Kanisa la TAG mbona kama limepoa?

Kanisa la TAG mbona kama limepoa?

Ya kale..""" ? Kale ya muda gani...??? Makanisa ya Kipentekoste yote ni juzi juzi tuu....Ni makanisa ambayo hayana msingi....akifa mchungaji na kanisa linaporomoka
Msingi wa kanisa ni Yesu Kristo, siyo mchungaji!
 
Yule jamaa anaenda kuchomeka vibaya sana kama huko tuendako kukawa na hukumu...mzee wa "toa sadaka kwa namba za simu zinazopita kwenye kioo chako cha Tv kisha nitaziombea zirudi kwako maradufu kwa njia ya Mpesa TigoPesa na Airtel money".hahahah watu nao wanaitikia aaamen.yaani badala awahamasishe watu wakatafute ridhki zao kwa kufanya kazi anawaaminisha eti watoe aziombee zirudi kwao!
Ana balaa huyu jamaa nae . Kanisa lake liko Mwanza n'a ninafahamu lilipo hilo kanisa lake but conclusively wachungaji n'a manabii wengi wa kizazi hiki they are nothing but crooks and thugs who have turned gospel services /churches into robbery /bandits gangs . Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo utagundua hili , we mchungaji au so claimed Prophets wamejilibikizia utajili mkubwa sana watu wanasali kwenye mabanda na waumini ni maskini wa kutupwa na bado mtu anakwambia toa sadaka mungu akupe utajiri what kind of bullshit crap is this?
KWELI KANISA HILI LIMEPOA SAAANA SABABU 1. WACHUNGAJI WAMEKUWA NA TAMAA YA KUPENDA PESA KULIKO MAELEZO, WACHUNGAJI WA KANISA LA T.A.G WANASHINDANA KWA MAISHA YA ANASA NA KUWALAZIMISHA WAUMINI WAO WAWACHANGIE PESA WANUNUE MAGARI MAZURI. MFANO KUNA KANISA LIKO MOSHI- SOWETO NI LA T.A.G LIMELAZIMISHA KILA MUUMMINI ATOE LAKI MOJA NA ZAIDI ILI KUMNUNULIA MCHUNGAJI GARI BILA KUJALI UWEZO WA KIUCHUMI WA WAUMINI WAO 2. UBAGUZI NDANI YA KANISA UMEKUWA MKUBWA SANA, WENYE PESA WANAPEWA KIPAUMBELE MASKINI HAWATHAMINIWI 3. UKABILA 4. VYEO VYA UPENDELEO NDANI YA KANISA 5. RUSHWA KATIKA CHAGUZI ZA MAASKOFU, MFANO UCHAGUZI UKIKARIBIA HUWA MAASKOFU WANATOA PIKIPIKI NA MAGARI KWA WACHUNGAJI NA WAANGALIZI, UCHAGUZI UKIISHA TU HAWAGAWI TENA. 6. KUKOSA KANISA KUBWA HALINA TV WALA REDIO ILA VIJANA WADOGO TU KINA MWAMPOSA/BULDOZA WANA REDIO NA TV. 7. KUTOTOA HUDUMA ZA KIJAMII, KANISA LINA MATAWI NCHI NZIMA ILA HALINA HATA HOSPITALI..WANA SHULE MBILI ZA SEKONDARI NAZO ZINZ MIUNDMBINU MIBOVU KULILKO HATA SHULE ZA KATA.8. KUKOSA UPENDO MIONGONI MWA WACHUNGAJI WAO KWA WAO, WACHUNGAJI WA MAKANISA YA MIJINI WANAISHI MAISHA YA HALI YA JUU SANA ILA WENZAO WA VIJIJINI WANA HALI MBAYA SANA NA WALA HAWASAIDIANI 9.TABIA YA KURITHISHANA MAKANISA KIUKOO NA KINDUGU MFANO BABA AKIZEEKA ANAMUACHIA MDOGO WAKE AU MTOTO WAKE HILI NALO NI TATIZO KUBWA MFANO CALVARY TEMPLE ARUSHA(T.A.G)
 
Kaka kanisa hili la TAG mbona lipo vyema mpaka sasa tena linampango mkakati kabambe wa kuivuna Tanzania yote kwa Yesu mpango huo upewa jina la miaka 10 ya mavuno.Pia wametengeneza mpango wa kujenga vyuo vya kufundisha Theologia kila jimbo la makanisa yao.
Hakika wanafanya vyema zaidi ni kuwaombea ili wafanye vyema na wawe na uamsho wa kiroho katka nguvu kubwa.
Ni kanisa pekee la Kipendecost lenye mipango na maono makubwa ya kumtangaza Yesu likifatiwa na EAGT,FPTC,KLPT,P Holiness etc
NAkushauri uokoke na wewe ili urudishe huo moto uliopotea ambao Mungu amekuonyesha.
Barikiwa sana
Hivyo vyuo si vya kufundisha kuhubiri injili iliyo hai iletayo wokovu..Ni vyuo vya kufundisha mambo ya kawaida tu hapa duniani kama zilivyo elimu zingine za kidunia.Mambo ya roho mtakatatifu hayasomewi chuoni.
 
