Kati ya Programmer na I.T

Kati ya Programmer na I.T

fundi makenika...
I know yote ni mahindi lakini naongelea unga wa dona na sembe ni upi unaolika na watu kwa sana???
Umenipata?
Hahaha, ulichouliza Sio kati ya unga wa mahindi na sembe kipi kinalika zaidi?
 
Yeah huwa nashauri bora upate darasa kamili ya IT kwa ujumla halafu ndio baadaye uchague fani moja ya kukomaa nayo kama vile programming.
Mimi hapa nilifuata CCNA, A+, N+ nakadhalika kabla nije kutulia kwa coding, na hakika ujuzi wangu wa IT in general umenifaidi sana kwenye masuala ya programming. Kuna mambo yanakuibukia na kama hukua umejiandaa vizuri kwenye hayo ya IT general, unapgwa chini. Hususa kama umekumbana na network programming.
Network programing hii ndo kitu gan tena hii???
 
ivi kuna utofauti kati ya mtu anaesoma bachelor of science in ICT na bachelor of science in IT
Hakuna tofauti ni sawa wanafunzi mwingine katumia majina mawili na mwingine katumia majina matatu katika usajili
 
Habari,
Aisee niende kwenye swali,
Ivi kati ya Programmer na IT yupi mwenye fursa nyingi za kujiajiri na kuajiriwa, na endapo wataajiriwa yupi ambae atapokea kiasi kikubwa cha mshahara kupita mwenzake???
cc. Chief-Mkwawa mchambawima1 MK254 snipa Isac M Barbarosa Na wengineo
IT anafahamu programming lakini kwenye swala la kuprogram ndo pagumu apo lakini programmer anatakiwa asiogope kucode na pia aweza kusolve matatizo katika jamii kwa kupitia code
 
Una inspire una motivate una kila kitu..yani mtu akisoma majibu yako Hukatishi tamaa unatoa Fact za kweli bila kuweka negetivity ndani yake..yani una encourage mpk mtu hujutii kutamani kua programmer au It coz hamna mahali umeegemea.

Bravo MK254 tUANZE HESABIA 2018..KUFIKA 2025 ntakutafuta..and this is A promise.

THANX.
 
Njia moja rahisi ya kukumbana na deals kubwa hapa Afrika, ikiwemo kwetu Kenya na pia hata Bongo ni kama ukifanya kazi on sub-contractual basis. Ni vigumu kwa programmer akiwa mwenyewe kupata deals kubwa hususan za kiserakali maana lobbying ya manyang'au huwa kali sana na deals hazipokezwi kwa kufuata sifa.

Kawaida mimi huachia makampuni yashindane kupata deal halafu wenyewe wananijia nifanye implementation kwa kunipa kandarasi ya sub contract. Unawacha wanaandika winning proposal kwa tender, wanafanya lobbying balaa maana serikali na makampuni makubwa wanataka kuona proposals za kiajabu ajabu zenye kuonyesha watendaji wa kampuni wenye masters degrees na mambo makubwa ambayo hata hayahusiani na mradi wenyewe.

Sasa kampuni ikishinda, wanasaka programmer ambaye ataongoza implementation na shughuli inafanyika. Humu siwezi kutaja baadhi ya miradi ambayo nimetekeleza, lakini kwa kifupi nimehusika katika very top projects za kiserikali na mashirika binafsi.
Usiku huu wa leo hapa nafanya coding ya system ambapo nipo hotelini, nimekuja na wafanyi kazi 20 wa wizara fulani ambapo nipo nawapa darasa ya system fulani ambayo nimewatengenezea. Tutaishi hotelini humu siku 30 kila siku tunapitia system nikiifanyia maboresho kulingana na mapendekezo yao. Ni system nimeitengeneza ndani ya miezi sita.

