Njia moja rahisi ya kukumbana na deals kubwa hapa Afrika, ikiwemo kwetu Kenya na pia hata Bongo ni kama ukifanya kazi on sub-contractual basis. Ni vigumu kwa programmer akiwa mwenyewe kupata deals kubwa hususan za kiserakali maana lobbying ya manyang'au huwa kali sana na deals hazipokezwi kwa kufuata sifa.
Kawaida mimi huachia makampuni yashindane kupata deal halafu wenyewe wananijia nifanye implementation kwa kunipa kandarasi ya sub contract. Unawacha wanaandika winning proposal kwa tender, wanafanya lobbying balaa maana serikali na makampuni makubwa wanataka kuona proposals za kiajabu ajabu zenye kuonyesha watendaji wa kampuni wenye masters degrees na mambo makubwa ambayo hata hayahusiani na mradi wenyewe.
Sasa kampuni ikishinda, wanasaka programmer ambaye ataongoza implementation na shughuli inafanyika. Humu siwezi kutaja baadhi ya miradi ambayo nimetekeleza, lakini kwa kifupi nimehusika katika very top projects za kiserikali na mashirika binafsi.
Usiku huu wa leo hapa nafanya coding ya system ambapo nipo hotelini, nimekuja na wafanyi kazi 20 wa wizara fulani ambapo nipo nawapa darasa ya system fulani ambayo nimewatengenezea. Tutaishi hotelini humu siku 30 kila siku tunapitia system nikiifanyia maboresho kulingana na mapendekezo yao. Ni system nimeitengeneza ndani ya miezi sita.
So kwa kifupi, nawashauri madogo ambao wanataka kuingia kwa fani hii, wajifunze IT in general ndani na nje, halafu kisha wakomae na programming. Kazi zitawafuata tu... zipo, programmers ni wachache kwenye nchi zetu hizi. Tatizo wengi wanataka shortcuts, anajifunza programming language kwa mihemko na kujiita programmer.
Programming is a lifestyle, it's a way of life...ukianza inabidi ubadilishe maisha yako kabisa, unakua boring kwa marafiki maana huna muda wa kwenda kucheza cheza pool table kitaa.