Karibuni Ruangwa

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,216
2,814
Wananchi na wakazi wa Ruangwa tuna bahati sana na iwapo tutatumia bahati hiyo basi tutanufaika sana katika level ya mtu mmoja mmoja, vikundi, vyama mashirika na hata taasisi nk.

Mtumishi wa Ruangwa atakayeshindwa kuishi (kufanyia kazi katika wilaya ya) Ruangwa basi huyo hawezi kwenda kwingine akafanikiwa.

Mishemishe zilizopo Ruangwa mjini zimekaa kitown town sana mpaka raha. Cheki bodaboda wanavyorun kazi zao, cheki mama ntilie cheki machinga cheki wenye biashara zao tofauti na hizo cheki... yaani mwenyewe utakubali.

Ruangwa ina fursa nyingi sana kubwa kubwa kwa ndogo ndogo. Siwezi kuzitaja zote hapa lakini wewe fika tu ujionee fursa hizo katika sekta zote ikiwemo kilimo (ufuta na korosho), biashara (kubwa na ndogo) na madini (dhahabu, bunyu nk).

Yote hayo pongezi ziende moja kwa moja kwa Mbunge wetu Mzee Kasim Majaliwa (kwangu yeye ni Mzee sawa na mzee wangu (yaani baba)). Mzee huyu ameufanyia haki ubunge wake haswaa na mimi binafsi nakiri ni mara ya kwanza kuona mwanasiasa (mbunge) akijitoa kiasi hiki kwa wananchi wake waliomchagua.

Ruangwa ile si Ruangwa hii, kama unatafuta mahala penye fursa za kupiga hela basi jisogeze tu Ruangwa na wala hutojutia, na kama uliikimbia hapo nyuma kwa sababu fulani fulani ndugu yangu rudi nyumbani kumenoga!

Hatukatai kuhusu changamoto kwani hakuna kizuri kikakosa kasoro (isipokuwa MwenyeziMungu). Namaanisha kuna changamoto kadhaa pia wilayani Ruangwa lakini za kawaida na binafsi nimeshazipeleka sehemu husika hivyo sitaziongelea hapa kwani sijajia hilo leo nimekuja kumwaga uzuri wa Ruangwa tu!.

Napenda niwaambie tu Wanaruangwa wenzangu na wengineo ni kwamba huyu kiongozi wetu (mbunge) kwa mambo aliyoyafanya Ruangwa hii basi ikitokea mtu anamzungumzia vibaya basi ni kwa vile hajui tu au anafuata mkumbo.

Laiti ingekuwa siyo 'kila kitu na muda wake' basi Mzee Majaliwa angeendelea kuwa kiongozi wetu tu mpaka Mungu mwenyewe atakapopenda maana sidhani kwa mazuri haya kama kuna ambaye angeweza kuchuana naye.

Kuna wanaosema eti kigezo (cha maendeleo haya) ni uwaziri ila nawapinga vikali kwakuwa yeye si waziri wa kwanza!

Wewe ambaye upo Ruangwa watafutie 'wanaokuhusu' maeneo na kazi za kufanya katika wilaya hii ili baadae msije kujuta. Kizuri kula na nduguyo ndugu zangu watanzania mimi nimeshamaliza kwa upande wangu kazi ibaki kwenu msije kusema sikuwaambia! Naiona Ruangwa ya kipekee sana miaka kuanzia mitano ijayo. Changamkieni fursa.

KARIBUNI RUANGWA!
 
Endeleeni kufurahia upendeleo, kama chato walivyofurahia, sasa hivi wanalia.
Upendeleo kivipi boss kwani hao wawekezaji wameshikiwa bunduki kwamba wasiende kwingine!? Mwambie Mbunge wako ajitahidi kuwavutia watamuelewa tu wala hakuna uchawi katika hili
 
Kati ya viongozi wakubwa wa nchi hii wanaoongoza kutotendea Haki Jimbo analotoka basi MEMBE anaongoza.

Mpaka anastaafu ubungena kuamua kugombea Urais Jimbo la mtama liko hovyo pamoja na jina kubwa la viongozi iliyowazalisha kuanzia aliyepita (MEMBE ) na hata huyu wa sasa Nape hakuna cha maana alichofanya Hadi sasa..Mtama sijui wanafeli wapi asee

Hongera Wana Ruangwa Kwa maendeleo

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Sijawahi kufika Ruangwa, lakini mazungumzo yako katika habari hii yamenifanya niamini kwa asilimia mia (100%). Kwanza, ni kutokana na huyo unayemzungumzia. Nadhani sio mimi tu nimeamini maneno yako; wapo wengi wameamini uliyoyaandika.

Kuna watu wakizungumziwa kuwa wameleta maendeleo mahala fulani, unaweza kushangaa na kuhoji jambo hilo, kwa kuwa hawakuzoea kumwona akifanya hivyo. Kwa Majaliwa, hakuna asiyejuwa utendaji wake. Najaribu kufikiria, hii husababishwa na nini?; ni tabia ya mtu, malezi aliyopewa na wazazi wake, au ni shinikizo?

Kwa mtu anayemfuatilia mzee huyu atagundua kuwa Majaliwa alikulia kwenye maadili mazuri. Kwa hiyo anachofanya sasa hivi sio maigizo, bali ni tabia aliyonayo tangu utotoni mwake. Lakini pia alikomazwa zaidi alikopitia katika maisha yake; shuleni, vyuoni, kazini, nk.

Nawapongeza Wanaruangwa, mmepata jembe, mtafika mbali sana, hayo mnayoyaona sasa ni manyunyu tu, mvua yenyewe bado.
 
Mkuu karibu mibure,namakuku,njawale ujionee Ruangwa yetu hasa nyakati za mvua....ila town MP big up sana amepaweka vzr
 
Mimi niliwai kukaa nyumba za national housing Ruangwa na Mh Majaliwa akiwa Naibu waziri

Huyu mtu ana moyo wakipekee sana. Majaliwa umewajali sana Watumishi wa serekali sana
Umefanya mambo makubwa sana Ruangwa ilikuwa nyuma sana

Mwenyenzi Mungu Mtakatifu akubariki sana ndugu yangu
 
Back
Top Bottom