Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
Steven Charles Kanumba.
Na Hemed Kisanda
Mwigizaji the big name ndani na nje ya Bongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great' amesema licha ya kuwa kwenye orodha ya mastaa watakaokosa zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi Mkuu Jumapili Ijayo kwa sababu flani, amejipanga kuwania ‘uheshimiwa' kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake maeneo ya Meeda Sinza, Dar, Kanumba anayemiliki kampuni ya ‘Kanumba Film Co' alisema kuwa ameamua kuweka wazi mipango yake hiyo ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, alikozaliwa.
"Nimejipanga kugombea Ubunge kwenye uchaguzi mkuu utakaofuata baada ya huu tunaofanya Jumapili kwani nitakuwa nimekomaa kifikra," alijigamba The Great.
Source: Global Publishers