Uzi wa matukio mbalimbali kwenye maisha ya ndoa

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari za wakati huu

Moja kwa moja niende kwenye mada husika maana huu uzi nitaleta na utajumuisha matukio mbalimbali kwenye maisha yetu ya ndoa.

Moderators msiuchanganye wala kubadilisha title ya huu uzi acheni usimame wenyewe watu wapate kujifunza changamoto mbalimbali zilizopo kwenye ndoa zetu.

Visa ni vya kweli kabisa na vimetokea

AMZUSHIA MKEWE KIFO KISA MCHEPUKO

Kuna huyo jamaa mmoja alipata mchepuko kazini ambaye alikuwa ni pisi kali kuliko mke aliyezaa naye.

Basi bila kuchelewa akamtongoza binti akakubali basi akamdanganya yule mchepuko kwamba mkewe amefariki kifo cha uzazi na amemuachia mtoto alee ila ameajiri mwanamke ili amlee (mkewe wa ndoa)

Basi siku moja akamchukua huyo mchepuko kumpeleka kwake anapoishi wakati huo mkewe yupo nyumbani walipofika mke kawapokea jamaa kamvuta mkewe nje akamwambia huyo ni mchepuko wa rafiki yake ameamua amsitiri ili mke wa rafiki yake asishtuke.

Kufika usiku jamaa akamfukuza mkewe nyumbani akamwambia aende kwao yeye hamtaki sababu ndugu zake hawamtaki ana dharau na kiburi.

Asubuhi sana mume kaenda ukweni akiwa barabarani akaanza kutukana na kuwaambia wakwe zake hamtaki mke wake sababu kwao hawamtaki.

Ule usiku mkewe akaenda kwa mjomba wa mume kushtaki na kuomba nauli aende kwao usiku huo huo akapewa nafasi akalala asubuhi mke akafichwa mumewe akaitwa akajitetea ni ugomvi wa kawaida tu.

Yule mchepuko sasa ndio akaenda kutangaza kazini kwamba jamaa ni mume wake na atamuoa na amekubali kulea mtoto aliyemkuta ili kupunguza gharama za kumlipa mfanyakazi.

Hapo ndipo siri ilipofichuka uzuri mkewe hajui kama kazushiwa kifo cha uzazi na mumewe sababu ya mchepuko..

Ikabidi jamaa tumuweke kikao jinsi ya kudeal na michepuko.

MKE AKIZAA TU ANACHWA

kuna huyo mwingine yeye anawatoto sita kwa wanawake 5 tofauti yani mkewe akizaa tu talaka inamuhusu

Mke wa kwanza huyu ni wa Tanga alimuoa alipozaa nae tu akapewa talaka Mtoto akiwa na miezi 3 tu akaoa mwingine wa Tabora.

Huyu wa Tabora naye alipozaa tu talaka hii hapa akamrudia yule wa Tanga naye aliposhika mimba nyingine na kuzaa kafurushwa na mabegi yake akavuta mali ya Singida.

Wa Singida wakaishi kama miaka 2 hivi akawa anamlazimisha azae alipozaa tu talaka hii hapa.

Akaoa mwingine mluguru mwaka mmoja tayari ujauzito alipozaa nenda kwenu sikutaki tena.

Baada ya hapo akaoa mke kutoka Lindi huko sisi mashemeji ikabidi tuingilie kati kumshauri mwanamke asizae kwanza kweli wakaishia wote miaka takribani 7 kaja kuzaa mwaka jana hapa nimekutana naye juzi ananiambia kaambiwa kodi ikiisha atafute pa kwenda na mwanae.

DADA MDOGO WAKE NA MUMEWE

Baada ya mkewe kujifungua kwa upasuaji Salimu akaamua kumwambia mkewe amlete mdogo wake amsaidie kulea mwanae basi mdogo mtu akaja maisha yakawa yanaendelea

Kama mjuavyo nyege mbaya mdogo mtu akapata bwana mtaani akawa anakula mali kwa vificho sana.

Siku moja mke wa Salimu aliingia kazini usiku akamuacha mdogo wake na mwanae naye Salimu akaenda kazini akaahidi atachelewa kurudi.

Kumbe mke wa Salimu hakwenda night shift bali kaenda kwa mchepuko naye shemeji yake Salimu akaenda kwa msela anayekula mali akalale huko akaenjoy vizuri. Salimu naye akaenda kwa mchepuko wake coz mkewe hatokuwepo usiku huo mtoto akaachwa ndani peke yake.

