepata maotekeo ya asilimia 5.2, lakini Machi 2023 tutajua kama tumebaki kwenye matokeo yaleyale," alisisitiza.
 
Ukitaka ona Kilimo ni hasara nenda masokoni

Maembe
Mananasi
Maparachichi

Yamejazana hakuna pa kuyauza maana viwanda vyanunua kwa bei ndogo sana

Perishables ni hasara kwa Tanzania maana umeme ni ghali hivyo mtu hawezi tumia mbinu ya kuhifadhi kwa umeme
 
Back
Top Bottom