Kashfa nzito ndani ya Benki ya NMB

Kashfa nzito ndani ya Benki ya NMB

- Mimi ni mkazi wa Tabata na mwajiriwa wa Benki ya NMB. Kwa maslahi mapana ya taifa na ya Benki hii, nadiriki kuyaweka maisha yangu na ajira yangu hatarini kwani nikijulikana either ntatoweka au ntafukuzwa kazi. Niko tayari kwa yote mawili, Ila siwezi kunyamaza kwenya kashfa la ajabu, aibu na la kijinga linalotia kinyaa kama hili linalotendeka ndani ya hii benki. Kwa lugha nyingine huu ni uozo, ambao nadhani serikali au Takukuru walichunguze. Hii benki haitaki kitu chochote kizuri kisichokuwa na maslahi binafsi kwa wakubwa. Nimeamua kuwa mpiga mbiu au kafara ikibidi.

- Kuna kampuni ya wajerumani walioleta teknolojia (suluhisho la uhakika) ambayo imeonekana kuwa ni ya hali ya juu kwenye maswala ya nishati. Wakazi wa Tabata tumeliona hili pale Kimanga kwa miaka miwili sasa. Ila hii teknolojia imepigwa vita kali sana ndani ya benki, na hatimaye hao wajerumani wakafukuzwa. Nimeambiwa walifukwa vibaya sana, wakiambiwa hawana vigezo kwa sababu walikubaliwa kufunga mitambo yao na afisa wa ngazi ya chini, huku hawa hawa viongozi wakiendelea kuchukua vitu vya hovyo kariakoo kuja kufunga kwenye hii saiti. Zaidi waliambiwa hawawezi kufanya lolote, wakitaka waende mahakamani

- Siku ya ijumaa 18/11/2016 niliondoka kazini mapema kidogo, mida ya saa 7 baada ya dada wa kazi kunitaarifu kwamba , mwanangu wa pili alirudishwa kutoka shule mapema baada ya kuonyesha dalili za kuwa na malaria. Pale Tabata Kimanga nina kabiashara kadogo, kwa hiyo nikaamua kupapitia kuangalia maendelo kabla ya kwenda nyumbani. Biashara yangu haipo mbali na jengo la ATM la NMB. Baada ya kuwasili, niliona umati mkubwa mbele ya jengo hilo, kidogo nilishtuka na kutaka kujua kulikoni. Wengi wa waliokusanyika pale, walionyesha kukerwa sana kwa sababu wajerumani walikuwa wanang’oa mitambo yao za kufua umeme walizofunga kwenye hizi ATM tatu za hapa Kimanga.

- Kwa wakazi wa Segerea, Kigogo, Buguruni, Ubungo, Tabata na viunga vyake vyote, wanalijua hili ATM kwa sababu ni sehemu pekee hapa DAR pakukimbilia umeme unapokatika kwa kipindi kirefu na huduma za ATM zikawa hazipatikani. Nina maana kwamba umeme unapatikana hapa masaa 24 na hakuna foleni. Waendesha bodaboda, wafanyabiashara wadodgo wadogo, na walinzi katika eneo hili walilitegemea sana hii mitambo ya wajerumani iliyokuwa inafua umeme na kutoa mwanga mkubwa pale umeme unapokatika hasa usiku. Kwa kifupi, hii sehemu haikuwa tu ni ya uhakika, ila pia ilikuwa ni kivutio kikubwa sana hapa Kimanga, ilitengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu, kila aliyepita alisimama na kupashangaa. Jana nioni mida ya saa mbili nilipita pale, ni giza !

- Kutaka kujua zaidi kinachoendelea, nilimpigia simu mshikaji wangu wa kitengo cha IT. Mshikaji aliogopa kuongea nami kwenye simu, na kuniomba tukutane jioni ili tupate Kinywaji, ingawa naye alionyesha dhahiri kukerwa na huu uamuzi. Basi jioni yake tukakutana maeneo ya Bima, Cha kwanza kabisa, mshikaji alichoniambia, aisee, hii issue ni nzito, hawa wajerumani ni tishio, teknolojia yao imegusa maslahi ya wakubwa, jamaa wamechachamaa kule ndani. Walikuwa wanakula sana kwenye hizi ATM. Inveter na betri zimekuwa zinafungwa na makampuni yao. Hawataki kabisa kusikia juu ya hawa wajerumani. Kwa miaka miwili sasa, ATM ya kimanga ndio sehemu pekee ndani ya Benki ambako umeme ulikuwa haukatiki na wala simu za mitambo kusumbua zilikwisha kabisa. Idara inayoshugulikia maswala ya umeme na ATM maintenance zilifurahi sana na kudhania viongozi wangelipokea hii teknolojia kwa furaha zaidi na kuisambaza nchi nzima, lakini ikawa kinyume chake. Cha kushangaza zaidi, ni kwamba, hao wajerumani walifunga hiyo mitambo iliyotumika kwa miaka miwili bila kulipwa hata senti tano, na walipoanza kudai malipo ndio mambo yakaharibika

