Kashfa nzito ndani ya Benki ya NMB

Kashfa nzito ndani ya Benki ya NMB

- Mimi ni mkazi wa Tabata na mwajiriwa wa Benki ya NMB.
- Sasa Napata picha ni kwanini Rais Magufuli anatumbua watu bila huruma. Ni kutokana na tabia za ajabu na ubinafsi uliopitiliza kama hizi hapa. Wewe kitu ambacho kimeonekana kuwa ndio suluhisho dhidi ya kero na matatizo siyo tu kwa benki, bali kwa wateja na wananchi, inapigwa vita kiasi hiki na hata vendor kufukuzwa? Kama siyo maslahi binafsi ni nini? Viongozi wangu ndani ya Benki, tendeni haki. Chunguzeni hii kitu kwa undani kabla ya huyu jamaa hajafukuzwa. Huyu ofisa asitolewe kafara. Bodi ya wakurugenzi wa NMB, ikibidi ingilieni kati. Vinginevyo serikali iingilie kati. Takukuru wawachunguze hawa viongozi wanaoweka maslahi binafsi kwenye taasisi za umma na kuzuia vitu vya maana vinavyoweza kutatua kero za wananchi huku wakiangalia matumbo yao binafsi. Huyu ofisa kwangu mimi ni shujaa kwa sababu alileta suluhisho. Kwanini ageuzwe kuwa kafara?
Wengi hawajui hilo wanapenda mwendelee a shida na majanga huku wakineemeka na mambo mema kama hayo unayoshuhudia hapa hawataki kusikia. Watu wanataka kupiga na si maendeleo ya kudumu...Kwa kuwa baadhi ya wakuu huwa wanapita humu kilio chako kitasikilizwa ila wabongo kwa kupigaaa na wizi, unafiki, uchoyo, rushwa na uongo...tunapenda sana ..na vitu hivyo ndio sababu ya Taifa kurudi nyuma..Hapo wako wanao jitahidi kwa hali na mali wamkwamishe Mh Rais lakini Mungu aliyempa hicho KITI atamsimamia kutimiza maombi ya walio wegi kuwa Taifa linaitaji kiongozi wa kufyeka uozo na mazoea machafu yenye kufifisha ustawi wa Taifa na watu wake
 
Ipo shaka juu ya uhusika wako katika hili..mfaidika toka kwa Wajerumani..Muathirika wa michakato ya kimaslahi ktk zabuni husika...

Nilitamani kuona tuhuma zenye kuathiri taifa kama taarifa za ufisadi unaofanywa kupitia Fraud kubwa zinazoratibiwa na wakuu wa Vitengo....

Rushwa katika mikopo ,Cash withdrawal kuanzia bilioni moja kwenda juu kinyume cha sheria za nchi na mengineo..
 
Nilitaka kufungua akaunti hapo baada ya kuambiwa changamoto za kutopata pesa kwenye ATM zimetatuliwa.
 
duh Nmb mnashida kumbe huwa mnaona Raha kutupangisha foleni kuanzia asubuhi mpaka jioni hamfai kabisa nyinyi
 
Kuna dili la wafanyakazi wa benki na makapuni yanayo service hizo ATM,wafanyakazi benkini wanaharibu vitu vidogovidogo,jamaa wanajifanya wana repair kwa cost kubwa na percent inaenda kwa aliyewasaidia kuharibu,hii dili iko muda mrefu tu na ndio chanzo cha ATM nyingi ku reportiwa ni mbovu ,anapokuja fundi kuna watu wana neemeka.Nadhani kila sehemu inahitaji kuwa na Magufuli wake maana uozo nchi hii ulikuwa umezidi.
 
NMB wana Huduma za hovyo sana wakati mengine nilikwenda mwezi wa 9/9 /2016 kuomba kadi nyingine kwani ya mwanzo ilianzafumuka kuharibika hivi toka muda huo mpk leo juzi na kwenda nakuta bado ilibidi nihamishe pesa zangu zote kwa CRDB na ninampango wa kubadili mshahara wangu kwa LAWSON upitie CRDB..
 
