Nyinyi mnafikiri mnampenda Lakini hamuelewi ukweli ya yale yanayomsibu au ya yale ambayo yangemsibu Mzazi wake ndiye anyejua yale ambayo yangemkuta kwa yale anayoyafahamu yeye kutokana na habari alizozipata.Mzee Ametumia busara na Nyinyi mnashabikia na FREE AMINA Kwasababu hakuna anayejua kwa undani yanayomsibu huyo Mh.Amina kwasasa na Ambayo yangemsibu baada ya kuwaweka sawa wapinzani wake kwamba anataka kulipua bomu.
Hulka ya wanadamu waliowengi ni Ubinafsi, Mnachoshabikia nyinyi ni kutaka kusikia kile Mh.Amina alichotaka kukitoa hadharani na ndiyo kelele zote za FREE AMINA,Lakini wale wenye Mapenzi ya kweli na wenye uchungu na wanaomthamini Na watakaoathirika zaidi na matokeo ya maamuzi ya Mh Amina na Wanaolijua litakalomfika Mh.Amina endapo ataendelea kupayuka kwasasa ndiyo wanaoguswa zaidi na hiyo hatua waliyoichukua ndiyo wao wanaona ni muafaka kwasasa.Nani Kama Mzazi au Wazazi.?
Tusiyafanye ya wenzetu kuwa rahisi,tuangalie na athari za yale yanayowakuta au yatakayowakuta wenzetu kutokana na matendo wanayokusudia kuyafanya au waliyoyafanya au watakayofanyiwa au waliyofanyiwa.Fikra kila mmoja na zake Lakini wachache wenye kujaliwa BUSARA.
Mwanakijiji!hili la sasa naogopa hata kusema (na mimi si mwoga hivyo...)... Mwe Majira haya ni ya kiangazi huku kijijini, na joto limezidi..!!
Ngoja kwanza, hivi kwani Amina ametekwa au namna gani? Mimi nilifikiri amejificha tu kwa kuogopa mkwara wa CCM au? Mnataka kuniambia issue yake ni kama ya Alan Johnson huko Gaza? Kama ni hivyo basi wana harakati kama Mnyika waandae maandamano makubwa Dar ya kumkomboa huyu binti mikononi mwa watekaji na hizo T-shirt zisambazwe kikwelikweli sio kwenye internet!
Tanzanianjema said:Ndugu wana JF
"ninachomuomba na kumshauri Bw. Kabwe, yeye afuate nyayo za Amina Chifupa ili aweze kujinadi na kueleweka katika anga za siasa" Mtoaukweli? Ar u serious?
Mimi nimmoja wa vijana wachache wanaoamini mchango wa dada yetu Amina lakini sidhani kama ni vizuri kumshauri Zitto kufuata staili ya Amina. Calibre ya Zitto ni nyingine na Amina ni nyingine. Wote wanawakilisha aina mbalimbali za Utanzania na ndio maana ya kuwa na Bunge
"Ushauri wa bure kwanza aache kutoroka bungeni!" Ndugu zangu kwani Zitto ni mtoro. Acheni kumuonea.
...........................
Padri asababisha kifo akimtoa mimba binti
na Ramadhani Siwayombe, Manyara
PADRI mmoja wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbulu (jina linahifadhiwa), anatuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari ya Dongobesh wilayani Mbulu.
Kama hiyo haitoshi, inadaiwa kuwa baada ya kubaini kuwa binti huyo ni mjamzito, padri huyo alimtorosha na kwenda naye mjini Babati kwa lengo la kuitoa mimba hiyo lakini kwa bahati mbaya binti huyo alifariki dunia wakati wa zoezi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi, shangazi wa binti huyo, ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini kwa kuhofia usalama wake, alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Veneranda Anthony Yessaya, ambaye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na padri huyo kwa muda mrefu.
Shangazi huyo alisema kuwa padri huyo alifanikiwa kumrubuni binti huyo kwa njia ya kujifanya mfadhili wake, ambaye atamgharimia masomo.
Alisema padri huyo alijitokeza wakati marehemu Veneranda akijiunga na kidato cha kwanza mwaka 2006 katika Shule ya Sekondari ya Gidhim, iliyopo wilayani Mbulu.
Alibainisha kuwa, padri huyo aliamua kumhamisha na kumpeleka Shule ya Sekondari ya Endaraftal, iliyopo wilayani Karatu.
Alisema baada ya muda, walishangaa padri huyo akimhamisha tena binti huyo na kumpeleka Dongobesh Sekondari, ambako aliendelea kuwa na mahusiano naye kimapenzi.
Akisimulia zaidi, shangazi huyo alisema walianza kuhisi uhusiano usiofaa baina ya binti yao na mfadhili wake Aprili 20, mwaka huu, baada ya padri huyo, ambaye alihamishiwa Kiru akitokea Dongobesh, kufika kijijini Dongobesh na kuonekana akiwa na binti huyo.
Na baada ya kuulizwa, padri huyo alidai amefika hapo kumchukua ili akamnunulie vitu muhimu vya shuleni.
