Kasi ya Mnyika yamtisha JK

Kasi ya Mnyika yamtisha JK

CHADEMA innatishia uhai wa CCM, na kwa kuthibitisha hilo tunangoja kwa hamu uchaguzi wa madiwani Arusha,ubunge Igunga na Sumbawanga

Bila kusahahu jimbo la Bahi, manake yule mla rushwa sidhani kama atapona, labda maccm yatumie mabavu kuyumbisha ile kesi
 
Cha muhimu ni kwamba Mnyika anafuatilia tatizo la maji na anawashirikisha wananchi. Tatizo hili ni sugu na inawezekana hata Wabunge waliopita walikuwa wanafuatilia pia lakini Dawasa na Dawasco wanaweka pamba kwenye masikio yao. Lowassa aliwaendesha sana kabla hajatoka na walianza kupata akili lakini baada ya Lowassa kuondoka wakarudi kule kule kuwa miungu watu. Tunashukuru kitendo cha kutaka kuandamana kimemfikia Rais wetu na ameamua kuchukua zigo hili la maji kwa mikono miwili. Naona akiamua kulifanyia kazi, kazi itatendeka. Tunahitaji mawaziri wa kumsaidia rais kwa kufanya kazi kwa kutumia utashi wao na sio kusukumwa. Hata swala la kisera wanalifanya la kisiasa na wanaficha kutowajibika kwao kuifanya issue inaonekana kubwa kwa sababu inafuatiliwa na Chama Cha Upinzani. Lazima ifike wakati watu wawajibike na waache uvivu na soga lisilokuwa na tija. Asante rais wangu Kikwete, kwa kulichukua swala la maji kwa uzito mkubwa. Tunaamini kikao chako cha Jumatatu kitatoa mwanga!
 
Mh. Dr. Kikwete na kule Mkoani Geita japo mbunge hasemi lakini mradi wa maji unaofadhiliwa na GGM kwa ajili ya mji wa Geita unaenda kisiasa badala ya Kiserikali.
 
This is an indication that our leaders are out of touch, how come you live in Dar ever since you were a minister and now a president yet you are not aware of the water shortage, this is absolutely ridiculous it is high time now that vetting be undertaken before entrusting some guys to higher offices.
 
Hii kali..Amestushwa na tatizo la maji Dar!!!????Kumbe muda wote huu alikuwa hajui/hajaelezwa!?

serikali sikivu, full intelijensia ya maandamano; raisi hajui tatizo la maji na mradi wa maji wa wachina!..DHAIFU
 
Siita lukolo hiyo mijitu ya ccm ilisha laaniwa. Ila tulikua wajinga wakati wa kwenda wakati wa kurudi tutakua waelevu.
Tatizo bado tuna watanzania wapo kwenye usingizi wa pono, hawana habari na hali inayotukabili hivi sasa, wanachowaza wao ni elfu kumi, tshirt na kepu wakati wa uchaguzi basi. Sema ndiyo hivyo, siasa siyo uadui, kwa hiyo inabidi tukubali tu matokeo hata kama yanauma.
 
8E9U7951.JPG
 
It's a good idea kwamba Raisi kaliona na analivalia njuga,tatizo yeye kama yeye hawa ambao walitakiwa kufanya hizo kazi na hawakuzifanya anawachukulia hatua gani,haoni kwamba hawa ndio wachafuzi wa chama cha CCM,haoni kuwa hawa ndio watu wasiomtakia mema katika uongozi wake,ndio hapo swala la upole kwa muheshimiwa linapokuja ingawa yeye binafsi anapinga kuwa hayuko hivyo.Mimi nadhani they stiil have time for making changes kama ataamua kuwa aggressive.

yaani hapa ndo alipaswa kuwawajibisha,iweje jambo dogo la maji kwenye JIMBO hadi rais aliingilie?
 
sababu Ikulu ni mali ya watanzaia...!!!ndomana hawazui watu kwenda
Kasi ya Mnyika imtishe Jakaya? Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi, Makocha wa Mnyika wamelambishwa sakafu kwa Nyakati tofauti, Mbowe 2005,Slaa 2010. Kama mnadhan kuitwa Ikulu ni ishu hata Mzee Yusuph Mzimba wa Yanga Asili na Mzee Dalali wa Simba kwa Nyakati tofauti wameenda magogoni kuzungumza na Mzee, Jakaya ni wa wote bila ya kujali Itikani,dini,kabila,jinsia wala kipato Hata mateja kama Ray C washaenda!
 
