Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu

Siku hizi ukiandika vitabu nani atavisoma. Miaka ya sabini hadi themanini watu walikuwa wanasoma sana vitabu; hata wazee wa huko vijijini waliokuwa wamejifunza kusoma na kuandika kwa njia ya elimu ya watu wazima walikuwa pia wanasoma sana vitabu hivyo. Kulikuwa na vitabu vilivyoandikwa na waandishi mahiri kama F. H. H. Katalambulla (aliandika vingi ila kile cha Simu ya Kifo ndicho kilikuwa maarufu sana na kuna wakati kilitumiwa kwa somo la fasihi ya kiswahili UDSM, na kilitolewa kama mchezo wa kuigiza na RTD), Euphrase Kezilahabi (aliandika vingi lakini kilichovuma zaidi ni Rosa Mistika), Casimiri Kuhenga, Penina Muhando (kitabu chake maarufu kilikuwa Wakati Ukuta ingawa aliandika riwaya nyingine pia),Hemedi bin Abdallah Buhriy (alikuwa mtunzi mzuri sana wa vitabu vya mashairi na tenzi), John B. Kabeya, Taban lo Liyong, David G Maillu (kitabu chake kimoja kilichojulikana kama Unfit for Human Consumption na kingine After 4:30 vilikuwa maarufu sana kwa vijana wakati huo), Adam Shafi Adam (kitabu chake cha Kuli kilikuwa maarufu sana), na Elistabalus Elvis Musiba (vitabu vyake vingi vilikuwa ni marudio ya hadithi za Nick Carter lakini akiziweka katika mazingira ya kikwetu; kimojawapo maarafu kilikuwa ni kile cha Kufa na Kupona), Gabriel Ruhumbika (yeye aliandika zaidi vitabu vya fasihi ya kiingereza, ila kitabu chake cha Uwike usiwike kutakucha kilikuwa maarufu sana nacho)

SIjui kama waandishi maarufu hao wote bado wako hai ila sasa tumempoteza Prof Kezilahabi.

Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu Kezilahabi
 
Japo mimi si wa makamo sana ila husoma sana Vitabu vya hawa nguli wa fasihi.

E. Kezilahabi nimesoma vitabu vyake kadhaa. Nilipenda zaidi Rosa mistika. Aisee hicho hakiishi utamu. Kinaendana na mazingira ya kila namna. Ama kwa hakika kila nikikisoma hugundua jambo jipya katika mtoririko wa aya zake.

Vile vile Dunia uwanja wa fujo nakumbuka harakati za Tumaini na jinsi alivoishia hukumu ya kunyongwa.

Kiufupi, mimi hupendelea riwaya zenye Kunga na uficho fulani kifasihi ambao hauhitaji mtu uelewe moja kwa moja kinachozungumzwa.
Ndio maana Hussen Tuwa nae huwa ananikamata sana na mfululizo wa vitabu vyake.
Ben R. Mtobwa nae huwa sishibi bubujiko la lugha yake ya kifasihi.

Nina soft copy ya Rosa mistika na Nagona. Ila nashindwa kuviattach hapa. Nielekezeni
Mkuu kama ikikupendeza nikutumie hata email unitumie
 
Siku hizi ukiandika vitabu nani atavisoma. Miaka ya sabini hadi themanini watu walikuwa wanasoma sana vitabu; hata wazee wa huko vijijini waliokuwa wamejifunza kusoma na kuandika kwa njia ya elimu ya watu wazima walikuwa pia wanasoma sana vitabu hivyo. Kulikuwa na vitabu vilivyoandikwa na waandishi mahiri kama F. H. H. Katalambulla (aliandika vingi ila kile cha Simu ya Kifo ndicho kilikuwa maarufu sana na kuna wakati kilitumiwa kwa somo la fasihi ya kiswahili UDSM, na kilitolewa kama mchezo wa kuigiza na RTD), Euphrase Kezilahabi (aliandika vingi lakini kilichovuma zaidi ni Rosa Mistika), Casimiri Kuhenga, Penina Muhando (kitabu chake maarufu kilikuwa Wakati Ukuta ingawa aliandika riwaya nyingine pia),Hemedi bin Abdallah Buhriy (alikuwa mtunzi mzuri sana wa vitabu vya mashairi na tenzi), John B. Kabeya, Taban lo Liyong, David G Maillu (kitabu chake kimoja kilichojulikana kama Unfit for Human Consumption na kingine After 4:30 vilikuwa maarufu sana kwa vijana wakati huo), Adam Shafi Adam (kitabu chake cha Kuli kilikuwa maarufu sana), na Elistabalus Elvis Musiba (vitabu vyake vingi vilikuwa ni marudio ya hadithi za Nick Carter lakini akiziweka katika mazingira ya kikwetu; kimojawapo maarafu kilikuwa ni kile cha Kufa na Kupona), Gabriel Ruhumbika (yeye aliandika zaidi vitabu vya fasihi ya kiingereza, ila kitabu chake cha Uwike usiwike kutakucha kilikuwa maarufu sana nacho)

SIjui kama waandishi maarufu hao wote bado wako hai ila sasa tumempoteza Prof Kezilahabi.

Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu Kezilahabi
watu wanaangalia sana TV siku hizi hawana muda wa kusoma vitabu taifa linaangamia
 
Ila huyu Kezilahabi alikuwa na lugha kalikali. Kwenye Dunia uwanja wa fujo kuna kabinti kalibalehe na kakaanza ishu za wavulana vichakani. Basi dingi yake akakakamata na kuanza kukapa stiki huku akisema " vimatako vyenyewe vikavu halafu unataka kutuletea nyege"
Napataje soft copy?
 
Back
Top Bottom