JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
KANUNI ZA BUNGE ZATENGULIWA KUPISHA MFUNGO
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetengua Kanuni kwa ajili ya kuruhusu Mfungo wa Mwezi wa Ramadhan ambapo mabadiliko hayo yataendelea hadi mwisho wa mfungo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, George Simbachawene amewasilisha hoja hiyo Bungeni Aprili 5, 2022, ambapo Kanuni ya 34 (2) na 34 (4) ya Kanuni za Kudumu za Bunge zimetenguliwa ili shughuli zimalizike mapema.
Lengo ni kuwaruhusu Waumini wa Dini ya Kiislam kuswali na kufuturu kwa wakati muafaka, hivyo mwisho wa shughuli za Bunge utakuwa saa 12:00 jioni badala ya saa 1:45 Usiku.
Source: TBC