Karibuni tupate kifungua kinywa...!!!

Huwa nakula sana hii makitu muda wa jioni...kwenye vituo vya daladala huwa kuna wale vijana wanavipika hivi na kuviuza.

Basi nikishatoka kwenye shughuli zangu za kubeba zege huwa nashusha viwili vitatu kabla ya kwenda kuegesha...


Ndivyo mlivyo wanaume wa siku hizi..
mimi49 anakupikia kila kitu ila ilimradi tu ununue na ule majiani...
 
Last edited by a moderator:

Swadaktaaa..
 
Hahaha anapika mkuu lakini ni nyumba chache sana ambazo chakula kama vitumbua hupikwa home...

Kweli aisee mikate na fast life imeharibu sana...mimi mpaka nishasahau kupika maandazi na mahanjumati yafananayo na hayo. Sijui kaka dada yako (mke wangu mtarajiwa) anajua hayo mambo. Ningependa times kama weekend hivi tunapika hizo makitu for breakfast!!!
 
Ndivyo mlivyo wanaume wa siku hizi..
mimi49 anakupikia kila kitu ila ilimradi tu ununue na ule majiani...

Loh asante kwa kunifumbua macho mshenga wangu, kumbe yahabibty mimi49 ajua hadi mapishi haya....
 
Last edited by a moderator:
Weee vile sio vitumbua zile tunaita mikate ya chila...

Miye nitajulia wapi hayo majina, huko Zenji huwa naenda kwa nadra...

Nakumbuka mara ya kwanza kuvila ilikuwa ni maeneo ya Mfereji wa Wima, pale pale njia panda nilikuwa nimetoka zangu kazini na kiza kimeanza kuingia...

ha ha ha huyu ni mbara nini farkhina loh... na Kibibi unakijua watu8

Miye mbara ndio huku kwetu hakuna hiyo mikate ya chila ila tuna mikate ya kumimina(mambo ya Tanga hayo) au ukienda usukumani kuna mabumunda
 

Huo mkate wa kumimina pia tunaita mkate wa mchele...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…