Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Messages
6,332
Points
2,000

GuDume

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2015
6,332 2,000
Huyu E. Kezihalabi ni nani?

Euphrase Kezilahabi alizaliwa 13 Aprili 1944 huko Namagondo kisiwani Ukerewe kilichopo ndani ya Ziwa Viktoria. Babake Vincent Tilibuzya alikuwa msimamizi wa kijiji na Euphrase alikuwa na ndugu 10 yaani wavulana 5 na wasichana 5. Alisoma shule ya msingi ya Nakasayenge halafu tangu 1957 Seminari ya kikatoliki ya Nyegezi aliyomaliza mwaka 1966.

1967 alijiandiskisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akasoma ualimu na fasihi hadi digrii ya B.A. katika mwaka 1970. Mwaka uleule 1970 akawa mwalimu wa shule ya sekondari Mzumbe (Morogoro) halafu kwenye shule ya sekondari ya Mkwawa (Iringa).

1971 alirudi chuoni Dar es Salaam akawa mhadhiri msaidizi wa chuo alipoandika pia tasinifu ya M.A. kuhusu riwaya za Shaaban Robert, tangu 1974 mhadhiri kamili na 1978 mhadhiri mwandamizi. Akaendelea na masomo ya Ph.D. huko Marekani kwenye Chuo Kikuu cha Wisconsin Madison alipotoa tasinifu yake mwaka 1985 kuhusu "African Philosophy and the Problem of Literary Interpretation". Sasa (mwaka 2012) ni profesa wa lugha za Kiafrika kwenye Chuo Kikuu cha Botswana.

Uandishi wake fikirishi uliowahi mletea shida sana kisiasa

kwa wale wenzangu ambao wamekuwa na utamaduni wa kujisomea bila shaka napotaja jina la Euprase Kezihalabi si geni masikioni mwao. Ukiacha ambao walisoma vitabu vyake wakiwa shule kwenye fasihi. binasfi nilianza kusoma vitabu vyake nikiwa nyumbani nikisoma kama burudani kabla ya kuja kufaham baadaye kile kilichokuwa kimeandikwa na athari zake. Nilisoma vitabu kama Rosa Mistika, Kichwa maji ,Dunia Uwanja wa Fujo,Gamba la Nyoka na Kaptula la Marx.

Vitabu hivi vitatu vilikuwa na ukakasi mwingi sana kufikia hatua viwili kati yake kufungiwa au kuzuiwa kuuzwa. Rosa Mistika na Kaptula la Max.

Nilisoma zamani sana Kichwa Maji...nimesahau kiasi maudhui yake lakini ni moja ya vitabu ambavyo naamini watanzania tunapopata muda wa kusoma tunapaswa kuvisoma na kuilewa fasihi ni nini.

Huwa unasoma vibonzo vya Masudi Kipanya? Ile ni fasihi kama ambavyo ungesoma kitabu ukakielewa kilichozungumzwa.

Kaptula la Marx

Ni kejeli kali kuhusu siasa ya Tanzania hasa ya Ujamaa na rais wa wakati ule Julius Nyerere.

Kutokana na ukali wa ukosoaji wake, tamthiliya haikuchapishwa hadi mwaka 1999 ingawa ilifanyiwa uigizaji wa kwanza Septemba 1988 huko Bagamoyo kwenye Tamasha la 7 la Sanaa na Utamaduni wa Mtanzania.

Tamthiliya ina sehemu 6 ambako mchezo hubadilisha mahali pake kati ya gereza lenye wafungwa 6 pamoja na kiongozi wao "Mwangaza Africanus" na serikali ya nchi isiyotajwa jina chini ya Rais anayeitwa Kapera.

Chanzo ni jaribio la wafungwa gerezani kukusanya habari nyingi za "dunia ya nje" iwezekanavyo kwa kuiangalia kupitia shimo dogo ukutani.

Wakati huohuo raisi anayeitwa Kapera baada ya kusoma Max anaamua kubadilisha siasa yake kwa manufaa ya watu wengi. Kwa kusudi hii anaamua kuvaa "Kaptula la Max" na shati ya Mao. Nguo zote mbili ni kubwa mno kwake. Mawaziri wake wanamwitikia na kuvaa vilevile. Pamoja wanaondoka walipo kutafuta nchi ya usawa.

Katika sehemu ya 4 wanaondoka kuelekea nchi ya usawa na undugu. Njiani wanakutana na jitu anayeitwa "Korchnoi Brown" na kuwapa maelekezo. Lakini wanashindwa kufika kwa sababu mawaziri hawafai.

Wafungwa gerezani wakati huohuo wanafanya maigizo kati yao wakijadili siasa ya nchi. Mwangaza Africanus anasoma ujumbe kwa viongozi wa Afrika anapokataa siasa zao.

Mawaziri wanaonyeshwa baadaye jinsi walivyo kama vipofu na kutumia mateso ya wafungwa kama mbinu.

Katika sehemu ya mwisho wafungwa wanatoka nje na kupindua serikali ya Kapera anayesalitiwa na mawiziri wake. Kicheko cha Korchnoi Brown kinafunga thamthiliya.

Mazingira ya kuandikwa kwa "Kaptula la Marx"

Kezilahabi aliandika "Kaputula la Marx" mara baada ya maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 5 Machi 1978 na azimio la rais Nyerere kuwafukuza wote chuoni na kupioga marifuku umoja wao DUSO.

