Kanisa la TAG mbona kama limepoa?

Kanisa la TAG mbona kama limepoa?

Mimi sio muumini wa TAG lakini nina uhakika hilo dhehebu halijapoa. Nimeingia kwenye makanisa yao kadhaa Wapo very smart hata katika ibada zao and perhaps it is the most smart pentecostal church in Tanzania! Hata Askofu mkuu wao tu ni Msomi wa PHD (Sio kama ya huyu mtukufu) na hata wasaidizi wake ni vichwa. Kwa hiyo mkuu halijapoa hilo chechi labda kwa awamu hii tu kwa sababu tunapitia kwenye jaribu zito wa Tanzania wote hasa financially, na mheshimiwa alishasema akiwa Singida pale siku ya mwaka mpya kuwa sadaka zita adimika hata makanisani!!!!
Phd na injili ni vitu 2 tofauti kbsaaa
 
Sijui mtoa uzi anatumia kipimo gani na kuona kuwa kanisa la TAG limepoa. Hakuna hata kimoja kilichokuwepo miaka ya nyuma ambacho kimepotea au kupungua. Kinyume chake kila eneo la ukristo wa kweli limeonyesha kukua. Washirika wengi makanisani wameokoka na ndiyo sifa mama ya kuwa mshirika wa kanisa. Wengi zaidi wamejazwa na Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha kuliko zamani. Wahubiri leo ni wengi zaidi kuliko mwanzo ambapo ni wachache tu waliokuwa wanahubiri. Kuna wainilisti wa kitaifa wengi zaidi leo kuliko zamani. Miujiza kanisani ndio mahali pake na hufanyika kila ibada. Tatizo tu ni kwamba kanisa halina Tv yake, kwa hiyo yanayofanyika huko huwa hayafahamiki kwa kasi na watu walio nje. Wagonjwa bado wanaombewa na kupona na ni kitu cha kawaida sana. Kanisa limekua sana. Ila kama unahitaji kuona mbwembwe kama za "mitume na manabii" hapo utasubiri sana. Kanisa la TAG halifanyi huduma kama maonyesho, huduma hufanyika kwa staha ya hali ya juu na kuzingatia maadili kwa hali ya juu. Hutasikia habari ya mafuta ya upako, wala maji ya upako wala chochote kinachofanana na hayo. Ila NENO huhubiriwa na kufundishwa kikamilifu na Roho Mtakatifu hulithibitisha kwa ishara na miujiza. Karibu katika kanisa lolote la TAG kwa msaada na ushauri zaidi. Lakini mwisho, unatakiwa uokoke binafsi ili uwe tayari kumlaki Yesu mara arudipo mawinguni. Mungu akubariki, binafsi nimeokoka na ninampenda sana Yesu. Nimeamua kuachana na dhambi. Ya kale yamepita, tazama yote yamekuwa mapya. Na wewe unaweza kuachana na maisha ya dhambi na haujachelewa bado.
Barikiwa sana
 
bible inasema kwa kuongezeka maasi upendo wa Mungu upoa maana yake Mungu hayupo mahali penye uovu hivyo ubaki kama dini zingine kwa hiyo hakuna muujiza tena kama kuna maasi/dhambi iliyokithiri mpaka imekuwa ya kawaida leo waimbaji makanisani ni WCB
 
bible inasema kwa kuongezeka maasi upendo wa Mungu upoa maana yake Mungu hayupo mahali penye uovu hivyo ubaki kama dini zingine kwa hiyo hakuna muujiza tena kama kuna maasi/dhambi iliyokithiri mpaka imekuwa ya kawaida leo waimbaji makanisani ni WCB
Kuna siku niluhudhuria pale jangwani kwa mwakubirwa EAGT Aisee masanja anafanya mizaha mazabauni yaani wanapokezana microphone na yule Silas mbise kama washehreshaji ktk mziki duh acha kbsaaa
 
ulokole kiujumla umepungua nguvu sio kama ulivyoanza......!!yan uko makanisani wanachokifanya dah bora nijisalie nyumbani tu...!
 
Hilo kanisa kwa sasa limeingiliwa na wahuni wakina mzee wa bapa n wenzake. Wanaofanya miujiza ya kulipia, watu wanatoa sadaka kwa madaraja.
 
Bado TAG wapo vizuri mkuu,nadhani wabongo unawajua kwa kushobokea vipya na mda mfupi wanasahau......
Miaka ya nyuma hakukuwa na mabii/mitume wengi kama Leo,hawa jamaa wameiga vitu vingi kutoka Pentecostal churches,ingawa kuna vingine wamechakachua,
Nachowapendea TAG wanasimamia neno(bible)
Utandawazi na emerging ya kizazi cha vijana wa kisasa kanisani kunapunguza ule uamsho kama wa zamani.
Utajiri wa Wachungaji,now days Wachungaji wamekua matajili sana wa pesa,hiyo ile halo ya kutosheka imewakamata baadhi ya viongozi hata ile kasi ya kumtafuta Mungu imeshuka
N:B bado TAG ni moja ya dhehebu bora kwa makanisa ya kipetecost,
Hii imeshakuwa dini ndg yangu kama dini nyingine yyt unayoijua! Mahubiri yao makubwa now ni kuponda makanisa mengine ya kipentecoste na kusisitiza hakuna nabii wala mtume ila ni Yesu tuu! Sasa najiuliza can you make the entire TZ become TAG members??? Falsafa yao ya kujiona bora kuliko wapentecoste wengine ndio kichefuchefu kikubwa haijalishi kuongezeka kiidadi mbona roman wako dunia nzima issue ni what au doing!
 
Ni kwanini makanisa ya Kipentekoste hayatangazi mapato yao hasa sadaka?
 
Back
Top Bottom