Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.

Samvulachole

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2006
Messages
414
Points
225

Samvulachole

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2006
414 225

JE HUYU BWANA MEDI MPAKANJIA inawezekana ikawa suala zima la WEIGHT likawa limemuanguasha mno.... SIJIDA KUBWA lakini anafanya mambo utafikiri MGALA bwana, mambo gani yakuenda kusemeleana kwa SPIKA....kwani BAKWATA HAPAJUI?OMARI KIMBAU mbona hatajwi?


AMINA AKIONGEA NA SPIKA...
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,874
Points
2,000

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,874 2,000
Kufuatia saka hili linaloendelea:

KLH News.... inaleta habari mpya:

a. Barua ya Mpakanjia kwa Spika ilitungwa na kuhaririwa na Emmanuel Nchimbi!

b. Bi. Chifupa hali yake (kiakili) inadaiwa si nzuri baada ya mambo haya kutangazwa, na kuna tetesi za kuaminika kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM ambao wanajaribu kumzuia binti huyo asizungumze na vyombo vya habari!


c. Chanzo kingine cha kuaminika kimetuhakikishia kuwa kuna orodha ya wabunge wa CCM (wengine kwenye baraza la mawaziri) ambao wanatembea na wabunge wengine vijana wa CCM na wale wa Upinzani kila wakikutana huko Dodoma. Ni kwa sababu hiyo basi "yeye asiyekuwa na dhambi hii, awe wa kwanza kuwatupia vijana hawa mawe!"

Maoni yangu:

Suala hili hasa ni la familia na nyumba za Chifupa, Mpakanjia na Zitto! Ingawa suala la maadili ni suala muhimu sana, maadili ya ngono (sexual morality) ni suala dogo kwa wanasiasa na viongozi. Tangu enzi za Solomoni hadi leo hii, viongozi wamekuwa wakianguka kwenye udhaifu huu kuliko kitu kingine chochote. Ni jambo linalotia aibu na kuumbua watu! Hata hivyo ukilinganisha na udhaifu huu na ule wa wizi wa mali za umma, ubadhirifu, rushwa, matumizi mabaya ya fedha nk.. suala hili la kitandani ni kiduchu kwa uzito wake!! Ni kweli jambo hili linavutia hisia na kuuza magazeti, lakini kuna mambo muhimu zaidi ambayo Watanzania inabidi wayafuatilia kuliko kutafuta nani alimvua nani chupi!! unless wakati anafanya hivyo pesa za serikali zilitumika!!
 

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Messages
4,159
Points
1,250

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2006
4,159 1,250
Bungeni Kuna Kuna Mambo Cuf Wao Waliooa Ndoa Za Kisomali Chadema Wao Wanamalizana Na Ccm, Jamani Hawa Wananchi Ndio Wategemee Nini Kwa Wabunge Hawa? Maana Tuliambiwa Ooh Wanamuziki Wabongo Hawana Maadili? Sasa Na Huku Tazameni Mambo
 

Samvulachole

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2006
Messages
414
Points
225

Samvulachole

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2006
414 225
Kwa taarifa yenu Wapemba wanaongoza popote pale duniani kwa
kuchukuliana wanawake na kujisifu"Aka wajua eh nshanchukua nke wa fulani"

BY THE WAY nchimbi mwenyewe ndo huyu hapa


anavimba MISHAVU tuuu
 

Mafuchila

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2006
Messages
752
Points
195

Mafuchila

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2006
752 195
Amina Chifupa kulipua bomu leo
na Mwandishi WetuMBUNGE wa Viti Maalumu, Amina Chifupa (CCM), amesema leo analipua bomu mbele ya waandishi wa habari kuhusu kuvunjika ndoa yake na Mohamed Mpakanjia, tukio analosema limesababishwa na kiongozi mmoja ndani ya Chama Cha Mapinduzi, ambaye pia ni Naibu Waziri.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Amina, alisema anamuomba Mwenyezi Mungu amuamshe salama, ili aweze kuzungumzia suala hilo ambalo anafahamu kuwa linaweza kumuweka katika wakati mgumu kabisa.

"Nafahamu ninapambana na watu hatari, lakini kesho (leo) namuomba Mwenyezi Mungu aniamshe salama, ili niweze kuliweka bayana suala hili mbele ya waandishi wa habari MAELEZO. Nimekusudia kusema ukweli wote kuhusu suala langu," alisema Amina.

"Daima nasimamia ukweli na sababu ya dhamira yangu. Nipo tayari kufungwa au kuchukuliwa hatua yoyote iwapo nitaonekana sina nidhamu… hata ikibidi kupoteza ubunge na uanachama wangu wa CCM. Mimi si mwanasiasa wa ‘ndiyo mzee'," alisema Amina baada ya kuulizwa iwapo ukweli anaotaka kusema hautamgharimu.

