Kati ya wayuhudi na wapalestina nani aikalie Palestina

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
4,640
4,426
KWA miaka mingi sana dunia inaendelea kushuhudia vita kati ya wayahudi na wapalestina huko mashariki ya kati wakigombea nchi inayoitwa Palestina. Vita hii inabeba dhana ya kidini zaidi kuliko kisiasa, ina historia ndefu na Ikumbukwe kwamba eneo hili ni chimbuko la dini kuu tatu za dunia ;uyuda(Judaism) ambayo ni dini ya kiyahudi na kwa wayahudi tu,; Ukristo na Uislamu.

Dini hizi ndizo chimbuko la vitabu vikuu vitatu vitakatifu ,Torati ya wayahudi, Biblia ya wakristo na Korani kwa Waislamu hawa wote kwa asili ya utamaduni wao ,wanaitwa "watu wa kitabu" kwa maana ya Agano la kale likijumuisha Torati.

Wakati wapalestina wanadai sehemu ya Palestina inayokaliwa na wayahudi ni nchi yao ya asili waliyopokonywa na wahayudi miaka mingi sana iliyopita ,wayahudi nao wanadai ni nchi yao waliyoahidiwa na Mungu wao,Yahweh, tangu enzi za Ibrahim mwaka 1925 kabla ya Kristo(KK).

Kwa sasa vita hii imevuka mipaka ya kisiasa na kidini ,na kuwa harakati za mapambano ya kitamaduni ,kati ya utamaduni wa Magharibi unaowakilishwa na Ukristo, na utamaduni wa Mashariki ya kati ,Kwa maana ya Uislamu, haya ni mapambano kati ya Israel na Umoja wa nchi za kiislamu Duniani (OIC) ,na utamaduni wa kimagharibi kwa ujumla.

Chanzo halisi kwamba ni nani hawa Waisrael na wayahudi ,na ni nani wapalestina ? Kuna ukweli gani hadi leo ,kwamba Mungu aliwapa wayahudi nchi ya Palestina ? Ni nini hatima ya vita hii, na kwa amani na usalama wa Dunia.?

Taifa la Israel liliundwa rasmi mwaka 1948 na idadi kubwa ya wahamiaji wa kiyahudi kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Lakini tangu hapo limekuwa ikiongozwa na wanasiasa waliozaliwa nje ya Israel ,hadi ilipompata Yatzhak Rabin. Rabin alipokuwa waziri Mkuu alijaribu kupatanisha pande zote mbili na alielekea kufanikiwa .

Kabla ya kumaliza jukumu la kufikiwa kwa amani ,Waziri Rabin aliuawa, Israel imekuwa ikiendeleza vitendo vya ukatili na hasa huu mpango wake wa ujenzi wa makazi mapya 1600 ya wayahudi huko mashariki ya Jerusalem huku wakibomoa makazi ya wayahudi bila kujali kupingwa na Marekani pamoja na Umoja wa mataifa.

Toka Mwaka 2012 Israel iliendelea na ubabe na kuweka himaya ya kiyahudi kwenye msikiti wa Al-Ebrahimi ulioko Hebron na msikiti wa Bilal Bin Raban uliopo mjini Bethlehem ,bila kujali ukweli kuwa misikiti hiyo ni ya waislamu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 1500.

Ujenzi wa Sinagogi la Kharab kwenye ardhi ya msikiti wa Al Agsa ambao ni msikiti wa kiislamu wa wapalestina kwa maelfu ya miaka mingi iliyopita ulikuwa unaendelea kujengwa , ujenzi wa sinagogi hilo katika msikiti huo linahusishwa na mpango wa kutaka kuchimba handaki chini ya msikiti huo kwa lengo la kuubomoa.

Huo ni msikiti Mtakatifu ambao ndio kibra ya kwanza na ndio msikiti wa tatu kwa utakatifu kwa waumini wa dini ya kiislamu kote ulimwenguni ,na Israel wanafanya hivyo ili wao waweze kujenga kile wanachohisi kuwa ni sehemu ya wao kufanyia ibada zao.

Umoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Kitengo cha Sosholojia (UDASUSO) mwaka 2012 walishawahi kutoa tamko la kupinga na kulaani vikali mashambulizi ya majeshi ya Israel dhidi ya Palestina.
Kwa upande wa umoja wa Afrika ,wenyewe upo bega kwa bega kuhakikisha wanafikia muafaka na kupata Uhuru wa kweli na wamekuwa Washauri wazuri kuhakikisha wanakaribisha meza ya Mazungumzo kwaajili ya mzozo huu uliodumu kwa zaidi ya miaka 27 sasa.

Palestina ya kale inakadiriwa kuwa na eneo la urefu wa kilometa 640 na upana wa kilometa 130 .kuanzia karne ya 20 KK ,kikundi cha watu waliojulikana kama "Hapiru" (yaani wazururaji au majambazi, kwa lugha ya kibabeli) kwenye kumbukumbu za mashariki ya kati wanatajwa kuwa walifika eneo hilo(Anat E: Palestine before the Hebrews). Hawa, inawezekana walikuwa waebrania wanaosemekana kutokea eneo la Uru ( Mesopotania) na kuishi kwa muda kaskazini magharibi mwa himaya ya Babeli .

Tunashawishika kuamini kwamba mtume Ibrahim wa Kabila la waebrania anayetajwa katika kitabu cha Yoshua 24:20----3, ndiye alikuwa kiongozi wa koo za wahabiru( Waebrania) hao.

Inaelezwa ,Ibrahim aliishi katika mji huu wa Uru, wa Wakaldayo ( au Babeli ya kale) kisha akahamia Harani alikoishi kwa muda kabla ya kuhamia Kaanani, ambayo ndiyo Palestina, iliyokuwa ikikaliwa na wakaanani .Baadaye wahabiru walihamia Misri kutafuta malisho bora ya wanyama wao ( Mwanzo 11:13 12:10, ----13:18) na kuiacha Palestina kwa wenyeji wazawa.

Kugunduliwa kwa vibao vya maandishi ya kifalme ya farao Amenhotep wa II eneo la Tell el Amarna, Misri ya kati ,mwishoni mwa karne ya 19 ambapo vibao 350 vimeonyesha maandishi kwa lugha ya kibabeli ya karne ya 15 na 14 KK, kunatoa mwanga juu ya aina ya watu wa enzi hizo ,tofauti na tunavyofikiri.

Vibao hivi vinavyoonyesha mawasiliano kati ya Farao na wafalme mbalimbali na maafisa wa Babeli ,Syria na kaanani, ni Uthibitisho tosha kwamba watu wa nchi hizi waliweza kutembeleana kwa Uhuru kati yao Katika Uru, Babeli ,Harani ,Kaanani na hata Misri.

Walikuwa watu wa dunia ya uelewa kwani ugunduzi wao Umeonyesha kwamba mji wa Ibrahim ,Uru ulikuwa na majengo makubwa ya ghorofa ,mahakama ,Majengo ya shule ,na Maktaba kuonyesha kwamba walikuwa wasomi. Kati ya karne ya 17 au 16 KK, kundi kubwa la wahabiru liliingia Misri na huenda ni katika kipindi hiki mmoja wao Joseph ,anayetajwa katika kitabu cha mwanzo Sura ya 37---50 ,alifanywa mtawala wakati ( wahabiru ) walipotawala Misri.

Baadaye yakatokea mapinduzi Misri, ikawa chini ya utawala wa farao, wakati huo idadi ya wahabiru ilikuwa ikiongezeka kwa kasi kubwa ,akaingiwa hofu kwamba wahamiaji hao wangechukua nchi au kuiangamiza kama wangeungana na wavamizi kutoka nje katika vita dhidi yake. Kwa hiyo ,walivuliwa uraia na kufanywa watumwa ,wakatumikishwa kwa suluba na Hata kuuawa kwa wingi ,na kutokana na mateso hayo waliamua kuondoka Misri kurejea Palestina.

Mmoja wao (Nabii ) Musa, aliweza kumshawishi farao awaache huru warejee Palestina kutokana na kwamba alilelewa na Binti wa Mfalme huko Misri ( kutoka 2:1 ---10;Ebr 11:23) Ndipo Musa akaongoza watu kati ya 6000-7000( bila kuhesabu wanawake na watoto ) wa makabila ya Kiebrania ( wahabiru) kwenda nchi waliyoahidiwa na Mungu ---Palestina tangu enzi za Ibrahim.

