Ruangwa, Lindi, Nanjilinji, Kilwa, Tunduru , Nachingwea ni Choka mbaya mara mia niishi Singidani au Masasi why sijasema Mtwara kubaya au Masasi coz kunamzunguko ila apo
Ukweli mchungu Ruangwa ni jehanamu ndogo unaongolea rami kuwekw [emoji23][emoji23][emoji23] mwaka wa tano huu porojo tu eti ohh barabara ina daraja nyingi..
Aya sema hapa Ruangwa ina vituo vingapi vya mafuta maana ni wilaya iyo.
Ruangwa ina supermaket ngapi, kampuni za mabasi yanayokuja na kurudu dar, kuna bakery hapo, bank ipo NMB na CRDB tofauti na izo zipo nyingine?
Unasema kuna shule za sekondari advance zaidi ya tano zitaje hapa.
Tunaomba taarifa ya mapato ya wilaya yako tuilinganishe ata na Tabora.
Wilaya nzima utatafuta kajisehemu kakupoa kula ata Pizza hakuna, watu wanakalia majungu tu.
Kwanini Maambukizi ya HIV yapo juu maana wamwela wanapenda kudinyana, uongo, majungu, ujuaji kufatilia maisha ya watu.
Apo karibu na mahakama kuna bar bondeni nlikua nakaa apo sana na mkuu wa mkoa na Mkurugenzi bro Ruangwa hakuna Fursa, utaanzisha kitu kitakufa au unataka nikupe mfano wa project nlizo anzisha zikafa?
Apo kama unaenda halmashauri si kuna fremu mpya mbona biashara zinafungwa?
Nimezunguka vijiji vyote Ruangwa maana kazi yangu ilikua inahusisha field sana, shule zote, ofisi za vijiji, zaanati nimezunguka apo Ruangwa mpka lindi mjini ni hoehae, Kilwa kisiwani, kilwa masoko na kivinje kote Elimu hakuna kusini zaidi ya porojo na udini sana plus umwinyi nyie mtu akifanikiwa mnahamia wote kwake.
Shida unakurupuka sana, punguza jazba
Lami imeongelewa muda mrefu sana, ni kweli. Ila nina wasiwasi ujenzi ulipoanza tu basi na ww ukahama Ruangwa maana sasahivi ujenzi upo ukingoni kabisa na haifiki mwakani April, mambo yote ni swafii. Nashangaa wewe unatapika pumba humu kama mtu aliyeishi Ruangwa miaka ya 90 vile.
Serious, unaulizia vituo vya mafuta Ruangwa, mzima kweli wewe? Ruangwa kuna vituo vya mafuta kibao. Yaani Ruangwa mjini tu vipo vingi hadi vinakera.. mi sijui vingapi, kaviangalie hata Google Maps basi uache kupayuka
Sasahivi unaulizia bakery wakati Royal Pub wameanzisha bakery kitambo tu na kila siku wanauza mikate mingi kwa wanaruangwa ukikosa basi wewe mwenyewe ndio ZOBA. Nikikuambia wewe ni mvivu mkuu, unakataa.
Halafu hata sitaki unitajie project zako ulizozianzisha zikafeli maana kwenye maisha kuna watu wana bahati mbaya tu, kila wanachoanzisha kinafeli. Pengine wakati unakaa Ruangwa ulikuwa na Nyota Chafu tu maana watu kibao wameanzisha biashara na wamefanikiwa. Au labda huna akili za biashara.
Supermarket ipo moja tu, hiyohiyo inakidhi mahitaji ya wanaruangwa kwa sababu wamwera hawazaliani ovyo.
Kwa shule kama una hela unampeleka mwanao private tu, na anasoma anafaulu. Pia iko wazi kabisa kuwa Wamwera hawapendi kusoma kwani nani hajui hilo?
Unaongelea zahanati mkuu, we uliishi Ruangwa gani. Kwanza sasahivi hospitali ya wilaya sasahivi imekuwa zahanati, ikajengwa hospitali moja bomba sana. Zahanati zipo nyingi we mwenyewe tu ulikuwa mvivu kutafuta
Shule za Advance kwa haraka haraka naweza kutaja Lucas Maria, Nkowe, Mbekenyera, Kassim Majaliwa, Mandawa na nyingine nisizozijua.
Pato la wilaya mi sijui, halafu kama wewe unaona ni dogo basi angalia hata na population ya Ruangwa. Nimeshakuambia Wamwera hawazaliani ovyo.
Kama ulitafuta sehemu za kula bata hata na kupoa na mademu halafu ukakosa basi wewe ni ZOBA sana. Yaani Kidia Hotel, Ruangwa Executive Lodge, Royal Pub, Ifram Lodge, Natii Pub na vibaa vyote hivi vya mjini ulishindwa kupata. Ruangwa Supermarket kwa nyuma na mbele kuna sehemu ya kula bata.
Sasahivi Pride Hotel ndo inakamilika na ina swimming pool nzuri, ningekutumia picha ila bahati mbaya ninatumia tablet sio simu. Naona tu jau kwenda nayo kupiga picha
Kama we uliiona Ruangwa jehannum basi pole, sisi tunaiona pepo[emoji41]