Amina ambaye ameihakikishia Tanzania Daima kuwa alipewa talaka na mumewe, Mei 3 mwaka huu, anasema tukio hilo lilikuja baada ya kiongozi huyo wa CCM ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho kumuita mumewe ofisini kwake.

"Nilipewa talaka siku ile ile baada ya Mpakanjia kutoka ofisini kwa kiongozi huyo. Kwa kweli (anamtaja) ndiye aliyevunja ndoa yangu kwa kumuambia mume wangu mambo ya uongo," alisema.

Habari zaidi ambazo gazeti hili limezipata zinaeleza kwamba, Amina anaamini kwamba kikubwa kilichosababisha akutwe na masahibu hayo, ni kile kinachoelezwa kuwa uamuzi wake wa kutaka kugombea uenyekiti wa taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), hatua ambayo inaonekana kuwashtua na kuwakera baadhi ya viongozi wa sasa wa umoja huo.

Hivi sasa Mwenyekiti wa UVCCM ni Emmanuel Nchimbi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana anayetarajiwa kumaliza kipindi chake mwakani.

Hata hivyo, Amina alipotakiwa kueleza iwapo alikuwa akikusudia kugombea nafasi hiyo, hakuwa tayari kusema lolote zaidi ya kumtaka mwandishi kusubiri hadi wakati utakapofika kwani kuna muda mrefu bado, kabla ya yeye kufikia uamuzi huo.

Mbali ya hilo, Amina alielezwa kushangazwa kwake kuona masuala yake ya ndoa, yakipelekwa bungeni, wakati mahusiano yake ya nyumbani hayana uhusiano wowote na ubunge wake au uanasiasa wake.

Habari ambazo zilithibitishwa zinaonyesha kuwa, Amina amekuwa akihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mbunge kijana wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ambaye alipopigiwa simu na gazeti hili jana, aliyapuuza madai hayo ambayo alisema; "hayana ukweli."


Zitto mmoja wa wabunge machachari wa upinzani, alisema anafahamu kwamba suala hilo limeandaliwa na kundi la watu wenye sababu za kisiasa, ambao wamekuwa wakimtafuta yeye na Chifupa kwa muda mrefu.

"Ukaribu wangu na Amina ni wa kikazi tu… na ukaribu huo ulianza siku Spika wa Bunge alipotuteua tuhesabu kura za wabunge zilizomuidhinisha Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

"Siku hiyo tulipokuwa tukihesabu kura, afisa mmoja wa bunge alitufuata katika chumba cha kuhesabu kura na akatutaka kutozitaja kura mbili zilizokuwa zimeharibika, jambo ambalo mimi na Amina tulilikataa. Tangu hapo nilianza kumheshimu Chifupa baada ya kubaini kuwa alikuwa mtu makini na mwenye msimamo. Tangu wakati huo tumekuwa na uhusiano wa karibu kikazi," alisema Zitto, alipohojiwa kwa njia ya simu.

Alisema, siku zote amekuwa na uhusiano mzuri na wabunge wote vijana kwa wazee, lakini anashangazwa na uvumi juu ya uhusiano wake na Amina kuonekana vinginevyo.

Gazeti moja la kila siku, (si Tanzania Daima), jana lilimkariri Mpakanjia, akithibitisha kumtaliki mkewe baada ya kubaini ndoa yake ikiingiliwa na mbunge wa CHADEMA ambaye hata hivyo hakumtaja.

Habari zaidi ambazo gazeti hili linazo zinaeleza kwamba, ushahidi mkubwa unaoonekana kuwaunganisha kimapenzi wabunge hao vijana, ni tukio la siku moja jioni, ambalo Amina alionekana akiwa amevaa koti la Zitto, wakiwa wameketi pamoja katika Hoteli ya Dodoma.

Source: Tanzania Daima 07-05-2007
 
Joined
Mar 6, 2007
Messages
38
Points
0
Joined Mar 6, 2007
38 0
Hizi mimi naona ni tuhuma sababu habari niliyoisoma hapa sijaoneka uthibitisho wa tuhuma hizo.

unajua kwa kumbu kumbu zangu wakati Amina anaolewa na huyu jamaa, amina kwanza alikuwa mdogo, pili uwezo wa kifedha wa bwana inaweza kuwa ndio chanzo cha ndoa yao. Hivyo kama tuhuma hizi ni za kweli kwa mtu anayetafakari hawezi kushangaa.

bali inawezekana baada ya kukomaa kiakili na kuimarika kiuchumi huyu binti sasa amenza kufanya maamuzi ya kimapenzi na sio msukumo wa fedha au udogo.

Ndoa ya hawa jamaa ni mkataba baina ya huyu binti na huyu mume wake, sasa kama huyu binti kakiuka mkataba, huyu bwana anapashwa kumshitaki mke wake kwa spika na sio huyu aliyemsaidia kazi yake. Maana huwezi kumshitaki mtu ambaye hayuko katika mkataba kuwa kavunja mkataba.