Iliwachukua miezi mitatu kutoka Misri hadi mlima Sinai (Horebu) mahali Musa alipopewa Amri na "Yahweh" kwenda misri ,hapa ,kwa mara ya pili alipewa amri kumi na Mungu huyo za kuongoza taifa teule ( la waebrania) kama chombo cha kupeleka baraka zake kwa mataifa yote Duniani.

Kutoka mlima Sinai walielekea Kaanani ,yaani Palestina ,wakiwa wameagizwa na Mungu wao kuwafukuza na hata kuwaua wenyeji wa nchi hiyo ,walikatazwa kuwaoa mabinti wa nchi hiyo wasije wakalitia najisi kabila lao la kiebrania kwa kuabudu miungu ya kigeni ( Kutoka 30:16) badala ya Mungu wa Torati ,Yahweh.

Na ili kujua ndani ya Palestina kuna nini?na kabla ya kuingia, Musa alitumia majasusi kumi kupeleleza ,ambao walirudi na jibu la kukatisha tamaa ,kwamba ingawa ilikuwa ni nchi nzuri iliyojaa Maziwa na asili ,lakini watu wake walikuwa majitu ya miraba minne ,( Nefilia) na wao walionekana kama vipanzi tu kuweza kupambana nao ,wakasema ,bora warudi Misri kwa usalama wao.

Wawili kati yao ,Joshua na Kalebu ,waliwashawishi Waebrania waendelee kwa kuwapa moyo wa ushindi kwa kuwa "Yahweh" alikuwa upande wao ,Ndipo ukazuka mgomo na maasi wakitaka kuchagua kiongozi mwingine badala ya Musa awarejeshe utumwani Misri.

Inadhaniwa kwamba ,malalamiko ,mashaka na maasi haya hayakuchochewa na Waebrania halisi, bali waliokimbia nao kutoka Misri. Inaelezwa kwamba hapo Yahweh alichukia uasi huo hivyo badala ya kuwawezesha Waebrania kuivamia Palestina ,akawapa adhabu ya kuzunguka na kutangatanga jangwani kwa miaka arobaini (40) mpaka wote ambao walikuwa na umri wa miaka 20 au zaidi wakati wa kutoka Misri ,wawe wamekufa wote;. na kwamba hapana hata mmoja angekanyaga ardhi ya Palestina isipokuwa yoshua na kalebu ( Hesabu ,Sura ; 13---16).

Na miaka 40 ilipotimia walikuwa wamefika karibu na nchi ya Palestina ; mto Jordani tu ndio uliokuwa umewatenga na nchi hiyo, Ndipo Musa akapanda juu ya mlima Nebo ,na Mungu akamwonyesha nchi ya Palestina kwa mbali akamwambia " hii ndio nchi niliyomwahidi Ibrahim ,Isaka na Yakobo na wanao, lakini hutaingia humo" .

Musa alifia juu ya mlima Nebo wakati huo ,na jukumu la kuwaongoza Waisrael kuivamia Palestina akapewa Yoshua ,Baada ya kuvuka mto Jordan ,wakafika mji wa Yeriko ,na kuta za mji huo zikaanguka ( pengine kutokana na tetemeko) ,wakauteka bila upinzani wakakalia nchi.

Uvamizi huu wa Waebrania kwa mara ya pili ulikuwa mpango wa muda mrefu ,kati ya karne mbili hadi nne, Waebrania hawa waliteketeza uhai na mali za wenyeji ,kutoka milimani hadi kwenye mabonde na nyika. Na kwa kuwa sasa nguvu ya Wa-Palestina ilikuwa imebuniwa kwa uvamizi huu, kabila lingine la wafilisti na mengine ya baharini ambayo hapo mwanzo hayakuthubutu kuvuka makutano ya mto Nile ,yalipata mwanya wa kuivamia Palestina .

Hatari hii ilisababisha Waebrania kuunda Umoja wa kitaifa ili kujihami na uvamizi. Kwa hiyo walihitaji jemedari shupavu mwenye uwezo ,wakamchagua Sauli, (1020---1000KK) kuwaongoza katika vita dhidi ya uvamizi wa wafilisti ,ambaye alifanikiwa kuunda jeshi la kudumu ,silaha zikiwa mikuki na kombeo, hata hivyo hakuweza kufanikiwa kujenga Serikali imara ya Umoja wa kitaifa, wala kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mara kwa mara.