Siri ikafichukaje
Msela anayekula shemeji yake Salimu akaomba geto kwa rafiki yake kuepusha maneno ya watu kumbe iyo nyumba ndio kapanga mchepuko wa Salimu.

Salimu akiwa kwa mchepuko wake akamuona shemeji yake usiku saa 4 anaingia kwa msela akawahi kwake akakuta mtoto yupo peke yake akaona bora aende kazini kufika akasubiri hadi asubuhi watu wanatoka kumuuliza rafiki wa mkewe anamwambia mkewe kachukua ruhusa mumewe yaani Salimu anaumwa kampeleka hospitali.

Kurudi nyumbani anawakuta mtu na mdogo wake wote wapo kilichotokea ugomvi uliamuliwa kwa mwenyekiti na kamati yake.

ACHOMA MOTO CV ZA MKEWE ASIOMBE KAZI

Kuna bodaboda mmoja alizichoma moto cv za mkewe ili asiende kuomba kazi kwenye kiwanda fulani kwa kisingizio huko atapata wanaume wengine.

Huo usiku zilipigwa ngumi za hatari na hadi sasa hivi hawaishi wote.

Kama unakisa chochote share nasi ili tupate kujifunza na kujua jinsi ya kuikwepa hiyo mishale

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
IMG_0055.jpg
 
JAMBAZI AMFUMANIA MKEWE NA KUMTAJA MCHEPUKO WA MKEWE NI JAMBAZI MWENZIE:

Jamaa mmoja alioa ila hawakua wamezaa bado, mke aliambiwa mumewe ni dereva wa magari makubwa hivyo husafiri mara kwa mara kumbe bwana yule ni jambazi tena sugu,
Mke akawa ana mchepuko wake wa kujipozea mumewe akisafiri,

Siku ya tukio, mume kaaga kama kawaida anaamsha ngoma inaenda Congo kama sio Rwanda, wakaagana kwa mabusu tele na ahadi za zawadi, huku nyuma mke akamuita mchepuko wake wakashinda siku nzima ndani,

Imefika usiku wa manane, mumewe anagonga mlango amfungulie, mke kwa hamaki akamuingiza mchepuko chini ya kitanda, akaenda kumfungulia mumewe anakutana na polisi kama wote huku mumewe kapigwa vibaya mno uso hautamaniki, polisi wakaingia ndani na kumuamuru mume aoneshe silaha zilipo ndio akasema chini ya kitanda kuna begi kubwa amehifadhi humo, polisi kuchungulia wanamkuta njemba anatweta, wakamvuta pamoja na begi, wakamuuliza yule mume, jamaa ni nani? Mume akajiongeza "ni mshirika mwenzangu na hizo silaha amezileta yeye kuzificha",

Jamaa akawa anajitetea yeye hajui lolote, kuulizwa mke kapatwa na kigugumizi, polisi wakakata shauri wawachukue wote pamoja na ushahidi wa zile silaha,

Utani utani mchepuko akapata kesi ya ujambazi na kumiliki silaha,

Yaliyotokea huko Segerea baada ya kukutana ana kwa ana hatujui ila mpaka sasa wanasota wote magereza.

KUMBUKA: Mume hakuwahi kujua kama mkewe anamsaliti.
Hii kiboko,hii ndo unaambiwa mshahara wa dhambi ni mauti
 
MIZINGA YA SINGLE MOTHER

Kuna single mother mmoja hapa mwanae alikuwa anaumwa basi kumpeleka zahanati wakapata dawa yingine wakaambiwa wakanunue

Akampigia simu mzazi mwenzake akaongeza cha juu kama elfu 20 hv niliumia sana hadi nikaropoko "mkatie mwanao bima unaibiwa" sijui kama jamaa alisikia ila hela yule single mother akaila na kulipia vikoba usiku mama wa mtoto kaja kunigongea twende kituo cha afya mwanae kazidiwa nimkopeshe na hela pumbavu

Kama huishi na mwanao mkatie bima kuepusha mizinga ya hapa na pale

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ya kuacha kila mwanamke akizaa ni ya kweli ninao mfano wa mnyaturu mmoja yeye alikua kila akioa mwanamke akizaa anamuacha. Anaenda kwao tena kijijini anaoa kitoto kidogo akija nako dar akikizalisha tu ndio talaka hiyo.
Ila alikuja g
Filisika maloli yake your yakapata ajali naye akafariki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom