jamani people, mbona hivi. naomba mjue sisi wote ni wamoja, wote ni watanzania. miaka yote tumeishi tukiongozwa kwa misingi ya amani, upendo, ushirikiano na mshikamano. Inakuaje tena hivi leo mambo hayo yametoweka ghafla? jamani me nasema hakuna kisasi kiletacho uzima hata siku moja bali ni maangamizo tu. Tuache kulipiza visasi na jeuri zisizo za misingi. sisi ni wamoja tupendande tu tukiachilia mbali tofauti zetu za kikabila na udini, tuwe na utaifa wote ni watanzania. biashara za kupigana sisi wenyewe ndani ya nchi yetu hazilipi kabisa. Mungu ibariki Tanzania na watu wake.