Hii ni nchi wadau.., sio kagroup ka watu wawili tu....!
Tecnologies zinauzwa, gharama zake wanajua wanaolipia....!! Tecnology ya mzungu gharama yake si ya kitoto...
Sijui tu, ile tungewekewa apa gharama zake tu geenda zetu kulala...!!! German..!! Chezea jeremen na tanganyika yake...!!
Jamaa walijenga tu miundombinu wasidai pesa ya installation mpaka walipoona huu ndo muda muafaka.. Kwamba hapa tukidai hawana jinsi watalipa tu....!!!
Sasa uyo mlipaji ndo anajua iyo pesa alodaiwa na uyu mkulu wa nchi tulonae na kasi yake ukimvalisha miwani kusoma iyo figure alafu ukaambiwa ii mzee ni ya kale kaeitiiem ka tabata na vitaataa vyake tu.....
Hakuna anependa kuacha ugali wake kwaajili ya mzungu ckuiz....!!!

Thats my take, otherwise nipite tu
 
- Mimi ni mkazi wa Tabata na mwajiriwa wa Benki ya NMB. Kwa maslahi mapana ya taifa na ya Benki hii, nadiriki kuyaweka maisha yangu na ajira yangu hatarini kwani nikijulikana either ntatoweka au ntafukuzwa kazi. Niko tayari kwa yote mawili, Ila siwezi kunyamaza kwenya kashfa la ajabu, aibu na la kijinga linalotia kinyaa kama hili linalotendeka ndani ya hii benki. Kwa lugha nyingine huu ni uozo, ambao nadhani serikali au Takukuru walichunguze. Hii benki haitaki kitu chochote kizuri kisichokuwa na maslahi binafsi kwa wakubwa. Nimeamua kuwa mpiga mbiu au kafara ikibidi.

- Kuna kampuni ya wajerumani walioleta teknolojia (suluhisho la uhakika) ambayo imeonekana kuwa ni ya hali ya juu kwenye maswala ya nishati. Wakazi wa Tabata tumeliona hili pale Kimanga kwa miaka miwili sasa. Ila hii teknolojia imepigwa vita kali sana ndani ya benki, na hatimaye hao wajerumani wakafukuzwa. Nimeambiwa walifukwa vibaya sana, wakiambiwa hawana vigezo kwa sababu walikubaliwa kufunga mitambo yao na afisa wa ngazi ya chini, huku hawa hawa viongozi wakiendelea kuchukua vitu vya hovyo kariakoo kuja kufunga kwenye hii saiti. Zaidi waliambiwa hawawezi kufanya lolote, wakitaka waende mahakamani

- Siku ya ijumaa 18/11/2016 niliondoka kazini mapema kidogo, mida ya saa 7 baada ya dada wa kazi kunitaarifu kwamba , mwanangu wa pili alirudishwa kutoka shule mapema baada ya kuonyesha dalili za kuwa na malaria. Pale Tabata Kimanga nina kabiashara kadogo, kwa hiyo nikaamua kupapitia kuangalia maendelo kabla ya kwenda nyumbani. Biashara yangu haipo mbali na jengo la ATM la NMB. Baada ya kuwasili, niliona umati mkubwa mbele ya jengo hilo, kidogo nilishtuka na kutaka kujua kulikoni. Wengi wa waliokusanyika pale, walionyesha kukerwa sana kwa sababu wajerumani walikuwa wanang’oa mitambo yao za kufua umeme walizofunga kwenye hizi ATM tatu za hapa Kimanga.

- Kwa wakazi wa Segerea, Kigogo, Buguruni, Ubungo, Tabata na viunga vyake vyote, wanalijua hili ATM kwa sababu ni sehemu pekee hapa DAR pakukimbilia umeme unapokatika kwa kipindi kirefu na huduma za ATM zikawa hazipatikani. Nina maana kwamba umeme unapatikana hapa masaa 24 na hakuna foleni. Waendesha bodaboda, wafanyabiashara wadodgo wadogo, na walinzi katika eneo hili walilitegemea sana hii mitambo ya wajerumani iliyokuwa inafua umeme na kutoa mwanga mkubwa pale umeme unapokatika hasa usiku. Kwa kifupi, hii sehemu haikuwa tu ni ya uhakika, ila pia ilikuwa ni kivutio kikubwa sana hapa Kimanga, ilitengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu, kila aliyepita alisimama na kupashangaa. Jana nioni mida ya saa mbili nilipita pale, ni giza !

