Gota8s
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 203
- 189
Japo mimi si wa makamo sana ila husoma sana Vitabu vya hawa nguli wa fasihi.
E. Kezilahabi nimesoma vitabu vyake kadhaa. Nilipenda zaidi Rosa mistika. Aisee hicho hakiishi utamu. Kinaendana na mazingira ya kila namna. Ama kwa hakika kila nikikisoma hugundua jambo jipya katika mtoririko wa aya zake.
Vile vile Dunia uwanja wa fujo nakumbuka harakati za Tumaini na jinsi alivoishia hukumu ya kunyongwa.
Kiufupi, mimi hupendelea riwaya zenye Kunga na uficho fulani kifasihi ambao hauhitaji mtu uelewe moja kwa moja kinachozungumzwa.
Ndio maana Hussen Tuwa nae huwa ananikamata sana na mfululizo wa vitabu vyake.
Ben R. Mtobwa nae huwa sishibi bubujiko la lugha yake ya kifasihi.
Nina soft copy ya Rosa mistika na Nagona. Ila nashindwa kuviattach hapa. Nielekezeni