- Habari zilizovuja za ndani kwa ndani ambayo ndiyo sababu yangu kubwa ya kuvuja hii habari, ni kwamba, Mkurugenzi wa kitengo cha Ugavi, alitamba mbele ya wajerumani akiwaambia kwamba, aliyewapa ruhusa kufunga hii mitambo, ni mtu mdogo sana ndani ya benki. Kwa maana hiyo hawana vigezo kufanya biashara na NMB na hawatalipwa, kwa hiyo wao wakaondoe madude yao, na wawe tayari kusikia habari za huyo ofisa aliyewapa hidhini kufukuzwa ndani ya benki siku chache zijazo. Wakitaka wampe kazi. Habari zaidi zinadai kwamba, siku hiyo hiyo wajerumani walipong’oa mitambo yao pale kimanga, kampuni ndogo isiyoeleweka kutoka Kariakoo ilipewa hiyo kazi. Na kichekesho cha mwaka, pale wajerumani walipoanza tu kung’oa mitambo yao, ATM mbili ziligoma kufanya kazi na foleni ikaanza kwenye ATM moja iliyosalia. Huu ni uozo na uwenda wazimu, tangu lini vifaa vya kichina kutoka kariakoo vikawa na ubora zaidi ya vifaa vya Kijerumani?

- Sasa Napata picha ni kwanini Rais Magufuli anatumbua watu bila huruma. Ni kutokana na tabia za ajabu na ubinafsi uliopitiliza kama hizi hapa. Wewe kitu ambacho kimeonekana kuwa ndio suluhisho dhidi ya kero na matatizo siyo tu kwa benki, bali kwa wateja na wananchi, inapigwa vita kiasi hiki na hata vendor kufukuzwa? Kama siyo maslahi binafsi ni nini? Viongozi wangu ndani ya Benki, tendeni haki. Chunguzeni hii kitu kwa undani kabla ya huyu jamaa hajafukuzwa. Huyu ofisa asitolewe kafara. Bodi ya wakurugenzi wa NMB, ikibidi ingilieni kati. Vinginevyo serikali iingilie kati. Takukuru wawachunguze hawa viongozi wanaoweka maslahi binafsi kwenye taasisi za umma na kuzuia vitu vya maana vinavyoweza kutatua kero za wananchi huku wakiangalia matumbo yao binafsi. Huyu ofisa kwangu mimi ni shujaa kwa sababu alileta suluhisho. Kwanini ageuzwe kuwa kafara?

Magu sio wa mchezo mchezo hili atakuwa kesha lichukua subiri watu kutumbuliwa
 
Uwe una acha ujinga. Elimu yako itumie ipasavyo!!
Bwege wewe, kila kitu unawaza ni elimu tu acheni umbea na majungu mmeajiriwa kufanya kazi kama unaona kampuni inakuboa acha kazi..sio kila kitu mnaanika kwenye mitandao! Pathetic
 
Chapa kazi mheshimiwa Rais wetu Magufuli,wanaanza kukuelewa taratibu.Mungu Ibariki Tanzania yetu.
 
NMB ina matawi kila kona hapa nchini, sasa unaitaje kashfa nzito kwa ishu ya kaeneo kamoja ambapo sioni kama inaathiri sera za benki kwa namna yoyote. Au na wewe ulikuwa unakula kwa wajerumani? Kwa udogo WA suala hili sioni kama ni kashfa nzito
Sijui ulimfuatilia vizuri hoja yake? Jamaa kasema badala ya kuikataa hii teknolojia ya mjerumani ilibidi isambazwe nchi nzima. Pia titizo dogo ndio huzaa tatizo kubwa lililo sugu linaloweza kuathiri sera za bank husika. Mdharau mwiba...
Pia hii ni sehemu tu ya uozo uliokithiri kitengo cha ugavi.
 
Jamaa unashangaa hilo tu mwaka 1983 kulikua na tafiti za kuzalisha umeme toka kwenye maporomoko ya maji huko morogoro kama hicho chanzo kingetumiwa umeme wa mgao Tanzania ungekua ni historia na umeme ungezalishwa mwingi kiasi cha kuweza kuuza nje, ila watu waliona wakielekeza mradi huo uko pesa za umeme wa dharura zisingeweza kupatikana kwaio wakapotezea huku hicho kina kikipungua maji kila mwaka hii nilisoma tu kwenye G.S A -level maana ticha wangu alidokezea tu ila nilishangaa sana...
 