HOJA ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) kuhusiana na suala la tatizo la upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Dar es Salaam, inaelekea kupata ufumbuzi kutokana na Rais Jakaya Kikwete kumuita Ikulu mbunge huyo Jumatatu wiki ijayo.

Wengine walioitwa kukutana na rais ni Mkuu wa Mkoa, Mecky Sadick, wakuu wote wa wilaya pamoja na wabunge na wataalamu kutoka Wizara ya Maji.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa daraja la Mtaa wa Golani, Kata ya Saranga, Rais Kikwete alisema kuwa kutokana na wananchi wa kata hiyo kupiga kelele kuhusiana na suala la maji ameamua kukutana na viongozi hao ili kupatiwa ufumbuzi.

Kikwete pia alitaka kuwepo na mfumo maalumu wa mabomba ya maji yatakayojengwa kwa saruji kutoka Ruvu Chini na kuja jijini Dar es Salaam moja kwa moja bila kuchepuliwa sehemu yeyote.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alikiri kuwepo kwa wizi wa maji katika maeneo ambayo mabomba ya maji yamepita.

“Watu wasifanye ukanjanja katika masuala ya maji, mabomba yanatandazwa na watu wanaiba maji, shida inayotokea ni maji hayo kutokufika jijini Dar es Salaam,” alisema.

Alifafanua kuwa lita milioni 65 zinahitajika ili kukabiliana na tatizo la maji na kwamba upanuzi wa Ruvu Juu na Chini ujenzi wake utakamilika Julai na kutaka hatua za haraka kuchukuliwa kuhakikisha maji yanapatikana kwa haraka ili kumaliza tatizo.

Hatua ya Mnyika kuitwa Ikulu imetokana na kusimama kidete katika suala la maji ambapo Aprili 4, mwaka huu aliwasilisha hoja binafsi na kuitaka serikali kuchukua hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es Salaam hoja ambayo ili iliondolewa bungeni kibabe.
 
[QUOTERais Kikwete, alionekana wazi kushutushwa na tatizo la maji na kutoa maagizo mazito kwa uongozi wa Wizara ya Maji, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, DAWASCO, wabunge na mkuu wa wilaya Kinondoni, wahakikishe Jumatatu ya wiki ijayo wanakutana naye Ikulu, kwa ajili ya kupanga mikakati ya kumaliza tatizo hilo.][/QUOTE]

Kila kitu Rais anashtuka ama kushangazwa. Ina maana Kikwete hajui ukubwa wa taizo la maji kwa mkoa wa Dar Es Salaam ama anataka kuwahadaa wananchi.

Baada ya kusikiliza kero ya maji, Rais Kikwete aliwaita viongozi wa Manispaa ya Kinondoni, akiwamo Kaimu Mkurugenzi, Godfrey Mugomi na kuwahoji ni lini watamaliza tatizo la maji.

Kama amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka nane na hajaweza kulitafutia ufumbuzi hilo tatizo la maji, anatarajia hao watendaji watampa jibu gani kwenye ziara yake ya masaa machache.

Pia Rais Kikwete, ameagiza kujengwa kwa bomba kutoka Ruvu Juu na Chini, ambalo litahudumia wananchi wa Dar es Salaam mbali ya miundombinu iliyopo sasa ambayo alidai imejaa udanganyifu na wizi wa maji njiani

Hilo bomba litajengwa lini na kwa kutumia bajeti ipi, ama bado anaendelea kutoa ahadi alizokuwa anatoa kwenye kampeni mwaka 2010 ambazo mpaka sasa ameshindwa kuzitekeleza
 
Kasi ya Mnyika imtishe Jakaya? Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi, Makocha wa Mnyika wamelambishwa sakafu kwa Nyakati tofauti, Mbowe 2005,Slaa 2010. Kama mnadhan kuitwa Ikulu ni ishu hata Mzee Yusuph Mzimba wa Yanga Asili na Mzee Dalali wa Simba kwa Nyakati tofauti wameenda magogoni kuzungumza na Mzee, Jakaya ni wa wote bila ya kujali Itikani,dini,kabila,jinsia wala kipato Hata mateja kama Ray C washaenda!

Ndiyo walilambishwa sakafu. Lakini ninakuambia huyo kwenye nyekundu mlikwiba. BISHA
 
Back
Top Bottom