Ukiaminiwa aminika: Kuvunja uaminifu kulivyosababisha Kifo

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,049
Kisa cha kwanza
Leo nimemkumbuka jamaa yetu fulani ambaye miaka mingi iliopita alikuwa mfanyabiashara kijana. Alikuwa akifuata mizigo Uganda na kuuza TZ. Mungu akambariki akanunua Fuso mbili za mizigo na gari moja la kutembelea.

Akajenga nyumba yake na kwa umri wake na mkoa alipokuwa, alikuwa kijana aliyefanikiwa sana kiasi kwamba kila mtu alimfahamu.

Watu aliokuwa akifanya nao biashara wakamwamini sana akawa akienda wanampa mali kauli akiuza nawalipa anachukua tena.

Lakini tamaa ya pesa ikamwingia kuna muda kachukua mali kauza pesa hakupeleka. Yule mganda akafunga safari mpaka kwa jamaa kuja kudai chake jamaa akamkataa.

Mganda akamwambia ataona kwani yeye si mjinga awe anampa mali bila kuandikishana halafu afikiri anaweza kutomlipa na mambo yapite tu.

Mganda akaondoka, muda ukapita mara jamaa akaanza kuwa kama mwehu. Akikaa ndani mara anadai eti redio inajiwasha anasikia sauti za watu wanamcheka. Mara akilala anasikia watu wanampampasa. Na alikuwa hajaoa aanaishi peke yake.

Jamaa akawa na wenge sana hana amani. Hata nyumba yake akaanza kuiogopa akawa na wenge kweli.

Baada ya muda kila mtu akaanza kusema jamaa amekuwa kichaa maana anazungumza peke yake mwisho akajiua kwa kujirusha mtoni kutokea darajani.

Kisa cha Pili
Miaka kadhaa iliopita kulikuwa na ndugu wawili, wa mwanaume na mwanamke. Mwanamke alikuwa akiishi Nairobi ambapo inasemekana alikuwa akifanya biashara ya ukahaba huku mwanaume alikuwa akiishi TZ akiwa na familia yake yani mke na watoto wake 3 huku akimlelea mtoto mmoja huyo dada yake aliyekuwa huko Nairobi.

Huyo dada wa Nairobi alikuwa akituma pesa kwa ndugu yake amjengee nyumba na alikuwa hajarudi TZ kwa miaka mingi. Jamaa kweli nyumba akaijenga na alipoimaliza akahamia.

Yule dada wa Nairobi akaanza kuumwa mara kwa mara hivyo akaamua kurejea. Kufika akawa anadai nyumba yake ndugu yake akamwambia hakuna nyumba yani wakazinguana. Yule dada wanadai alikuwa tayari mwathirika.

Akaendelea kuumwa na uchungu wa ndugu yake kumpiga nyumba kabla ya kufa alimwambia kamwe hatokaa kwenye hiyo nyumba na akafa.

Baada ya kufa yule mtoto aliyemwacha akawa ni mtu wa kutanga tanga maana uncle yake akawa hamjali tena. Ila ile familia ikakaa kwenye ile nyumba kwa muda fulani mara yakaanza mauza uza.

Yule baba akapata msala kazini akafungwa mkewe akapata bwana mwingine akaolewa. Nyumba ikabaki tupu, wakawa wakija wapangaji hawakai wanasema kuna mauza uza.

Nyumba ilibaki tupu hadi ikaanza kuharibika. Mimi nilikuwa bado dogo tulikuwa tuna tabia ya kukaa kibarazani wakati imeshakuwa kama gofu. Sijui kama leo ile nyumba ina watu maana ni zaidi ya miaka 20 sijapita pale.

Ukiaminiwa aminika.
 
Vijana wa3 mtwara waliaminiwa na mpemba wakapewa 35m wamnunulie ufuta na choroko, wakaenda sawa Baadae wakajifanya wajanja wakazila pesa,mpemba Kila akifatilia anajibiwa utumbo
Mpk dkk hii amebaki mmoja na sijui km yupo hai maana na yeye alikua anaumwa anakaa tumbo
 
Back
Top Bottom