Kati ya Wanaume na Wanawake nani mabingwa wa kuharibia wenzao maisha?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Kwema wakuu!

Kama swali linavyoeleza.
Kwa upande wangu naona sisi wanaume ndio mabingwa wa kuharibia wanawake maisha. Kwenye wanawake kumi basi tisa wameharibiwa maisha na wanaume.

1. Kutia mimba na kutelekeza.
2. Kuwafanya tegemezi na kuzima ndoto zao. Hii inawafanya wanawake kuwa watumwa na bendera fuatana upepo.
3. Kuwanyanyasa kihisia kwa kuoa Wanawake wengi.
Mambo hayo matatu yameharibu maisha ya wanawake wengi Mno. Na yote mhusika ni mwanaume.

Wanawake wengi maisha yao yameharibiwa na wanaume kwa kuwapa imani na hisia wanaume wabinafsi.
Ingawaje wanawake wengi ni wabinafsi lakini uchunguzi wangu unaonyesha asilimia kubwa ya wanawake mioyo yao hugeuka na kuwa mibaya baada ya kuumizwa na wanaume wao wa awali.

Kwa maoni yako unafikiri nani kati ya mwanaume na mwanamke anayeharibu maisha ya mwenzake?
 
Wanaume. Ndio maana akitia mimba mwanafunzi anaenda jela mwanamke anabaki.


Mwanamke anafanya mambo yake kwa kukopi kwa aidha mama yake au mume/mwanaume wake, sasa akikopi kwa mwanaume jambazi anajifunza ujambazi siku akimuacha anamuacha na roho ya ujambazi, atakaechinjwa ni anaefuata. Yaani unaweza ukalipa gharama kwa makosa aliyofanya mwanaume mwenzio!
 
Kaka kweli leo unadiriki kusema wanaume ndo huaribu maisha ya binti wakati kila siku wanaume huchukua mabinti kibao wenye maisha mabovu na kuamua kubeba mamizigo yake yote kwa jina la #NIMEOA

Kaka fanya tafiti ni kwanini vijana wanachanganyikiwa na maisha na kuamua kupita njia sizo ili kujipatia fedha na umaarufu utaona dharau za wanawake nyuma zinazompa kijana hasira ya kutafuta kama kichaa ili aje kuwapa hao wanawake.

Visa vingi vya mapenzi na wanaume kwenda jela kwaajili ya kuua au kujeruhi kwa sababu ya wivu wa mahusiano kutokana na wanawake kutokuwa waaminifu.

Umesahau kwamba wanaume wanakufa mapema mno kwaajili ya depression na magonjwa ya moyo kwaajili ya haohao

Vipi kuhusu magonjwa ya zinaa ambayo kiuhalisia mwanamke mmoja anaweza kuambukiza hata wanaume 10 kwa mkupuo ndani ya siku tatu kutokana na kutakwa kwake kwa wingi wa wanaume hao

Vipi kuhusu ndoa ikivunjika nani huumia zaidi katika mgao wa mali?

Leo tutaongea kwa kujifanya tunakemea vitendo vya ushoga na hata hao wanawake utawasikia wakisema "Eeh Mungu aniepushe uzao wangu mwanangu wa kiume asiwe shoga" lakini ndo utawakuta vibarazani na kwenye mashughuli wakibueudika na haohao mashoga.

Acha hilo, Nenda kwa waganga kafanye survey uone Kati ya Mwanamke na mwanaume nani anaongoza kumloga mwenzie.

Kaka tazama wanawake wametufanya tumekuwa watumwa wa ngono, Ngono imekuwa ngumu kuepukika maana kila ukiscroll kwenye page za mitandao ya kijamii utawaona wakiwa kama walivyozaliwa na huku namba ya cm wakikuwekea kwenye bio zao

Kaka ... ebu niache tu usiseme wala
 
1.Kutia mimba na kutelekeza -Hapa nakubaliana na wewe,ila ni kwa wanawake waliobakwa tu,hawa wengine wanajiharibia wenyewe kwa tamaa zao na uzembe wao.Condom hawazioni p2 hawazioni?
2. Kuwafanya tegemezi na kuzima ndoto zao. Kama alikuwa na kazi yake huwezi kumwachisha eti kwasababu kaolewa na wewe ataendelea na kazi yake,Hawa wengine ndoto zao zilishazima tangu wakiwa kwa wazazi wao ndoa ndio ikawa nusra yao.
3. Kuwanyanyasa kihisia kwa kuoa Wanawake wengi - Hata wao wanakuwa na wanaume weeengi wasiojulikana na wanao uwezo hata wa kutubambika watoto.
 