Sijui ulimfuatilia vizuri hoja yake? Jamaa kasema badala ya kuikataa hii teknolojia ya mjerumani ilibidi isambazwe nchi nzima. Pia taitizo dogo ndio huzaa tatizo kubwa lililo sugu linaloweza kuathiri sera za bank husika. Mdharau mwiba...
Pia hii ni sehemu tu ya uozo uliokithiri kitengo cha ugavi.
Nadhani, kama ni kweli, hii issue itakuwa case study nzuri sana. Ila siamini kama kweli hii kitu ilifanya kazi. Viongozi wa NMB wasingekataa technolojia yenye manufaa kwa benki yao
 
Bwege wewe, kila kitu unawaza ni elimu tu acheni umbea na majungu mmeajiriwa kufanya kazi kama unaona kampuni inakuboa acha kazi..sio kila kitu mnaanika kwenye mitandao! Pathetic
Hivi una accoint yeyote hata katika simu?
huna elimu na kilichobaki ni kuzifutika kwenye makalio na kuzinywea
Watu wanaokoa Benki zao zitoe huduma safi mijitu mingine ipo kiwiziwizi tu hapa
 
Hivi una accoint yeyote hata katika simu?
huna elimu na kilichobaki ni kuzifutika kwenye makalio na kuzinywea
Watu wanaokoa Benki zao zitoe huduma safi mijitu mingine ipo kiwiziwizi tu hapa
Hakuna cha kutetea wala nn hayo ni majungu tu, wabongo ni wanafiki sana
 
na Ngosha akitumbua watu wanakuja na makelele eti aache panga panua huku wakopaji wakitozwa riba inayoishia kwenye makampuni ya ubabaishaji.
 
Jamaa unashangaa hilo tu mwaka 1983 kulikua na tafiti za kuzalisha umeme toka kwenye maporomoko ya maji huko morogoro kama hicho chanzo kingetumiwa umeme wa mgao Tanzania ungekua ni historia na umeme ungezalishwa mwingi kiasi cha kuweza kuuza nje, ila watu waliona wakielekeza mradi huo uko pesa za umeme wa dharura zisingeweza kupatikana kwaio wakapotezea huku hicho kina kikipungua maji kila mwaka hii nilisoma tu kwenye G.S A -level maana ticha wangu alidokezea tu ila nilishangaa sana...
Kitaje hiko chanzo ili iwe "baseline" kwenye mjadala utakaoanzishwa kuhusu hiko chanzo.
 
Nadhani, kama ni kweli, hii issue itakuwa case study nzuri sana. Ila siamini kama kweli hii kitu ilifanya kazi. Viongozi wa NMB wasingekataa technolojia yenye manufaa kwa benki yao

Mkuu kwenye mashirika ya UMMA hilo awajali - wanajali maslahi tu, kwao masuala ya teknolojia ya uhakika hiyo kwao ni secondary.

Binafsi ninacho kiona mimi si ajabu kuna kajikampuni mshenzi kamejitokeza kuwauzia NMB vifaa vya nishati mbadala, kampuni hiyo inaweza kuwa inamilikiwa na ndugu au jamaa wa mmoja wa maafisa wakubwa wa Benki ya NMB, wakala njama za kusitisha huduma za kampuni ya Kijerumani unceremonously, awajali kitakacho tokea, mashirika ya UMMA mengi yako hivyo Wakurugenzi wanajifanya Miungu watu na wala awamwogopi JPJM - wamekwisha jijengea mizizi utawafanya nini?

Binafsi ningeshauri PCCB ifatilie suaka hili haraka sana ili wajue undani wa sakata hili: Ni nani wahusika wakuu na hicho kijikampuni cha Kariakoo kifatiliwe kiseme nani alikipa tenda ya kufunga vifaa vyenyewe walakini, na kwa nini Kampuni ya Kijerunani ilisitisha huduma zake.

Bodi ya NMB nayo inapaswa kuwajibishwa kwa kushindwa kusimamia utendaji wa Viongozi wakuu wa NMB
, kama BODI ingekuwa na meno Viongozi wakuu wa NMB wasingekuwa na ubavu wa kufanya upuuzi huu.
 
Kwa njia yoyote ile tutafika tuu na lazima tunyooke....Ata mungu ilibidi Aue Kizazi cha Israel Jagwani..................................Na hivi ndivyo ilivyo katika hii Tanzania ya leo ambapo ilifika kila mmoja kama ana sehemu yake ya nchi kwa kutaka pesa za uraisi
 
Back
Top Bottom