So kwa kifupi, nawashauri madogo ambao wanataka kuingia kwa fani hii, wajifunze IT in general ndani na nje, halafu kisha wakomae na programming. Kazi zitawafuata tu... zipo, programmers ni wachache kwenye nchi zetu hizi. Tatizo wengi wanataka shortcuts, anajifunza programming language kwa mihemko na kujiita programmer.

Programming is a lifestyle, it's a way of life...ukianza inabidi ubadilishe maisha yako kabisa, unakua boring kwa marafiki maana huna muda wa kwenda kucheza cheza pool table kitaa.
Umenipa mwanga hapa nilikuwa gizani sana
 
Nitakujibu kwa maneno machache maana umeniita.
Binafsi nilizunguka mjini sana nikiwa muda mwingi nimefulia kipindi nafanya kazi general za IT kama vile computer and printer repairs, networking n.k.

Lakini baadaye nikaamua kukomaa na programming. Yaani sijajutia kwangu mimi kuwa coder. Inalipa na pia ina watu wachache maana wengi huanza kwa mihemko halafu wanaishia njiani. Lazima uwe na moyo wa chui, nguvu za simba na mvumilivu kama nyoka ili ufaulu kwenye taasisi ya programming.
Kubali kuwa chizi mwenye uwezo wa kufanya coding week yote huku unalala masaa machache sana.

Ukiwa na passion ya kihivyo utakua bingwa na kazi zitakufuata, wateja watakufuata, hutotaka kuajiriwa na mtu.
Vipi kuhusu anayetaka kujifunza Data analysis/Data science.Je naye atahitaji kwanza kuwa programmer au kujifunza lugha ngapi ukiitoa lugha ya PYTHON.
 
Nitakujibu kwa maneno machache maana umeniita.
Binafsi nilizunguka mjini sana nikiwa muda mwingi nimefulia kipindi nafanya kazi general za IT kama vile computer and printer repairs, networking n.k.

Lakini baadaye nikaamua kukomaa na programming. Yaani sijajutia kwangu mimi kuwa coder. Inalipa na pia ina watu wachache maana wengi huanza kwa mihemko halafu wanaishia njiani. Lazima uwe na moyo wa chui, nguvu za simba na mvumilivu kama nyoka ili ufaulu kwenye taasisi ya programming.
Kubali kuwa chizi mwenye uwezo wa kufanya coding week yote huku unalala masaa machache sana.

Ukiwa na passion ya kihivyo utakua bingwa na kazi zitakufuata, wateja watakufuata, hutotaka kuajiriwa na mtu.
Mkuu MK254 kumbe we ni coder.Nilijua utakuwa mjaluo wa kwenye mtaa wa mabanda,kibera
 
Programmer ndiye anaendesha Dunia kwa sasa. Software zote zinaandikwa na yeye. Michongo ya Hela ipo nje nje kwa programmer. Kibongo bongo programmer mzuri hatafuti kazi Bali kazi zinamtafuta.

Coding ni kama kipaji yaana uwanjani wapo wachezaji wengi wanaojiita I.T ila akina Lionel Messi, Mbappe na Ronaldo ni macoder ambao ni wachache.

N.B
Kuwa coder ni lazima uwe na akili na unajua kufikiria vizuri. Programming haifundishwi darasani.
 
Vipi kuhusu anayetaka kujifunza Data analysis/Data science.Je naye atahitaji kwanza kuwa programmer au kujifunza lugha ngapi ukiitoa lugha ya PYTHON.

Sijui vipi bora ila haya makitu ukiwa na background ya coding huwa yanatiririka tu yenyewe, ukianzia kujipa ustawi kwenye programming na ikakukaa vizuri, hayo mengine hayawezi kukupa tabu.
 
Hizi ndio mada za kujadiliwa vijana wanao taman kujinyanyua kimaisha,much like Kwa wadau wote Wanao peperusha ujuzi wao kusaidia wengine wenye uhitaji.
 
Back
Top Bottom