Daudi Alichukua utawala (1000KK) kutoka kwa Sauli ambaye alijiua kwa kushindwa vita na wafilisti ,aliweza kuyaunganisha makabila na kuanzisha utawala wa kinasaba(dynasty) uliodumu kwa miaka 400; na Yerusalem ikawa Makao Makuu ya taifa la Israel.

Utawala wake ulikuja kipindi kile kile cha kuanguka kwa falme za mashariki ya kati. Akaitumia vyema ombwe hili ya kimadaraka ( Administrative vacuum) ,yeye na Mfalme aliyefuata Suleiman kujenga utawala imara.

Kwa njia hii ,karibu miji 400 iliweza kuunganisha kuunda shirikisho la kitaifa ,jeshi la taifa likaimarishwa Kwa matumizi ya magari ya kuvutwa na farasi ( the charioty) . Daudi alifariki kabla ya kukamilisha mipango yake na mwanae Suleiman akatwala ,961---922 KK. ( Frye,R.N.: The Heritage of Persia).

Moja ya kazi kubwa alizofanikisha Suleiman ni ujenzi wa hekalu na kufanya Yerusalem kuwa makao makuu ya kidini na kisiasa , hata hivyo Kwa kupenda anasa ,uasherati na ulevi aliifilisi nchi. Na pale mwanae aliporithi utawala, ufalme wake uligawanyika Yerusalem ukafanywa mji mkuu wa ufalme mpya wa kusini ,Yuda : na Samaria ukawa makao makuu ya ufalme wa kaskazini, Israel .

Pigo la mwisho kwa waebrania lilikuja mwaka 597 KK wakati mfalme Nabukadreza wa Babeli ,aliwapoteka zaidi ya theluthi ya Waebrania na kuwapeleka utumwani nchini Babeli. Hapo ndipo falme hizo mbili zilipofikia kikomo.

Kwa vizazi viwili mfululizo ,Waebrania walitumikishwa Babeli na wakati huohuo machafuko yaliendelea huko Yudea na Israel ,Hekalu likavunjwa na kufanya dini kongwe ya Musa na manabii kufifia na hatimaye kutoweka. Wakiwa Babeli walimkumbuka Musa ,manabii na nchi yao, wakazidi kujipanga moyo kwamba " Mungu wa Israel hakubakia Palestina ,alikuwa Mungu wa Israel popote Waisrael walipokuwa. ; na sheria zake Zote " (Johnson,P. civilization of the Holy Land).

Waliendelea kusali pamoja na kwa kiburi cha ki--imani ,walikataa kata kata kuchanganyika na jamii ya kibabeli ,kama inavyoelezwa katika Zaburi137:
"kando ya mto Babeli ndiko tulikoketi ;Tukalia tulipoikumbuka sayuni ,katika miti iliyoko katikati yake, tukavitundika vinubi vyetu , maana huko waliotuchukua mateka walitaka tuwaimbie wimbo wa bwana katika nchi ya ugenini?

Wengi wanaamini Israel inalindwa na inatetewa na madola makubwa ya ulaya magharibi ambayo yanafuata siasa za kibeberu . bado inaaminika wapalestina wanateseka ndani na nje ya taifa lao kutokana na ubeberu. wengine wanaamini Israel ni wavamizi na kwamba Mungu hawezi kuruhusu watu kuua wengine tena ndani ya ardhi walizozikalia kwa muda mrefu.

Na kwamba Marekani inaonekana ni mnafiki kuendesha usuruhishi kati ya Palestina na Israel na kwamba haina tija kwa kuwa Marekani inaingia Kwenye vikao vya usuruhishi ikiwa upande mmoja na Israel. Kwamba Marekani ipo na Israel moja kwa moja katika wema na Ubaya unaofanywa na taifa hilo la kiyahudi ,kwa nguvu kubwa ya Marekani kama taifa kubwa Israel imekuwa ikifanya itakavyo huko mashariki ya kati bila kuchukuliwa hatua yoyote na jumuiya ya kimataifa.

Mwaka 2012 kwa mfano , Shirika la Sayansi ,Elimu na utamaduni la Umoja wa mataifa ,UNESCO liliiweka Palestina kama mwanachama wa umoja huo. Marekani mara moja ikatangaza kuondoa misaada yao katika shirika hilo.