Aprili 26, binti huyo aliomba ruhusa kwa uongozi wa shule, kwa madai kuwa alikuwa anakwenda nyumbani kwa wazazi wake, ambapo baba yake ni mwalimu katika Shule ya Msingi ya Dumanangw na alipofika nyumbani alipewa fedha na wazazi wake na kuaga kuwa anarejea shuleni.
Shangazi yake huyo alisema hata hivyo, binti huyo hakufika shuleni tena na badala yake alikwenda Babati, ambako inadaiwa alikutana na padri huyo na walikwenda katika moja ya nyumba ya kulala wageni mjini hapo.
Ilielezwa kwamba baada ya siku kama mbili, padri huyo alimfikisha binti huyo katika hospitali moja (jina tunalo), iliyopo mjini Babati, akiwa mahututi. Baadaye, padri alimpigia simu mama mzazi wa binti huyo, ambaye kwa wakati huo alikuwa mjini Arusha.
Baada ya kuona hali ya binti huyo ni mbaya, kabla hata ya wazazi wa binti huyo kufika, padri huyo alitoroka na kumwacha binti huyo katika hospitali hiyo na baadaye alifika mama yake na baba yake ambao walilazimika kumchukua na kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi, alisimulia shangazi huyo.
Uchunguzi uliofanywa na daktari katika Hospitali ya KCMC ulibaini kuwa binti huyo alikuwa ametolewa mimba lakini kitendo hicho hakikufanywa ipasavyo kwani kulikuwa na uchafu uliokuwa umebaki tumboni na kufanya sehemu za mwili wake zianze kuoza.
Akisimulia mkasa huo kijijini kwake Dongobesh juzi, baba mzazi wa marehemu, Mwalimu Anthony, alisema: Uchunguzi wa madaktari wa Hospitali ya KCMC umegundua kuwa utumbo pamoja mfuko wa uzazi navyo vilianza kuoza.
Mwalimu Anthony alisema kutokana na hali hiyo, familia yake imeamua kufungua kesi Polisi dhidi ya padri huyo. Hata hivyo, alidai kuwa uongozi wa kanisa jimboni Mbulu unamkingia kifua padri huyo ambaye amejificha.
Mmoja wa madaktari walioufanyia uchunguzi mwili wa binti huyo, ambaye alikataa kutajwa kwa vile si msemaji wa hospitali hiyo, alisema binti huyo aliyekuwa na ujauzito wa miezi mitano, alikuwa ametolewa mimba kwa vifaa vichafu.
hili la sasa naogopa hata kusema (na mimi si mwoga hivyo...)... Mwe Majira haya ni ya kiangazi huku kijijini, na joto limezidi..!!
Hivi kaka mchongoma umetukimbia tena? Looo acha uchoyo huo ama kazi ya kulinda urithi wa babu inazidi kuwa ngumu. Usiwe na shaka kaka kwa pamoja tutatoka tuu katika kipindi hiki kigumu.Hodi wanabodi! Heshima yenu wakuu! kwa kipindi kirefu mimi nimekuwa msomaji tu makala mbali mbali humu, bila kuchangia chochote, hivyo naheshimu sana mawazo na michango yenu yote, ila katika hili imenibidi nitoe maoni yangu.
Ama kwa hakika suala la ndoa si suala la kuliingilia, kwa maana kwamba, kwangu mimi sitaona ajabu baada ya muda mfupi ujao Bwana MM akaamua kumrudia mkewe Bi AC! Jambo ninalopenda kuwatahadharisha wanabodi n kwamba itakuwa ni aibu kubwa kwa wazee wenye busara kama nyie mkianza 'kusutwa' hadharani mkinukuliwa posts mlizoweka humu.
Jaribuni kulitafakari hili, nadhani Mzee mwkjj, Mkandara na wengineo wachache wamekuwa wajanja katika kutizama pande zote za shilingi bila kuwahukumu hao watuhumiwa moja kwa moja. Hii thread iendelee kujadiliwa ila, muwe makini kuwa huu ni udaku!, na itapofikia wakati wazee wetu mkianza kusutwa, hata maoni yenu mengi tu ya busara yataonekana kama ya udaku udaku tu. Heshima yenu wazee, naomba kutoa hoja!
Shukran.
Kuna mtu anaweza kufafanua? Ni kama ninakosa conection mahala fulani hapa.Anachofanya huyu jamaa ni kujaribu kuanzisha mjadala ndani ya umoja wa vijana wa CCM kuhusu uaminifu wa AC kwa "SIRI" za CCM kwa kujifanya kumlenga Kabwe. Hayo ndiyo aliyokuwa akiyatumia mwanzoni na wenzake ambao mpaka sasa bado hakuna ulazima wa kuanikwa. Baada ya kuona mwanadada anaendelea kuvuma ingawa tayari alishamwaga hiyo sumu ndipo akaamua kutumia hiyo Nyuklia yake ambayo tayari imeshaanza kumrudi.