Sikufahamu kabisa ila naweza kuotea kuwa imetoka kwenye familia ambayo mama ana sauti sana kuliko baba, au familia ya single mother, au familia ambayo umelelewa na kukulia sana upande wa ukoo wa mama yako zaidi.

Hili linajidhihirisha kwa namna unavyojenga hoja zako kwa kuforce kueleweka au kukubalika kuwa unajua sana na kuelewa wanawake kushinda wanaume wote.

Hapa kwa kifupi unachofanya tunaita unasell out kwa wanaume wenzako au tutumie neno common wewe ni simpleton so unasimp.

Wanawake hawavutiwi na wanaume wanaonyesha udhaifu wa hoja kama wewe maana hata wao mwisho wa siku wanajua wanafanya mambo mengi kwa kukosea na wanategemea wanaume tushike nafasi zetu kwenye kuwaongoza.

Huwezi ongoza watu ambao unafanana nao upeo wa kifikra. Wanaume wana namna yao ya kuona mambo tofauti na wanawake. Huu mtazamo wako ni wakike na umechemka sana.

1. Mwanamke habebi ujauzito wa mwanaume ambaye hajataka kuzaa nae hata siku moja. Ukisema wanaume wanapachika mimba na kukimbia hapo umeongelea upande m'moja tu wa hii situation. Upande wa pili yupo mwanamke asiye wajibika na maamuzi anayofanya. Unabebaje ujauzito wa mwanaume ambaye hajakuposa, hajaja kujitambulisha kwenu, hakuna urasmi wa mahusiano yeye anabebaje mimba? Halafu ndipo wanakuja watu kama wewe na kuwakingia kifua kuwa sio kosa lao bali ni la wanaume huo ni upumbavu tu wa kukosa mshipa wa aibu na kuongea vitu ambavyo havina mashiko.

2. Unapozungumzia ndoto za mwanamke ni zipi hizo? Ndoto za kuwa boss lady ambazo huwa hazitimii? Waulize hapa wanawake ndoto zenu ni zipi na huwa zinaishia kuwaacha mazingira yepi utaelewa vema namna umepuyanga na hii hoja yako.

Hivi nje ya maisha ya ndoa mwanamke ana maisha gani? Naomba tu wewe utuelezee kwa kina kwamba mfano binti aamue kuachana na maswala ya Ndoa then aanze sasa kuhangaika na ndoto zake huwa mwisho inakuja kuwa vipi? Mwanamke ana muda mfupi sana wa umri kati ya miaka 16 hadi 29 kucheza kadi zake vema. Akivuka tu huo muda tayari anakuwa chizi fresh na huko nje atakutana na kila aina ya majanga, kuanzia kuzaa na wanaume za watu, kukutana na wanaume reject, kuwa na high body count, kuzaa na watu ambao hana future nao, kuwa single mother, stress, matatizo ya akili, magonjwa yasiyo ya kuambikiza kama kisukari na pressure, etc. Yote kwaajiri ya nini sasa?

3. Jambo usilolijua kuhusu wanawake ni kwamba hawajaumbwa kudeal na mwanaume pekee yao. Yaani mwanamke m'moja hawezi ishi na mwanaume pekee yakw bila msaada wa wanawake wenzake. Kinachofanya hili jambo lionekane ni geni ni mataifa ya magharibi na ideologies zao kuaminisha jamii yoyote kuwa mwanaume m'moja huwa na mwanamke m'moja tu na ndio mapenzi ya kweli. Hiyo si kweli.

Ushahidi wa kuwa mwanamke hajaumbiwa kuishi na mwanaume pekee yake ni kwenye maeneo yafutayo.

> Wanawake hawawezi kuridhika kingono hadi wakutane na mwanaume mzoefu anayejua trick za kila aina za namna ya kumpa mwanamke raha. Hii experience mwanaume anapata wapi akiwa na mwanamke m'moja tu?