MAPENZI SI JAZIBA WALA HAYANUNULIWI KAMA NDOA IMEGOMA MNAACHANA KWA VIZURI KILA MMOJA ANAENDA KUJARIBU KILE ATACHOONA KINAFAA.
 

Halisi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2007
Messages
2,812
Points
1,250

Halisi

JF-Expert Member
Joined Jan 16, 2007
2,812 1,250
Baba yake Amina, Mzee Chifupa, leo ameibuka pale Idara ya Habari Maelezo na kusema kwamba Familia imeamua akumzuia Amina kufika maelezo kutoa kile alichokiita kuwa ni Bomu. Mzee Chifupa, akasema kwa kuwa yy ni mwanajeshi mstaafu, bomu ni hatari na kisiasa asingependa mwanae, ambaye "ndio pensheni yake" ajihusishe na mabomu. Akakanusha kuwa Amina kapewa talaka tatu, amesema amepewa talaka moja, ambayo anapaswa kuendelea kupata huduma za mumewe. LAkini alipoulizwa alipo alisema familia haijui aliko, na kwamba aliwasiliana naye kwa njia ya mtandao.

Alisema kama kuna masuala ya kichama yatashughulikiwa na chama na kama kuna masuala ya kifamilia yatashughulikiwa na familia. Kwa ujumla UKUMBI WA MAELEZO ULIFURIKA, waandishi wengi, wa michezo, burudani na habari za siasa, ambao waliondoka bila kupata kilichowapeleka, walitaka kusikia kutoka mdomoni kwa Amina kuhusu NAibu Waziri (Nchimbi) aliyeingilia ndoa yao.

MAONI YANGU NI KWAMBA, hili suala linaashiria MCHEZO MCHAFU KUANZA UPYA, inanikumbusha enzi za JANE MIHANJI..... INATISHA ZAIDI KUSIKIA TAARIFA ZA MWANAKIJIJI kuhusu afya ya AMina. Haina tofauti na ya JANE alipopambana na NCHIMBI. MAMBO yale yalihusishwa pia na mapenzi/Siasa kwa wakati mmoja na mchezaji alikua Nchimbi. Kazi kwenu. Nadhani kwa sasa Zitto asizungumze, ili asije kuwapa faida katika kampeni zao za UVCCM
 

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,752
Points
2,000

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,752 2,000
Mpakanjia kachemsha,toka lini taarifa ya kuvunja ndoa ikapelekwa Bungeni?Nakumbuka siku za nyuma habari zilikuwepo za chinichini juu ya tabia isiyo muafaka ya mkewe katika vyombo vya habari nafikiri katika kugawa `fadhila`kwa kupendelewa kupata uwakilishi wa vijana. Hakushtuka, zaidi ya yote akafanya naye TOUR eti anampa kampani. Tatizo hapa nikuwa `fadhila`hizo walizitaka wazee ndani ya CCM pekee,sasa hata Kabwe naye Kala?! loh ndio balaa linaanzia hapo.Mpakanjia alitakiwa ajiulize mara mbili,jee mama alikuwa na sifa kweli za kuukwaa uheshimiwa katika kipindi kile?au alibebwa?na kama alibebwa ni kwanini? Ndio faida ya kujikomba kwake CCM. Mpakanjia alishajiona mdau wa CCM,subutu! CCM ina wenyewe yeye akubali matokeo tuu na hizo Tenda za biashara anazozipata kila siku.
 

alles

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2006
Messages
356
Points
0

alles

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2006
356 0
Kulikuwa na umuhimu ngani wa Mr Mpakanjia kutoa taharifa kwa spika wa Bunge. Ndoa si ni mambo ya familia?Je tuliowa/kuolewa na wabunge ndoa zetu zikivunika inatakiwa tulipoti bungeni?

Wanazuoni wa sheria na mambo ya bunge naomba mnijibu.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,874
Points
2,000

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,874 2,000
Halisi, believe me.... binti yuko katika hali mbaya.. leo ameamka akiwa anabwabwajabwabwaja na jambo la maana ni watu kupiga kelele ili aruhusiwe kuja hadharani... hofu yangu ni kuwa kuna watu "wanamshikilia" Bi. Amina against her will ambavyo ni sawa na kumteka nyara!!!!
 

FairPlayer

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2006
Messages
4,166
Points
1,225

FairPlayer

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2006
4,166 1,225
Halisi,

Nimegee kuhusu Jane Mihanji. Maana alinipita pembeni. Plizzzzzzz

AC hana kipya anatafuta umaarufu wa kisiasa, kwa uwenyekiti wa UV taifa, ninasema NOOOOOOOO!!! Nchimbi tumia mbinu zooote huyu bibie asisogee, hana sifa kabisaaaa.
FD
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,390,544
Members 528,186
Posts 34,054,182
Top