Kezilahabi aliyekubali hoja za wanafunzi alishtuka sana kutokana na matendo ya viongozi wa chuo na siasa waliokataa kuwasikiliza. Tamthiliya iliandikwa haraka na kusambazwa kwa kopi lakini haikufanyiwa uigizaji wakati ule. Hata hivyo ilisomwa na watu wengi waliipenda. Kampuni ya Tanzania Publishing House ilitaka kuchapisha tamthiliya lakini iliambiwa na serikali kutoendelea.

Nukuu:

Maelezo ya jitu Korchnoi Brown kwa Rais Kapera na mawaziri waku kuhusu njia ya kufikia nchi ya usawa:

“Mtakwenda! Halafu mtapinda, mtapinda tena, halafu tena mtapinda, mwishowe mtapindapinda hadi mtakapofika mabonde yenye matope. Mtapita katikati ya matope. Halafu milima, halafu misitu yenye miiba hadi mtakapofika jangwani. Kutoka jangwani mtaingia tena bondeni chini kwa chini hadi baharini. Hakuna mitumbwi wala ngalawa. Mtaogelea, ingawa kuna papa wengi. Mkishavuka mtafika nchi iitwayo Svoboda. Kabla ya kuondoka katika nchi hii itawabidi kupambana na majitu yanayofanana na mimi. Mkitoka hapo mtafika kwenye njia nyembamba. (Akiwaonyesha mawaziri) Hawa hawatapita hawa! Njia hiyo itawafikisha katika nchi iitwayo Fraternite. Kutoka Fraternite mtafika Usawa. Ulizeni tu watu watawaonyesha! Mkifika Usawa mtawakuta Waswahili wenzenu wameketi nje ya ikulu ndogo ya Ravensto” (Kaptula la Marx uk. 20)"
jaribu kusoma kitabu hiki na kingine uongeze mbolea katika ubongo wako

Kwa hisani ya wikipedia pia.

Fungua kiambatanisho kujisomea.
Max.jpg
 
Attachments:

Last edited:

Rita Warobi

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2017
Messages
346
Points
1,000

Rita Warobi

JF-Expert Member
Joined May 17, 2017
346 1,000

Kwa hisani ya wikipedia pia
Hiki kitabu nilikua natamani sana kukisoma , kama kuna mtu anaweza kunambia nawezaje kukipata hata online nitafurahi sana
 
Taso

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2010
Messages
2,026
Points
2,000

Taso

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2010
2,026 2,000
Hivi kwa zama hizi ambazo kumkosoa mh.rais ni kosa la jinai
eti zama hizi kumkosoa mheshimiwa ni kosa, ni lini ilikuwa sio kosa ?

umesoma kilichoandikwa humu kwamba hiki kitabu kilipigwa marufuku?

halafu tunaambiwa Nyerere alikuwa hapigi mawazo makonzi...

wazee waongo kweli hawa
 
Thad

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2017
Messages
12,053
Points
2,000

Thad

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2017
12,053 2,000
eti zama hizi kumkosoa mheshimiwa ni kosa, ni lini ilikuwa sio kosa ?

umesoma kilichoandikwa humu kwamba hiki kitabu kilifungiwa?

halafu tunaambiwa Nyerere alikuwa hapigi mawazo makonzi...

wazee waongo kweli hawa
Ingekuwa zama hizi, kisingefungiwa kitabu tu bali hata mtunzi angefungwa!
 
Raja msomi

Member
Joined
Oct 29, 2019
Messages
10
Points
45

Raja msomi

Member
Joined Oct 29, 2019
10 45
Mkuu zamani wabongo walikuwa wanaandika Fasihi bora sana. Sikuhizi ukikuta riwaya zinazouzwa hazivutii hata kusoma na macover yao ya marangirangi.
Nilibahatika kusoma Dunia uwanja wa fujo.Hicho Kaptula la Marx sijawahi soma. Ni wakati wa serikali na Baraza linalohusika wafungulie vitabu walivyofungia. Kuna kile shamba la wanyama/ Animal farm na kile the dark side of Nyerere. Hakuna haja ya kuendelea kuvifungia. Kuna kitabu kimoja cha zamani kinaitwa Bosi, umewahi kisoma?
 
BabaDesi

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2007
Messages
3,375
Points
2,000

BabaDesi

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2007
3,375 2,000
...Kweli, Mkuu. Mzee wetu Kezilahabi alikuwa na Lugha Kali, ambazo zilionekana Kali zaidi kutokana na Nyakati hizo.
Kwenye 'Roza Mistika' kuna sehemu anaelezea kuhusu Roza kupita mbele ya Wanafunzi wenzake huku kigauni chake kikiwa kimeingia katikati ya matako take huku yeye akiwa hajui! ...nahisi Sikh hizo tungesema tu nguo imeingia katikati ya makalio...kama sio tu 'Nguo imeingia Kabatini' !
Ila huyu Kezilahabi alikuwa na lugha kalikali. Kwenye Dunia uwanja wa fujo kuna kabinti kalibalehe na kakaanza ishu za wavulana vichakani. Basi dingi yake akakakamata na kuanza kukapa stiki huku akisema " vimatako vyenyewe vikavu halafu unataka kutuletea nyege"
 
Forum statistics

Threads 1,355,857
Members 518,781
Posts 33,121,550
Top