- Kutaka kujua zaidi kinachoendelea, nilimpigia simu mshikaji wangu wa kitengo cha IT. Mshikaji aliogopa kuongea nami kwenye simu, na kuniomba tukutane jioni ili tupate Kinywaji, ingawa naye alionyesha dhahiri kukerwa na huu uamuzi. Basi jioni yake tukakutana maeneo ya Bima, Cha kwanza kabisa, mshikaji alichoniambia, aisee, hii issue ni nzito, hawa wajerumani ni tishio, teknolojia yao imegusa maslahi ya wakubwa, jamaa wamechachamaa kule ndani. Walikuwa wanakula sana kwenye hizi ATM. Inveter na betri zimekuwa zinafungwa na makampuni yao. Hawataki kabisa kusikia juu ya hawa wajerumani. Kwa miaka miwili sasa, ATM ya kimanga ndio sehemu pekee ndani ya Benki ambako umeme ulikuwa haukatiki na wala simu za mitambo kusumbua zilikwisha kabisa. Idara inayoshugulikia maswala ya umeme na ATM maintenance zilifurahi sana na kudhania viongozi wangelipokea hii teknolojia kwa furaha zaidi na kuisambaza nchi nzima, lakini ikawa kinyume chake. Cha kushangaza zaidi, ni kwamba, hao wajerumani walifunga hiyo mitambo iliyotumika kwa miaka miwili bila kulipwa hata senti tano, na walipoanza kudai malipo ndio mambo yakaharibika

- Habari zilizovuja za ndani kwa ndani ambayo ndiyo sababu yangu kubwa ya kuvuja hii habari, ni kwamba, Mkurugenzi wa kitengo cha Ugavi, alitamba mbele ya wajerumani akiwaambia kwamba, aliyewapa ruhusa kufunga hii mitambo, ni mtu mdogo sana ndani ya benki. Kwa maana hiyo hawana vigezo kufanya biashara na NMB na hawatalipwa, kwa hiyo wao wakaondoe madude yao, na wawe tayari kusikia habari za huyo ofisa aliyewapa hidhini kufukuzwa ndani ya benki siku chache zijazo. Wakitaka wampe kazi. Habari zaidi zinadai kwamba, siku hiyo hiyo wajerumani walipong’oa mitambo yao pale kimanga, kampuni ndogo isiyoeleweka kutoka Kariakoo ilipewa hiyo kazi. Na kichekesho cha mwaka, pale wajerumani walipoanza tu kung’oa mitambo yao, ATM mbili ziligoma kufanya kazi na foleni ikaanza kwenye ATM moja iliyosalia. Huu ni uozo na uwenda wazimu, tangu lini vifaa vya kichina kutoka kariakoo vikawa na ubora zaidi ya vifaa vya Kijerumani?

- Sasa Napata picha ni kwanini Rais Magufuli anatumbua watu bila huruma. Ni kutokana na tabia za ajabu na ubinafsi uliopitiliza kama hizi hapa. Wewe kitu ambacho kimeonekana kuwa ndio suluhisho dhidi ya kero na matatizo siyo tu kwa benki, bali kwa wateja na wananchi, inapigwa vita kiasi hiki na hata vendor kufukuzwa? Kama siyo maslahi binafsi ni nini? Viongozi wangu ndani ya Benki, tendeni haki. Chunguzeni hii kitu kwa undani kabla ya huyu jamaa hajafukuzwa. Huyu ofisa asitolewe kafara. Bodi ya wakurugenzi wa NMB, ikibidi ingilieni kati. Vinginevyo serikali iingilie kati. Takukuru wawachunguze hawa viongozi wanaoweka maslahi binafsi kwenye taasisi za umma na kuzuia vitu vya maana vinavyoweza kutatua kero za wananchi huku wakiangalia matumbo yao binafsi. Huyu ofisa kwangu mimi ni shujaa kwa sababu alileta suluhisho. Kwanini ageuzwe kuwa kafara?
hiyo ni benki binafsi unataka jpm aje kutumbua? wewe una maslahi binafsi au ni uzalendo kwa mwajiri wako. kama ni uzalendo kwa mwajiri wako usiogope kupeleka malalamiko au maoni yako kwa uongozi wa juu wa benki.
 
hiyo ni benki binafsi unataka jpm aje kutumbua? wewe una maslahi binafsi au ni uzalendo kwa mwajiri wako. kama ni uzalendo kwa mwajiri wako usiogope kupeleka malalamiko au maoni yako kwa uongozi wa juu wa benki.

Mkuu umeajiriwa au ulishawai kuajiriwa....au ww ni mpiga dili mtaani haujui misingi ya kuajiriwa.
 
Back
Top Bottom