Karibuni tujadili Ibara za kubaki, kuondolewa au kufanyiwa marekebisho kwenye Katiba ya Tanzania

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,090
22,368
Wakuu nawasalimu kwa jina la jamhuri ya JMT.

Nataka tujadili katiba iliyopo kwamba vitu gani vibaki, viondolewe kabisa au kufanyiwa marekebisho. Mimi ninawaleteeni ibara tatu ambapo ya kwanza naona ibaki ilivyo, ya pili ifanyiwe marekebisho na ya tatu iondolewe kabisa. Ukizisoma ibara hizo kwa makini utajua sababu.

IBARA YA 25 IBAKI KAMA ILIVYO; iko very clear kuhusu kazi.

25.-(1) Kazi pekee ndiyo huzaa utajiri wa mali katika jamii, ndilo chimbuko la ustawi wa wananchi na kipimo cha utu. Na kila mtu anao wajibu wa-
(a) kushiriki kwa kujituma na kwa uaminifu katika kazi halali na ya uzalishaji mali; na
(b) kutimiza nidhamu ya kazi na kujitahidi kufikia malengo ya uzalishaji ya binafsi na yale ya pamoja yanayotakiwa au yaliyowekwa na sheria.

(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), hakutakuwapo na kazi ya shuruti katika Jamhuri ya Muungano.

(3) Kwa madhumuni ya ibara hii, na katika Katiba hii kwa jumla, ifahamike kwamba kazi yoyote haitahesabiwa kuwa ni kazi ya shuruti au kazi ya kikatili au ya kutweza endapo kazi hiyo, kwa mujibu wa sheria ni-
(a) kazi inayobidi ifanywe kutokana na hukumu au amri ya mahakama;
(b) kazi inayobidi ifanywe na askari wa jeshi lolote katika kutekeleza majukumu yao;
(c) kazi ambayo mtu yeyote inabidi aifanye kutokana na
kuwapo hali ya hatari au baa lolote linalotishia uhai wa ustawi wa jamii;
(d) kazi au huduma yoyote ambayo ni sehemu ya-
(i) majukumu ya kawaida ya kuhakikisha ustawi wa jamii;
(ii) ujenzi wa taifa wa lazima kwa mujibu wa sheria;
(iii) jitihada za taifa za kutumia uwezo wa kila mtu kufanya kazi kwa ajili ya kuimarisha jamii na uchumi wa taifa na kuhakikisha maendeleo na tija ya kitaifa.

IBARA YA 7.-(1)(a) IFANYIWE MAREKEBISHO; Wabunge angalau wawe na elimu kuanzia shahada ya kwanza. Mbunge mwenye elimu duni ni mzigo kwa taifa.

7.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;

IBARA YA 74.-(2) IONDOLEWE; Sio vema Rais ambaye pia ni kada wa chama cha siasa kitakachoshiriki uchaguzi kuteua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. Huyu mwenyekiti kuwa huru na kazi yake ni mtihani mzito.

74.- (2) Rais atamteua Makamu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kwa kufuata kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.

Waungwana karibuni nanyi mtaje ibara zingine.
 
Katiba ni hii hii tu,

Mzanzibari tukubaki alituzidi akili kiasi kwamba hata Tanganyika ikapotea ila Zanzibar bado ipo

Yani kwenye kazi wazanzibari wanapewa asilimia 21 ya kazi za huku, khaaa!! Kiukweli ilikuwa ni akili kubwa.
 
Ibara ya 63(3)(e) inasema ili mikataba ya nchi ijadiliwe na Bunge ni sharti 1) iwe ni baina ya Tanzania na nchi nyingine 2) lazima mikataba hiyo iwe na sharti kwamba Bunge liridhie.

Ibara hii inalizuia Bunge kuitisha na kujadili mikataba ambayo Serikali inasaini kati yake na nchi nyingine na au wawekezaji
 
Hapa hakuna Cha kujadili viraka,tunahitaji katiba iliyochambuliwa na tume ya walyoba ambayo walipiga kila mkoa na wilaya zake.tunataka Sasa katiba rais asaini ili tuipigie kura watanzania
 
Hii ni fursa ya mabadiliko ya sheria zilizopitwa na wakati na sio vifungu vya Katiba au nasema uongo ndugu zangu?

Waanzishe sheria ya local content kuwalazimisha wakandarasi wa nje kutoa angalau 35% ya value ya miradi kwa wakandarasi wa ndani .
 
Yaani Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba, ambayo kimsingi ndiyo Katiba Tarajiwa ya Wananchi, ipo kwenye makabati yenu!

Nyinyi bado mnatuletea hiyo Katiba iliyojaa viraka!
Watanzania tunataka Katiba Mpya! Na siyo hiyo ya ccm ya 1977!
 
Ambao hata katiba ya sasa hatuijui ila tunataka katiba mpya ndio tuna comment wapi?
 
Yaani Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba, ambayo kimsingi ndiyo Katiba Tarajiwa ya Wananchi, ipo kwenye makabati yenu!

Nyinyi bado mnatuletea hiyo Katiba iliyojaa viraka!
Watanzania tunataka Katiba Mpya! Na siyo hiyo ya ccm ya 1977!
Umeelewa uzi?
 
Hapa hakuna Cha kujadili viraka,tunahitaji katiba iliyochambuliwa na tume ya walyoba ambayo walipiga kila mkoa na wilaya zake.tunataka Sasa katiba rais asaini ili tuipigie kura watanzania
Walyoba = Warioba. Wewe kwa uandishi wako huu uzi haukuhusu. Uelewa wako ni mdogo.
 
Tuwekee Rasimu ya Katiba ya Warioba tuione kwanza na tuijadili tulinganishe na mapendekezo yako. Usijibu watu kwa ujeuri.
Uwekewe kama nani? Nitolee upumbavu hapa. Majitu hamjui chochote kuhusu katiba mnafuatisha wanavyoropoka kuhusu rasimu ya Warioba. Pumbavu sana
 
Uwekewe kama nani? Nitolee upumbavu hapa. Majitu hamjui chochote kuhusu katiba mnafuatisha wanavyoropoka kuhusu rasimu ya Warioba. Pumbavu sana
Unaanzisha uzi, halafu unawashambulia wachangiaji kwa matusi na kejeli! Yaani unataka tuchangie kwa kuegemea kwenye mtazamo na mawazo yako!!!
 
Unaanzisha uzi, halafu unawashambulia wachangiaji kwa matusi na kejeli! Yaani unataka tuchangie kwa kuegemea kwenye mtazamo na mawazo yako!!!
Uzi unahusu katiba iliyopo halafu anajitokeza mpumbavu na kusema niwawekee rasimu ya Warioba huoni kama ni ushenzi?
 
Back
Top Bottom