Mimi sio muumini wa TAG lakini nina uhakika hilo dhehebu halijapoa. Nimeingia kwenye makanisa yao kadhaa Wapo very smart hata katika ibada zao and perhaps it is the most smart pentecostal church in Tanzania! Hata Askofu mkuu wao tu ni Msomi wa PHD (Sio kama ya huyu mtukufu) na hata wasaidizi wake ni vichwa. Kwa hiyo mkuu halijapoa hilo chechi labda kwa awamu hii tu kwa sababu tunapitia kwenye jaribu zito wa Tanzania wote hasa financially, na mheshimiwa alishasema akiwa Singida pale siku ya mwaka mpya kuwa sadaka zita adimika hata makanisani!!!!
 
Sikuzote ivumayo haidumu, shida hapo ni Elim, hii nikuazia wachungaji mpaka waumini.. Kwanini
Kukosa misingi mizuri ya kuweka mipango imara yenye kudum ndani ya kanisa. Najua wengi mtanipinga lkn ukweli utabaki palepale..
Labda nani anaejua mchungaji wa Tag ana degree?
Nimeshuhudia darasa la saba mtu akikabidhiwa kanisa na mojakwamoja kuitwa mchungaji.
Kuongoza jamii pia kunahitaji Elim sio kitu rahisi sana.
Pengine tujifunze kitu.. Kutoka makanisa ya Romani catholic, pendecoste, kkkt,Sabato.. Hawa wengi wao viongozi wana uwezo kielim.. Ni degree, phd nk.misingi yao hudum.
Na hawayumbi nawala hawana papara.
Wewe utakuwa unaongelea TAG ya "Kolomije"!
Minimum qualification kwa wachungaji wa TAG ya leo ni Diploma ya miaka 3!
Zinduka usingizini...
 
Kwa ufahamu wangu haya makanisa ya TAG nguvu ilianza kupungua tangu kipindi kile cha KULOLA kuanzisha EAGT. Lakini wakajitahidi sana kukaa ktk mstari wa unyoofu hapa na maanisha kuhubiri na kuishi sawa sawa na NENO la Mungu yaani utakatifu. Kilichikuja kuharibu ni usasa hasa baada ya kuanza ile mikutano ya jagwani na kwingineko kwa kushirikiana na foreign ministries hasa za USA. Wale walipoingia wakaleta usasa taratibu wanawake wakaanza kuvaa suruali na kujiremba kanisani na kila aina ya mapambo. Hapa wakapunguza nguvh ya Mungu. Shetani akaanza kuingia taratibu ktk hayo makanisa uzinzi ktk kwaya ukawa kawaida...wachungaji kufumaniwa ikawa kawaida. Wakaibuka waimbaji binafsi ndani ya makanisa ikazidisha mgongano was kimaslai among singers. Mara wachungaji binafsi wakapata kibali kujenga makanisa yako lna kuyaendesha ilimradi tuu yako affiliated na TAG ie
mlima wa moto .
Tatizo likawa kubwa zaidi watu wakaanza kutafuta maslai na si injili tena. Ule umoto wao wa injili miaka ya 2000 kurudi nyuma umepotea kwa kazi lkubwa sana. Na sasa kuibuka kwa makanisa mengi ya kibinafsi yanayohubiri miujuza ujiza ya kitapeli mara maji chumvi mafuta ya upako sijui utapata gari nyumba mke mume utaenda ulaya yamekuwa changamoto kweli kwa TAG. TAG washajua ni wapi wamekosea ila wanaogopa gharama za kurudi ktk mstari wao kuhubiri utakatifu kwa wachungaji wavaa suruali wanawake au wanaume waziznzi ni gharama kubwa. Kuanza kuwaambia watu waache mapambo na vimini ibadani ni gharama kubwa sana kwao koz watakosa sadaka zao na kwenda kwingine. Hapa ndo ilitakiwa wampate anaza KULOLA kuwanyoisha siyo hiyo mijitu ina phd ya theolojia haina chchote. However wapo wachungaji ndan TAG kam KATUNZI anajua anafanya nini
Katunzi yupo EAGT
 
Siamini kama kazi ya kanisa ni kutafuta sifa na kujulikana hapana, kazi ya kanisa ni kufundisha kweli za Kimungu ili binadamu aokolewe mwili na roho. Kati ya kanisa maalufu sana duniani ni kanisa katoliki lakini hakuna wakati wowote lilipowahi kujitafuta kwa kutukana au kudhalilisha wengine. Hivyohivyo TAG huenda wameona mambo yameanza kwenda mlama miongoni mwao wakaamua wale waaminifu kufanya yawapasayo, kutokuwasikia mitaani sio kigezo cha kuwapima kwamba wako dhaifu au imara, kama wanafanya yale ya imani yao, let them keep it up.
 
