Kasi ya Mnyika yamtisha JK

Kasi ya Mnyika yamtisha JK

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,190
Reaction score
162,698
KASI ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), kushikia bango tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es Salaam, ni wazi jana ilionekana kumshutua Rais Jakaya Kikwete.

Kwa muda mrefu sasa, Mnyika amekuwa mstari wa mbele kupiga kelele kuhusu maji na hata wiki iliyopita aliitisha maandamano ya amani kwenda Wizara ya Maji, ili kumshinikiza kero za wananchi wa jimbo lake zisikilizwe.

Rais Kikwete, alionekana wazi kushutushwa na tatizo la maji na kutoa maagizo mazito kwa uongozi wa Wizara ya Maji, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, DAWASCO, wabunge na mkuu wa wilaya Kinondoni, wahakikishe Jumatatu ya wiki ijayo wanakutana naye Ikulu, kwa ajili ya kupanga mikakati ya kumaliza tatizo hilo.

Rais Kikwete alitoa agizo hilo jana, alipokwenda kukabidhi kituo cha kisasa cha polisi, nyumba za askari polisi na kufungua Shule ya Msingi Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Baada ya kusikiliza kero ya maji, Rais Kikwete aliwaita viongozi wa Manispaa ya Kinondoni, akiwamo Kaimu Mkurugenzi, Godfrey Mugomi na kuwahoji ni lini watamaliza tatizo la maji.

Lakini katika hali ya kushangaza, viongozi hao walishindwa kueleza mikakati yao. Hali hiyo ilionekana kumshutua na kuamua kutoa maagizo ya kuwataka wafike Ikulu Jumatatu ijayo.

"Wananchi wa Kinondoni naomba msiandamane kudai maji, nimebaini tatizo liko wapi, nawaagiza viongozi wote waje ofisini kwangu Jumatatu wanieleze mipango yao," alisema Rais Kikwete.

Pia Rais Kikwete, ameagiza kujengwa kwa bomba kutoka Ruvu Juu na Chini, ambalo litahudumia wananchi wa Dar es Salaam mbali ya miundombinu iliyopo sasa ambayo alidai imejaa udanganyifu na wizi wa maji njiani.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliagiza halmashauri ya Kinondoni kukutana na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) haraka, kwa ajili ya kutafuta fedha katika vitega uchumi na kulipa fidia ya nyumba nne zilizopo karibu na daraja la Golani, ili kuondoa kona kali iliyopo.

CCM, CHADEMA

Katika ziara hiyo, wafuasi wa CCM na CHADEMA waliokuwa wamejipanga kando kando mwa barabara, walionekana wazi kutunishiana misuli.

Wafuasi wao, waliokuwa wamevalia fulana, kofia na bendera na kuelekea kwenye daraja la Golani, linalotenganisha Kata ya Kimara Suka na Saranga, lilionekana wazi kuibua hisia kali mbele ya Rais Kikwete.

Kabla ya kuwasili Rais Kikwete, wafuasi hao walionekana kurushiana maneno ya chini chini, huku wote wakitaka kupeperusha bendera zao.

Kutokana na hali hiyo, hali ya usalama katika eneo hilo ilianza kupotea kitendo ambacho Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Jordan Rugimbana na polisi kuingilia kati na kuwasuluhisha.

Wakati Rais Kikwete, akisaini kitabu cha wageni, tafrani ilizuka karibu na jukwaa kuu, baada ya wafuasi wa CCM kutaka kuondoa viti vya madiwani wa CHADEMA.

Hata hivyo, wakati wa utambulisho shangwe zilizizima pale walipokuwa wakiwataja viongozi wa Chadema, akiwamo Mnyika na madiwani wa CHADEMA.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete ameahidi kutoa mifuko 100 ya saruji kwa kila kaya kwa wananchi waliohamishiwa Mabwepande.

Nayo Kampuni ya Home Shooping Centre, waliahidi kutoa mabati 30 kwa kila kaya, ambao ni wadhamini wa ujenzi wa makazi ya wakazi wa Mabwepande.


CHANZO:MTANZANIA
 
Wabunge wa CCM kwa kushirikiana na naibu spika waliihujumu hoja ya John Mnyika lakini wananchi wameonyesha kutoyumba, wameendelea kumuunga mkono na sasa raisi wa nchi ametambua hali halisi na kuingilia kati ili kutatua tatizo la maji.

Masnitch wote waliokuwa wanambeza Mnyika sasahivi vichwa chini kama vile wameshikwa ugoni.
 
