habari wadau.
Utafiti wangu binafsi katika Kata moja inayoitwa TAMBANI iliyopo Mbagala Mbande kuna misikiti 36 ambayo imejengwa na wafadhili taasisi za kiislamu za wa Arabu na bado inaendelea kujengwa mingine.
kinachonishangaza kwa nini Wafadhili hao hawajajenga shule hata moja waislamu wasome vizuri wazalishe Ma engineer, Madaktari na wataalamu wa fani mbali mbali,
kinachonishangaza pia kwa nini wafadhili hao hawajajenga kiwanda hata kimoja ili waislamu ama raia wa TAMBANI wapate ajira waache kushinda vijiweni bila kazi waondokane na umaskini
KWA NINI MSAADA UWE KUONGEZA NYUMBA ZA IBADA TU ?
najiuliza wafadhili hao kwa nini wasijenge hata chuo cha ufundi ama cha teknolojia hata kimoja ili watu wa TAMBANI wapate mafunzo ya kitaalamu wajikomboe kiuchumi ?
kujenga misikiti sio jambo baya , ni jambo zuri kufadhili kuwajengea wananchi sehemu za kuabudia. ila nimeshangaa sana why msaada uwe kujenga misikiti tu na kuchimba visima vya kutawazia.
Tunapaswa tuwaambie wafadhili adui wetu mkubwa ni Ujinga, Maradhi na Umaskini. Vitu vya kupambana ma hawa maadui watatu ndio wanapaswa kutujengea kwa wingi.
Kutujengea Shule, zahanati na viwanda ndio ufadhili wa kweli.
Kiwanda kimoja kinafuta umaskini wa watu wengi.. kuliko kujenga nyumba za ibada kila mtaa huku waumini wanazo sehemu za kusali tayari