Labda hujanielewa, naomba urudie majibu yangu yote taratibu na utapata picha nzima ya nini ninachokisema. Fahamu kwamba chuo hakikufanyi uwe programmer, uwezo wa kuwa programmer ni juhudi zako mwenyewe. Ujifungie chumbani na kuyasahau ya dunia, wewe na vitendea kazi vyako hadi kieleweke.
Wapo watu wengi wenye shahada za sayansi ya kompyuta lakini kuandika software inakua shughuli, wamejaa nadharia tupu. Nilichokisema ni kwamba baada ya chuo kukuandaa kwenye mambo muhimu ya msingi, unafaa kuanza kutia bidii na kuhakikisha umekua programmer mwenyewe.
Wapo programmers wazuri ambao hawakupitia chuoni, lakini kila mmoja atakuambia ilibidi atumie nguvu nyingi sana ili kufanikiwa. Hivyo kama unao uwezo wa kupitia chuo, nenda kasome kwanza, lakini kama uwezo huo haupo, usikate tamaa, komaa, tafuta videos, download vitabu, andaa mazingira chumbani, jifungie ndani kitaa, ingia kwenye online forums za programmers, husika katika mijadala, pambana tu na kitaeleweka.