Kanisa la TAG mbona kama limepoa?

Kanisa la TAG mbona kama limepoa?

Habari za muda huu waungwana?
Natumai mnaendelea vizuri hasa baada ya mihangaiko ya siku.

Niende moja kwa moja kwenye mada niliyokusudia kuianzisha leo.

Kwa wale wakristo mtakua mpo aware zaidi kuhusu ukristo ulivyo na ulivyo hapa nchini.

Miaka ya nyuma kidogo ukristo ulikua imeenea zaidi kwa makanisa ya Romani Catholic, Lutheran na Pentecoste. Miaka ilivyokwenda zaidi ndipo tulipo shuhudia idadi kubwa ya makanisa hapa nchini.

Nakumbuka miaka ya 2000 kanisa la TAG lilianza kuja kwa kasi sana. Kufikia miaka ya '03-0'5 walikua wanasikika sana kutokana na makongamano makubwa na mahubiri yao.
Hawa watu walikua wanaponda sana makanisa mengine hususan wakatoliki.Hapa ndipo walipopata waumini wengi kutoka makanisa kongwe niliyotaja hapo juu kutokana na miujiza waliyokua wanafanya makanisani mwao kama kutoa pepo na kuombea wagonjwa just little to mention.

Walikua kwa kasi sana na hapa matajiri wengi pia walihamia huko wakajenga makanisa nchi nzima na kukua kwa kasi kutokana na styl yao mpya ya kuabudu na mahubiri.

Ilikua changamoto sana kuoa binti wa kilokole enzi hizo.Ilifika mahali mtu akitoka katoliki,lutheran au pentecoste akajiunga TAG alikua anatengwa na familia na ndugu na aliitwa muasi.Ikafika mahali kukawa na kama ka uadui fulani kati madhehebu hayo.
Enzi hizo karibu kila mlokole alikua anaweza kutoa pepo na kuongea zile lugha zao.

Miaka ilivyo anza kwenda sasa;taratiiibu ile power yao ya ku preach na kufanya miujiza ikaanza kupotea na kufifia.
Hivi sasa wameshazoeleka na wapo very normal sana.
Hivi sasa wana intergrate na wakristo wengine vizuri sana tofauti na zamani.

Maswali yangu:

1:Kwanini TAG wamepoa sana na hawapo hot kama zamani?
2:Je mi kwa sababu waumini wamesha jaa hivyo basi hawana nia ya ku expand zaidi?
3:Au ni utandawazi unachangia?

Karibuni kwa mawazo
Ukitaka kufika mbinguni hamia TAG wapo vizur sana chini ya Dr mtokambali, uzuri wa kanisa hili halifungamani na siasa kabsa, miaka kumi ya mavuno Tanzania kwa Yesu
 
Jamani vipi kanisa la CCF lililokuwa na makao makuu yao pale sinza kumekucha mbona halisikiki tena,walikuwa wanandaa mkesha mkubwa pale uwanja wa taifa anayejua habari yake atujuze plz.
 
Habari za muda huu waungwana?
Natumai mnaendelea vizuri hasa baada ya mihangaiko ya siku.

Niende moja kwa moja kwenye mada niliyokusudia kuianzisha leo.

Kwa wale wakristo mtakua mpo aware zaidi kuhusu ukristo ulivyo na ulivyo hapa nchini.

Miaka ya nyuma kidogo ukristo ulikua imeenea zaidi kwa makanisa ya Romani Catholic, Lutheran na Pentecoste. Miaka ilivyokwenda zaidi ndipo tulipo shuhudia idadi kubwa ya makanisa hapa nchini.

Nakumbuka miaka ya 2000 kanisa la TAG lilianza kuja kwa kasi sana. Kufikia miaka ya '03-0'5 walikua wanasikika sana kutokana na makongamano makubwa na mahubiri yao.
Hawa watu walikua wanaponda sana makanisa mengine hususan wakatoliki.Hapa ndipo walipopata waumini wengi kutoka makanisa kongwe niliyotaja hapo juu kutokana na miujiza waliyokua wanafanya makanisani mwao kama kutoa pepo na kuombea wagonjwa just little to mention.