Askofu wao mkuu ana PHD anaitwa Barnabas Mtokambali ingia google uwacheck hao watu.Pia wanachuo chao kinaitwa CENTRAL BIBLE COLLEGE kipo Dodoma kinatoa hadi level ya Masters elimu Bibilia na Theologia pia wanachuo kikubwa Lindi,Mbeya,Arusha na Mwanza na wanajenga kingine kikubwa pia Tabora na kingine kipo pale opposite na Blue Pearl Hotel Ubungo kinaitwa Global Harvest kinatoa hadi Masters pia wamejiafiliate na chuo kipo Marekani kinaitwa Globa University .No research no right to speak.
Hayo si mambo ya kujivunia kwa mujibu wa misingi ya imani yao.Ni mambo ya kawaida kuwa nayo kama zilivyo taasisi zingine za aina yake. Ishu hapa ni kupoa kiimani kuliko mwanzo.Huo ufahari ndiyo utazidi kuwapooza kiimani mpaka wawe sawa na waliowadharau kuwa hawana imani.Hivyo vitu si vya kiimani maana vinaonekana na vinajengwa
 
Kwa utafiti wangu wanawanashule tano za Sekondari ambazo ni Faraja,Siha,Ebeneza,nyingine ipo Singida ,nyingine ipo Sumbawanga.Pia wanachuo cha ualimu kipo Iringa Tanangozi.
Kwa upande wa Radio wanayo ipo jimbo la Mbeya mjini.
Hospitali wanayo katika chuo chao cha Dodoma na clinic ya kuzalishia wajawazito.
Mkuu hichi ndicho kilichowapooza kiimani.
 
Mimi sio muumini wa TAG lakini nina uhakika hilo dhehebu halijapoa. Nimeingia kwenye makanisa yao kadhaa Wapo very smart hata katika ibada zao and perhaps it is the most smart pentecostal church in Tanzania! Hata Askofu mkuu wao tu ni Msomi wa PHD (Sio kama ya huyu mtukufu) na hata wasaidizi wake ni vichwa. Kwa hiyo mkuu halijapoa hilo chechi labda kwa awamu hii tu kwa sababu tunapitia kwenye jaribu zito wa Tanzania wote hasa financially, na mheshimiwa alishasema akiwa Singida pale siku ya mwaka mpya kuwa sadaka zita adimika hata makanisani!!!!
Unaharufu ya kiitikadi huto weza kushawishi mtu kwa point..
 
Wachujgaji wa makanisa haya wengi ni wana usalama waliopenyezwa kwa sababu maalum,sio kumhubiri Yesu wa Nazareth,ndio maana unayaona yako mengi na wanaonyesha kila TV wakati waumini wao hata wengine hawafikishi 60

Wanachofanya ni kazi maalum ya kisaikolojia kuwaondoa wananchi kwenye hoja za kuihoji serikali kuhusu mambo ya uchumi,afya,elimu,na maendeleo kwa ujumla,na kuwaambia mambo yote na shida zao ni kazi ya mungu,hivyo waendelee kumuomba

Sehemu ngumu iliyowasumbua ni misikitini,lakini wamefanikiwa kuwakaba bakwata lakini bado usumbufu wa akina sheikh ponda na wengine upo,wao wanaita usumbufu
Hapa penyewe wamefanikiwa,ona sasa tunachojadili.
 
Mimi sio muumini wa TAG lakini nina uhakika hilo dhehebu halijapoa. Nimeingia kwenye makanisa yao kadhaa Wapo very smart hata katika ibada zao and perhaps it is the most smart pentecostal church in Tanzania! Hata Askofu mkuu wao tu ni Msomi wa PHD (Sio kama ya huyu mtukufu) na hata wasaidizi wake ni vichwa. Kwa hiyo mkuu halijapoa hilo chechi labda kwa awamu hii tu kwa sababu tunapitia kwenye jaribu zito wa Tanzania wote hasa financially, na mheshimiwa alishasema akiwa Singida pale siku ya mwaka mpya kuwa sadaka zita adimika hata makanisani!!!!
Bukoba sio Singinda Mkuu
 
TAG Haijapoa kama unavyo fikiria kila zama na ukurasa wake TAG bado wako vizuri kumbuka kila kitu hakijabadrika ila huwafuatilii labda
Hoja mbona iko wazi na inajibika? Ufahari ndiyo umewapooza hawaoni tena kiimani
 
Back
Top Bottom