Idadi ya Wanaume duniani ni kubwa zaidi kuliko ya wanawake

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,625
22,277
Hii ni taarifa maalum kwenu wadada wote mliojikatia tamaa kwamba hamuwezi kuolewa kisa wanaume ni wachache kuliko wanawake.

Ni wakati sasa wa kuachana na huzuni kisa umekosa mwanaume wa kukuoa. Ukweli ni kwamba wanaume ni wengi kuliko wanawake.

Ikiwa kuna idadi kubwa ya wanawake kuliko wanaume katika eneo au nchi yako, hiyo haioneshi ukweli wa kimataifa. Kwa idadi kubwa kama hii duniani ya wanadamu 8,118,835,999, kulingana na takwimu, Wanaume : wanawake = 1 : 1.

Kuna wastani wa..
wanaume 4,079, 164,815 na wanawake 4,039,671, 184 duniani. Hii inawasilisha 50.24% ya wanaume na 49.76% ya wanawake kwa idadi ya watu duniani. (U. N World Population Prospects 2024).

Katika nchi kama China, India, Saudi Arabia, UAE na Oman, wanaume ni wengi kidogo kuliko wanawake. Katika nchi nyingi za Ulaya Mashariki na Afrika Kusini mwa jangwani la Sahara wanawake ni wachache zaidi kuliko wanaume.

Uwiano wa asili wakati wa kuzaliwa kwa wavulana : wasichana = 107 : 100
Lakini wanaume wana muda mfupi wa kuishi kutokana na sababu mbalimbali za kijamii. Hivyo basi ikiwa wewe ni bachelor tambua kuwa maisha ni mafupi hivyo ni vyema ukajipatia popote duniani mwenza wako mapema kabla hajafa.

NB tunaishi katika global village unaweza kujipatia mwenza wa kukuoa popote pale duniani, wanaume ni wengi sana.

Ubarikiwe.
 
Sawa mkuuu
FB_IMG_1713506520150.jpg
 
kambi ya Fisi acha kuwapa moyo watu kwa nchi kama Tz wanawake ni wengi ata ukifanya Observation research utagundua wanawake ni wengi na pia hakuna uhusiano wowote ule kati ya uwingi wa wanaume na wanawake kuolewa
Na kama kungekuwa na uhusiano kati ya uwingi wanaume na Ndoa Basi wanawake wote wenye sifa za kuolewa wangekua tayari washaolewa.
 
Takwimu za kupika ,hapa nilipo naangalia ..Ofisini mwaka jana watu kama saba walipata watato ila wawili tu ndio wamepata wa kiume... Ukweli mchungu wanawake ni wengi nenda hospital pale kaangalie uone ..
Takwimu za mama Anna Makinda hizo zinahusu bongo pekee ni kweli wanaume ni wachache bongo, Ila tukienda kimataifa takwimu zinaonesha wanaume ni wengi sana kuliko wanawake.
 
kambi ya Fisi acha kuwapa moyo watu kwa nchi kama Tz wanawake ni wengi ata ukifanya Observation research utagundua wanawake ni wengi na pia hakuna uhusiano wowote ule kati ya uwingi wa wanaume na wanawake kuolewa...
Mie nawachochea waruke kimataifa kuna wanaume wengi huko kuliko Tanzania.
 
Back
Top Bottom