Walikua kwa kasi sana na hapa matajiri wengi pia walihamia huko wakajenga makanisa nchi nzima na kukua kwa kasi kutokana na styl yao mpya ya kuabudu na mahubiri.

Ilikua changamoto sana kuoa binti wa kilokole enzi hizo.Ilifika mahali mtu akitoka katoliki,lutheran au pentecoste akajiunga TAG alikua anatengwa na familia na ndugu na aliitwa muasi.Ikafika mahali kukawa na kama ka uadui fulani kati madhehebu hayo.
Enzi hizo karibu kila mlokole alikua anaweza kutoa pepo na kuongea zile lugha zao.

Miaka ilivyo anza kwenda sasa;taratiiibu ile power yao ya ku preach na kufanya miujiza ikaanza kupotea na kufifia.
Hivi sasa wameshazoeleka na wapo very normal sana.
Hivi sasa wana intergrate na wakristo wengine vizuri sana tofauti na zamani.

Maswali yangu:

1:Kwanini TAG wamepoa sana na hawapo hot kama zamani?
2:Je mi kwa sababu waumini wamesha jaa hivyo basi hawana nia ya ku expand zaidi?
3:Au ni utandawazi unachangia?

Karibuni kwa mawazo
mija kati y a ujinga wenye msaada alionifundisha mchungaji wangu wa TAG ni kuwa nisipende kujibu hoja ambayo iandhamiria kulikebehi kanisa na wala sio kufikia muafaka wa muulizaji kupata uelewa.
 
Vp na haya makanisa yanayovuma kwa jina la mtu mmoja mmoja kwa mfano Lusekelo au Malisa, hayo makanisa yako chini ya mwamvuli gani? Wajuvi ufafanuzi tafadhali
 
Kwanza nikupongeze kwa kuileta mada hii hata hivyo niseme tu kwamba wewe hauabudu huko TAG hivyo basi hata ufahamu wako kuhusu TAG inavyojiendesha si mpana kivile. Niseme tu kwamba TAG ilianza kuyumba wakati ule wa mgogoro kati ya Askofu Lazaro na Mwinjilisti Moses kulola (Hayati) ambao hatimaye uliamuliwa na mahakama na kufanya TAG igawanyike kuzaa EAGT iliyokuwa chini ya Moses kulola. Kwa bahati mbaya sana TAG wameendeleza na ule ugomvi hadi leo kwa kuendelea kuwaita EAGT waasi (Roho mtakatifu hawezi kufanya kazi mahali pasipo na msamaha wa kweli). Jambo moja lipo wazi kwamba TAG wamekosa mbadala wa Moses kulola wa kusimamia ile idara ya uinjilisti kitaifa ingawa baadhi ya nyakati wamekuwa wakifanya kazi na Egon Folk na kumwalika Rev Reinhard Bonkey na Daniel Kolenda (wa Christ for all Nations) mwaka jana. Nadhani pia pia uendeshwaji wa TAG (Central Administration) ni changamoto ambapo kama sikosei watumishi/huduma wanawezeshwa kimaisha na Headquarter bila kujali idadi ya washirika mtumishi anaosimamia LAKINI pia Wachungaji wengi umri umesogea sana na hivyo kushindwa kuendana (Mahubiri + Ushuhudiaji) na hali ya kizazi cha sasa.

NB: Nipo tayari kukosolewa

Habari za muda huu waungwana?
Natumai mnaendelea vizuri hasa baada ya mihangaiko ya siku.

Niende moja kwa moja kwenye mada niliyokusudia kuianzisha leo.

Kwa wale wakristo mtakua mpo aware zaidi kuhusu ukristo ulivyo na ulivyo hapa nchini.