> Wanawake ndani ya siku 30 hutumia siku tano na zaidi kuingia period, kuna siku hatokuwa sawa kihisia, ubusy wa majukumu ya familia, uchovu na kadhalika. Hizi vitu kwa ujumla wake vitamtaka mwanamke ndani ya siku 30 kuwa na ufanisi mdogo sana kitandani. Sasa jiulize ni mwanaume gani ambaye ni rijali atakaa na mwanamke siku 30 za kila mwezi na kuwa na siku labda 5 tu za kupata full attention ya mkewe ili kufurahia mahaba?

> Mwanamke anabeba ujauzito miezi 9 na anahitaji kufocus na mtoto kwa muda wa miaka siyopungua 3 ndipo anaweza rudisha akili kwa mumewe. Mwanaume gani ataweza vumilia kuona anatengwa kihisia kwasababu za kihalali kabisa za malezi ya mtoto?

> Tafiti zinaonyesha wanawake hawajui wanalotaka na hivyo kuongozwa ndio tiba ya hilo tatizo. Kukiwa na mfumo rasmi wa kijamii na makubaliano, inawezekana kabisa wanawake 6 kukaa na mwanaume m'moja na wakatulia na kuishi na kufanya maendeleo bila shida. Ila kasumba ya kutoshare mume ambayo inatengenezwa na wazungu ndio chanzo cha mivutano kwenye ndoa za waafrika ambao sio asili yetu kuoa mke m'moja tu, wake ni kuanzia 6 hadi 12.

Jidanganye kuwa wanawake wanaumia hisia kuona mwanaume wake ana mwanamke au wanawake wengine. Kinachokuwa kinampa machungu mwanamke hapo ni kuwa hakuna mfumo rasmi unaolinda maslahi yake na watoto alipata na mwanaume wake, anahofu anaweza pinduliwa dakika yoyote na kupokonywa mali za mumewe. Ila walikaa nyumba moja na kushare matunzo ya mume utaona wanatulia na watamtii tena sana huyo mwanaume.

Sheria ipitishwe tu jamii ibadili mitazamo utaona wadada watakavyogombania uke wenza tena wa kuishi nyumba moja bila kelele zozote. Hapa sasa hivi wanajishaua sababu wanapata maslahi fulani fulani nje ya ndoa ndio maana.


Naona umeamua kuwa mpotoshaji kwa kuvu zote. Nimekushusha sana vyeo.
 
Hiyo hoja ya wanaume kutelekeza mimba inatosha kuwapa kombe

Unyanyasaji wa kijinsia kama kupigwa, kubakwa, waathirika wakubwa ni ke, wanaonewa na me

Hakuna kitu ke wanaweza tufanyia ambacho sisi tunashindwa kuwafanyia pia kasoro kutukausha damu

Nimeweka hoja zangu bisha kwa hoja me wengi humu ni wajinga ooh 'feminist' ooh 'simp' mnataka kila kitu kihusu wanaume
 
Kwema wakuu!

Kama swali linavyoeleza.
Kwa upande wangu naona sisi wanaume ndio mabingwa wa kuharibia wanawake maisha. Kwenye wanawake kumi basi tisa wameharibiwa maisha na wanaume.

1. Kutia mimba na kutelekeza.
2. Kuwafanya tegemezi na kuzima ndoto zao. Hii inawafanya wanawake kuwa watumwa na bendera fuatana upepo.
3. Kuwanyanyasa kihisia kwa kuoa Wanawake wengi.
Mambo hayo matatu yameharibu maisha ya wanawake wengi Mno. Na yote mhusika ni mwanaume.

Wanawake wengi maisha yao yameharibiwa na wanaume kwa kuwapa imani na hisia wanaume wabinafsi.
Ingawaje wanawake wengi ni wabinafsi lakini uchunguzi wangu unaonyesha asilimia kubwa ya wanawake mioyo yao hugeuka na kuwa mibaya baada ya kuumizwa na wanaume wao wa awali.

Kwa maoni yako unafikiri nani kati ya mwanaume na mwanamke anayeharibu maisha ya mwenzake?
Mkuu unawajua wanawake kweli ndugu yangu?

Kama huwajui ipo hivi.

Jiulize kwanini wanawake tunawaita ""hawa viumbe..."" Utapata jibu
 
Dini ya kikristo imewaaribu wanawake kuwaaminisha mwanaume anapaswa kuwa na mke mmoja .

Wakija kugundua uhalisia wanashindwa kukabiana na ukwel .

Kwenye hivyo vingne naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom