Mkuu hili nalo Ni tatizo la mtazamo wako.
Hapa Tz karibia kila mkoa watu wake wamejazana Sana tu,mfano wachaga wamejaa Sana kimara,nao tuseme wamepakimbia Kilimanjaro kisa huko hakuna cha maana?
Alafu Kumbuka Lindi ipo karibu na dsm so mtu wa Lindi Ni rahisi kuja Dar kutafuta maisha maana Ni mji mkubwa,na miji mikubwa duniani kote watu hukimbilia huko hasa vijana ili kujikwamua na maisha.
Na ukisema kusini Kuna fursa ya mazao tu,hivi Tanzania hii ukiondoa mini mikubwa kama dsm,Arusha(utalii) na Mwanza biashara,miji iliyobaki Kama Moro,Iringa,Lindi,mtwara nk,nje na kilimo Kuna fursa gani zingine za maana? Tena ni Mara kumi Lindi na mtwara Kuna kilimo Cha mazao mengi mfn,msimu wa mbaazi,wa korosho,wa kunde na choroko,wa mahindi na mpunga,wa maembe (Sasa hivi embe za kusini zimejaa Dar),ambapo inapelekea angalau mzunguko wa fedha unakuwepo kulinganisha na mikoa yenye kutegemea zao moja Kama ndizi!!? Na ndiyo maana si ajabu kuona Lindi na mtwara zipo top ten mwezi huu December ya gdp per capital. Pesa angalau inakutana misimu ya mazao ipo mingi kulinganisha na mikoa/maeneo mengine.
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.
Sent from my CPH1923 using
JamiiForums mobile app