Kasi ya Mnyika imtishe Jakaya? Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi, Makocha wa Mnyika wamelambishwa sakafu kwa Nyakati tofauti, Mbowe 2005,Slaa 2010. Kama mnadhan kuitwa Ikulu ni ishu hata Mzee Yusuph Mzimba wa Yanga Asili na Mzee Dalali wa Simba kwa Nyakati tofauti wameenda magogoni kuzungumza na Mzee, Jakaya ni wa wote bila ya kujali Itikani,dini,kabila,jinsia wala kipato Hata mateja kama Ray C washaenda!
 
Hapo rais ametambua uwepo wa CHADEMA. Nawasihi wananchi wenzangu wa Tanganyika kuwa vyama visitutenganishe na ule upendo wetu wa asili kwani vyama huja na kupita ila sisi bado tutaendelea kuombana chumvi na lifti sikuzote. Big up John Mnyika.
 
Niliona kwenye ITV bendera za CHADEMA kwenye msafara wa Rais.

Sent from my GT-I9100 using Tapatalk 2
 
Safi sana Mnyika ka kulivalia njuga tatizo la maji kwenye jimbo lako, nampongeza pia Rais Kikwete kwa hatua alizochukua kutaka kumaliza tatizo la maji, pia imedhirisha jinsi viongozi wa serikali yetu wasivyo na mipango thabiti ya kumaliza tatizo la maji, mpaka Rais anagundua kabisa kun ubabaishaji, namshauri angewafukukuza kazi hao wababaishaji ili tusonge mbele
 
inaonekana propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA haziwaingii kabisa wananchi, ni sawa na kelele za chura....
 
Kasi ya Mnyika imtishe Jakaya? Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi, Makocha wa Mnyika wamelambishwa sakafu kwa Nyakati tofauti, Mbowe 2005,Slaa 2010. Kama mnadhan kuitwa Ikulu ni ishu hata Mzee Yusuph Mzimba wa Yanga Asili na Mzee Dalali wa Simba kwa Nyakati tofauti wameenda magogoni kuzungumza na Mzee, Jakaya ni wa wote bila ya kujali Itikani,dini,kabila,jinsia wala kipato Hata mateja kama Ray C washaenda!

Kwa hiyo? :A S 39: :rockon:
 
CHADEMA innatishia uhai wa CCM, na kwa kuthibitisha hilo tunangoja kwa hamu uchaguzi wa madiwani Arusha,ubunge Igunga na Sumbawanga
 
Safi sana Mnyika ka kulivalia njuga tatizo la maji kwenye jimbo lako, nampongeza pia Rais Kikwete kwa hatua alizochukua kutaka kumaliza tatizo la maji, pia imedhirisha jinsi viongozi wa serikali yetu wasivyo na mipango thabiti ya kumaliza tatizo la maji, mpaka Rais anagundua kabisa kun ubabaishaji, namshauri angewafukukuza kazi hao wababaishaji ili tusonge mbele
It's a good idea kwamba Raisi kaliona na analivalia njuga,tatizo yeye kama yeye hawa ambao walitakiwa kufanya hizo kazi na hawakuzifanya anawachukulia hatua gani,haoni kwamba hawa ndio wachafuzi wa chama cha CCM,haoni kuwa hawa ndio watu wasiomtakia mema katika uongozi wake,ndio hapo swala la upole kwa muheshimiwa linapokuja ingawa yeye binafsi anapinga kuwa hayuko hivyo.Mimi nadhani they stiil have time for making changes kama ataamua kuwa aggressive.
 
Jk anaangalia mtu mwenye maono ccm hakuna wakushauriana nae kero za wananchi na jinsi ya kuya tatua kumtoa lowassa na january makamba na mwakyembe,waliobaki wanachojua ni matusi kwa wapinzani hata mambo ya msingi wao wanatia siasa.
 
  • Thanks
Reactions: ESI
"Home Shopping Centre"!!!???:tape2::tape2:
 
ungebadili title pale kwenye mnyika ukaweka jk na kwa jk ukaweka mnyika ningejua umemaliza japo form two
 
Hongera sana Mnyika.
Matunda ya kazi yako yanaonekana na yataendelea kuonekana.
Wakazi wa Ubungo tupo bega kwa bega na wewe.
 
Walifikiri mbinu ya kutotatua kero ya maji Ubungo ingeua upinzani, kumbe ndiyo imeongeza chuki kwa chama tawala kutokana na makusudi yao.
 
Back
Top Bottom