Pichani chini; Rais wa Palestina, Yasser Arafat akifurahia jambo na Mwl Nyerere.
 
I
IMG-20220625-WA0023.jpg
 
Wayahudi ndio watu wa asili ya eneo la Palestine, Wapalestine ni wavamizi.
Ili kuumaliza mgogoro yafaa waungane wawe taifa moja maana wote ni watoto wa baba mmoja.
 
Wapalestina ni wafilisti nduguze Goliathi
Wao ndio walivamia Israel
Wakazi original wa hiyo nchi ni wayahudi

Taifa pekee duniani ambalo.mipaka yake ilitajwa na Mungu mwenyewe ni Israel pekee
Nchi zingine zote duniani mipaka ilichorwa na wakoloni yetu ilichorwa na Berlin Conference ya wayahudi Mungu mwenyewe alitaja mipaka yao kasome Biblia
Taifa la Israel halikuundwa 1948 lilikuwepo karne na karne. Wapalestina yaani wafilisti walivamia wayahudi wakatawanyika 1948 ndio ikaamriwa warudi nchini kwao
Wapalestina wakubali yaishe wawatambue wayahudi maisha yaendelee sababu wayahudi hawasemi wapalestina yaani wafilisti waondoke wako tayari kwa co existence wanachotaka amani na utulivu .Wafilisti wako hata upande wa Israel kuna waarabu waislamu wafilisti kibao wanaishi jiji la Nazareth mji wa Yesu alikotokea ukoo wake kule asilimia kubwa ya wakazi ni waarabu wafilisti waislamu lakini huishi kwa amani na wayahudi bila shida
Tatizo liko kwa waarabu wafilisti waislamu wa Palestina
 
... inatia faraja sana suala la nani mmiliki halali wa Ardhi ya Yakobo master plan yake imeandaliwa na kupigwa "mihuri ya moto" na Kiti cha Enzi"; hizo nyingine stori tu!

Ilivyo miujiza yule Mungu mwingine hajazungumzia "vilivyo" suala hili zaidi ya vijihabari vya kuokoteza tu. Lau angalikuwa amefanya hivyo, kwa yakini pasingekalika.

Hapana Mungu ila Mungu wa Ibrahim, na Isaka, na Yakobo ndiye Mungu.
 
natamani siku niende huko nikajionee hizi historia za kustaajabisha na kushangaza.ila Mimi nipo upande wa Palestine
 
Nasikia wapalestina waliwakaribisha kwao na kuwapa eneo wayahudi baada ya nchi zote Europe kuwakataa matokeo yake ndio hayo,kwa haya yanayotokea leo unaweza sema Hilter alikua Sawa hawa zionists wanavyoua raia bila sababu inasikitisha sana!
 
Wagogo
 
Kuna wapelestina ni waisrael na Kuna waisrael ni wapelestina... Kuna maeneo wanaishi tu mtaa mmoja🤣🤣🤣
 
Wapalestina ni wafilisti nduguze Goliathi
Wao ndio walivamia Israel
Wakazi original wa hiyo nchi ni wayahudi

Taifa pekee duniani ambalo.mipaka yake ilitajwa na Mungu mwenyewe ni Israel pekee
Nchi zingine zote duniani mipaka ilichorwa na wakoloni yetu ilichorwa na Berlin Conference ya wayahudi Mungu mwenyewe alitaja mipaka yao kasome Biblia
Taifa la Israel halikuundwa 1948 lilikuwepo karne na karne. Wapalestina yaani wafilisti walivamia wayahudi wakatawanyika 1948 ndio ikaamriwa warudi nchini kwao
Wapalestina wakubali yaishe wawatambue wayahudi maisha yaendelee sababu wayahudi hawasemi wapalestina yaani wafilisti waondoke wako tayari kwa co existence wanachotaka amani na utulivu .Wafilisti wako hata upande wa Israel kuna waarabu waislamu wafilisti kibao wanaishi jiji la Nazareth mji wa Yesu alikotokea ukoo wake kule asilimia kubwa ya wakazi ni waarabu wafilisti waislamu lakini huishi kwa amani na wayahudi bila shida
Tatizo liko kwa waarabu wafilisti waislamu wa Palestina
Nilishanga kukukosa ktk uzi huu mkuu
 
Back
Top Bottom