Miaka ya nyuma kidogo ukristo ulikua imeenea zaidi kwa makanisa ya Romani Catholic, Lutheran na Pentecoste. Miaka ilivyokwenda zaidi ndipo tulipo shuhudia idadi kubwa ya makanisa hapa nchini.

Nakumbuka miaka ya 2000 kanisa la TAG lilianza kuja kwa kasi sana. Kufikia miaka ya '03-0'5 walikua wanasikika sana kutokana na makongamano makubwa na mahubiri yao.
Hawa watu walikua wanaponda sana makanisa mengine hususan wakatoliki.Hapa ndipo walipopata waumini wengi kutoka makanisa kongwe niliyotaja hapo juu kutokana na miujiza waliyokua wanafanya makanisani mwao kama kutoa pepo na kuombea wagonjwa just little to mention.

Walikua kwa kasi sana na hapa matajiri wengi pia walihamia huko wakajenga makanisa nchi nzima na kukua kwa kasi kutokana na styl yao mpya ya kuabudu na mahubiri.

Ilikua changamoto sana kuoa binti wa kilokole enzi hizo.Ilifika mahali mtu akitoka katoliki,lutheran au pentecoste akajiunga TAG alikua anatengwa na familia na ndugu na aliitwa muasi.Ikafika mahali kukawa na kama ka uadui fulani kati madhehebu hayo.
Enzi hizo karibu kila mlokole alikua anaweza kutoa pepo na kuongea zile lugha zao.

Miaka ilivyo anza kwenda sasa;taratiiibu ile power yao ya ku preach na kufanya miujiza ikaanza kupotea na kufifia.
Hivi sasa wameshazoeleka na wapo very normal sana.
Hivi sasa wana intergrate na wakristo wengine vizuri sana tofauti na zamani.

Maswali yangu:

1:Kwanini TAG wamepoa sana na hawapo hot kama zamani?
2:Je mi kwa sababu waumini wamesha jaa hivyo basi hawana nia ya ku expand zaidi?
3:Au ni utandawazi unachangia?

Karibuni kwa mawazo
 
Point of correction (in green): Katunzi yuko EAGT siyo TAG! Mengine uliyoandika kwa kiwango kikubwa kuna ukweli fulani.
In red: Wachungaji wanaoanzisha makanisa kwa jina la TAG imepelekea makanisa hayo kuwa mali ya familia. Mwongozo au katiba ya TAG haifuatwi katika makanisa hayo. Idara ndani ya kanisa licha ya kuwa na uongozi, viongozi wa idara hawana mandate ya kuamua chochote pasipo mchungaji au mke wake kuridhia hata kama uamuzi wao uko ndani ya mipaka ya miongozo iliyoainishwa na TAG. Baraza la wazee limewekwa kama rubber stamp kupitisha mawazo ya mchungaji. Wazee wa kanisa ambao ni "ndiyo baba/mama mchungaji" yaani wasiopinga chochote hukumbatiwa sana. Mke wa mchungaji ambaye kimsingi siyo mmoja wa baraza la wazee huwa kiongozi wa baraza iwapo mume wake hayupo. Mke wa mchungaji huvuruga sana kanisa hasa kutokana na "sense of insecurity". Mama mchungaji huingilia kila kitu ili aonekane na kutambuliwa. Hiyo ni kwa sababu organization chart ya TAG kiuongozi haioneshi nafasi ya mke wa mchungaji, kwa hiyo lazima ajitutumue kuonesha kwamba yupo na ana nguvu.
Pia siku hizi hukumbatia idadi ya waumini (quantity) pasipo kusimamia maadili ya kiroho (spiritual quality)!
Asante kwa correction nimekumbuka ndo maana KATUNZI alikuwa msimamizi wa mali za KULOLA.
 
Cha ajabu wazee hao wa TAG wapo na wanaona huu upupu unaotokea ktk makanisa yao. Long ago it was hard mtu kuingia tuu kanisani TAG akiwa na kwa mwanamke au nguo za kubana those were the days siku lakini siku hizi duhh....wanagombania tuu uongozi na mapato
 
Nimejifunza mengi kwa kweli
Kumbe kuanzisha threads/mijadala humu kunasababisha mtu kupata material knowledge kwa kweli.

