Kanumba: Sipigi kura, 2015 nitagombea ubunge

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Kanumba2.jpg

Steven Charles Kanumba.

Na Hemed Kisanda

Mwigizaji the big name ndani na nje ya Bongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great' amesema licha ya kuwa kwenye orodha ya mastaa watakaokosa zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi Mkuu Jumapili Ijayo kwa sababu flani, amejipanga kuwania ‘uheshimiwa' kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake maeneo ya Meeda Sinza, Dar, Kanumba anayemiliki kampuni ya ‘Kanumba Film Co' alisema kuwa ameamua kuweka wazi mipango yake hiyo ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, alikozaliwa.

"Nimejipanga kugombea Ubunge kwenye uchaguzi mkuu utakaofuata baada ya huu tunaofanya Jumapili kwani nitakuwa nimekomaa kifikra," alijigamba The Great.


Source: Global Publishers
 
Akamuulize Nakaya kwanza.
Hivi ukiwa mgombea ndio huruhusiwi kupiga kura?
 
Bravo. ubunge siyo usanii na kama ni usanii aende kwa chama cha Msanii (CCM)
 
"Nimejipanga kugombea Ubunge kwenye uchaguzi mkuu utakaofuata baada ya huu tunaofanya Jumapili kwani nitakuwa nimekomaa kifikra," alijigamba The Great.
source:global publishers

Kugombea watakuwepo wengi tu ila kupata hilo ni shauri jingine............ajiandae angalau na Tshs 20 milioni za kuwalipa mawakala.................vinginevyo atakuwa ni msindikizaji tu.....na hilo kundi tunao wengi tu.......
 
Kwa tiketi ya chama gani?


Si unamuoana alivyo busy na mashati ya kijani?

Anafikiri atakuwa kama sugu, mwenzie mjanja alikuja CHADEMA chama kinachotoa fursa sawa kwa wote, yeye abaki huko kwa mafisadi halafu aulize yalimkuta shigongo!
 
Habari wanajamvi nilikua napita mnara wa voda eneo maarufu kwa mafundi vitanda ambapo pembeni kuna ofisi za CHADEMA Shy mkoa nkakuta tetesi kuwa msanii Steven Kanumba atarudi kugombea 2015 kupitia chadema against Masele wa CCM hebu tusaidiane je ina logic? Source mi
 
kwani anamapungufu gani ya yeye kuwa mbunge? Prof majimarefu na wenzake wanamzidi nini ambacho yeye hawezi kuwakilisha wananchi?
 
wakuu hi nimeitupia kama nlivyoikuta ikibishaniwa by the way jamaa shy ni kwao alaf yuko popular anauzika huyu!
 
ni haki yake kugombea
kama cantona anafikiria kugombea uraisi wa ufaransa kwanini kanumba asifikirie ubunge wa shinyanga......

mimi nawashauri wale ambao wanamwona hafai wampigie kura yule ambae wanamwona anafaaa, kama wagombea wote anawaona hawafai then itakuwa vizuri nao wakachukue fomu kwa ajili wao wanafaa
 
Back
Top Bottom