Bado naendelea kujifunza.

Wenye material leteni jamani
 
Kwanza nikupongeze kwa kuileta mada hii hata hivyo niseme tu kwamba wewe hauabudu huko TAG hivyo basi hata ufahamu wako kuhusu TAG inavyojiendesha si mpana kivile. Niseme tu kwamba TAG ilianza kuyumba wakati ule wa mgogoro kati ya Askofu Lazaro na Mwinjilisti Moses kulola (Hayati) ambao hatimaye uliamuliwa na mahakama na kufanya TAG igawanyike kuzaa EAGT iliyokuwa chini ya Moses kulola. Kwa bahati mbaya sana TAG wameendeleza na ule ugomvi hadi leo kwa kuendelea kuwaita EAGT waasi (Roho mtakatifu hawezi kufanya kazi mahali pasipo na msamaha wa kweli). Jambo moja lipo wazi kwamba TAG wamekosa mbadala wa Moses kulola wa kusimamia ile idara ya uinjilisti kitaifa ingawa baadhi ya nyakati wamekuwa wakifanya kazi na Egon Folk na kumwalika Rev Reinhard Bonkey na Daniel Kolenda (wa Christ for all Nations) mwaka jana. Nadhani pia pia uendeshwaji wa TAG (Central Administration) ni changamoto ambapo kama sikosei watumishi/huduma wanawezeshwa kimaisha na Headquarter bila kujali idadi ya washirika mtumishi anaosimamia LAKINI pia Wachungaji wengi umri umesogea sana na hivyo kushindwa kuendana (Mahubiri + Ushuhudiaji) na hali ya kizazi cha sasa.

NB: Nipo tayari kukosolewa
nashukuru kiongozi.
Mimi siabudu TAG ila nime observe experience yangu huku mtaani mkuu.

Hili kanisa enzi zake wakipiga bible walikua wana hit sana na kweli walivuna watu wa maana ila sasa ndo hivo wamepoa
 
Yalikuwa makanisa ya mpito tu, na Hiyo TAG itafutika au kuisha kabisa, yatabaki Makanisa ya Wachungaji tu, nayo yatafutika pale mwenye Kanisa akifa
Luther umeniasi nawe watakuasi
Hivi haya maneno hayakuwahi kutamkika eti!?
 
Kila zama na kusudi lake yamkini Mungu aliwakabidhi jukumu la kueneza injili wakati ule
 
Wachujgaji wa makanisa haya wengi ni wana usalama waliopenyezwa kwa sababu maalum,sio kumhubiri Yesu wa Nazareth,ndio maana unayaona yako mengi na wanaonyesha kila TV wakati waumini wao hata wengine hawafikishi 60

Wanachofanya ni kazi maalum ya kisaikolojia kuwaondoa wananchi kwenye hoja za kuihoji serikali kuhusu mambo ya uchumi,afya,elimu,na maendeleo kwa ujumla,na kuwaambia mambo yote na shida zao ni kazi ya mungu,hivyo waendelee kumuomba

Sehemu ngumu iliyowasumbua ni misikitini,lakini wamefanikiwa kuwakaba bakwata lakini bado usumbufu wa akina sheikh ponda na wengine upo,wao wanaita usumbufu
Ni km nashawishika kukuamini
 
Kwa ufahamu wangu haya makanisa ya TAG nguvu ilianza kupungua tangu kipindi kile cha KULOLA kuanzisha EAGT. Lakini wakajitahidi sana kukaa ktk mstari wa unyoofu hapa na maanisha kuhubiri na kuishi sawa sawa na NENO la Mungu yaani utakatifu. Kilichikuja kuharibu ni usasa hasa baada ya kuanza ile mikutano ya jagwani na kwingineko kwa kushirikiana na foreign ministries hasa za USA. Wale walipoingia wakaleta usasa taratibu wanawake wakaanza kuvaa suruali na kujiremba kanisani na kila aina ya mapambo. Hapa wakapunguza nguvh ya Mungu. Shetani akaanza kuingia taratibu ktk hayo makanisa uzinzi ktk kwaya ukawa kawaida...wachungaji kufumaniwa ikawa kawaida. Wakaibuka waimbaji binafsi ndani ya makanisa ikazidisha mgongano was kimaslai among singers. Mara wachungaji binafsi wakapata kibali kujenga makanisa yako lna kuyaendesha ilimradi tuu yako affiliated na TAG ie
mlima wa moto .
Tatizo likawa kubwa zaidi watu wakaanza kutafuta maslai na si injili tena. Ule umoto wao wa injili miaka ya 2000 kurudi nyuma umepotea kwa kazi lkubwa sana. Na sasa kuibuka kwa makanisa mengi ya kibinafsi yanayohubiri miujuza ujiza ya kitapeli mara maji chumvi mafuta ya upako sijui utapata gari nyumba mke mume utaenda ulaya yamekuwa changamoto kweli kwa TAG. TAG washajua ni wapi wamekosea ila wanaogopa gharama za kurudi ktk mstari wao kuhubiri utakatifu kwa wachungaji wavaa suruali wanawake au wanaume waziznzi ni gharama kubwa. Kuanza kuwaambia watu waache mapambo na vimini ibadani ni gharama kubwa sana kwao koz watakosa sadaka zao na kwenda kwingine. Hapa ndo ilitakiwa wampate anaza KULOLA kuwanyoisha siyo hiyo mijitu ina phd ya theolojia haina chchote. However wapo wachungaji ndan TAG kam KATUNZI anajua anafanya nini
Siyo makanisa
Ni madhebu,
Kanisa lipo moja na staki maswali maana hayatabadili ukweli huu
 
TAG ilikuwa na nguvu tangu 19970's mpaka miaka ya kati ya 1980. Waliposhindwa kusolve tatizo mpaka ikapelekea kanisa kupasuka na ikazaliwa EAGT mwaka 1989....likawa anguko la TAG. Limebaki kanisa la wachungaji kushinda kusoma falsafa za dini yao ya assemblies tu na kupelekana marekani kusoma. Kuhubiri injili si issue tena kwao.....Hiyo miaka ya 2000 unayoisema sijui ni TAG gani unayoizungumzia.
 
Wachujgaji wa makanisa haya wengi ni wana usalama waliopenyezwa kwa sababu maalum,sio kumhubiri Yesu wa Nazareth,ndio maana unayaona yako mengi na wanaonyesha kila TV wakati waumini wao hata wengine hawafikishi 60

Wanachofanya ni kazi maalum ya kisaikolojia kuwaondoa wananchi kwenye hoja za kuihoji serikali kuhusu mambo ya uchumi,afya,elimu,na maendeleo kwa ujumla,na kuwaambia mambo yote na shida zao ni kazi ya mungu,hivyo waendelee kumuomba

Sehemu ngumu iliyowasumbua ni misikitini,lakini wamefanikiwa kuwakaba bakwata lakini bado usumbufu wa akina sheikh ponda na wengine upo,wao wanaita usumbufu

Ngoja niwahi mkesha mimi....
 
Ubaguzi ni kitu kibaya sana. TAG wanaona wao tu ndio wenye tiketi ya Mbinguni. Wameshindwa kusimamisha makanisa vijijini. Makanisa yao yako mjini. Yaani ukiwa na pesa pale TAG utaheshimika sana na pastor atakuombea kweli,maskini TAG si kwao maana huishia kudharauliwa. Mahubiri yao ni kutoa fungu la kumi tu. Hii imepelekea kutohubiri watu kuacha dhambi. Cha ajabu kabisa,mashemasi na wazee wa kanisa ni wakorofi balaa. Ukienda kusali utasukumwasukumwa kama nini. TAG labda watubu kwanza ndio watarudi kwenye mstari.
 
Back
Top Bottom