Kanisa la TAG mbona kama limepoa?

Kanisa la TAG mbona kama limepoa?

Bado TAG wapo vizuri mkuu,nadhani wabongo unawajua kwa kushobokea vipya na mda mfupi wanasahau......
Miaka ya nyuma hakukuwa na mabii/mitume wengi kama Leo,hawa jamaa wameiga vitu vingi kutoka Pentecostal churches,ingawa kuna vingine wamechakachua,
Nachowapendea TAG wanasimamia neno(bible)
Utandawazi na emerging ya kizazi cha vijana wa kisasa kanisani kunapunguza ule uamsho kama wa zamani.
Utajiri wa Wachungaji,now days Wachungaji wamekua matajili sana wa pesa,hiyo ile halo ya kutosheka imewakamata baadhi ya viongozi hata ile kasi ya kumtafuta Mungu imeshuka
N:B bado TAG ni moja ya dhehebu bora kwa makanisa ya kipetecost,
Usisahau FPCT hawa wameenea kila mkoa wapo?
 
Yalikuwa makanisa ya mpito tu, na Hiyo TAG itafutika au kuisha kabisa, yatabaki Makanisa ya Wachungaji tu, nayo yatafutika pale mwenye Kanisa akifa
mambo yote yatapita lakini neno la Mungu halitapita
 
Tanzania Assemblies of God-T.A.G is even stronger than before:
1.Imekuwa na matawi nchi nzima, kila wilaya, kila kata.
2. T.A.G is the strongest Pentecostal denomination in the country. Askofu mkuu wa T.A.G ndiye Rais wa makanisa yote ya ki Assemblies ya Africa.
3.Ndiyo dhehebu pekee la kipentecost nchini lenye vyuo vya Biblia vinavyotoa diploma, degree hadi masters kwa kushirikiana na Global University ya USA
3.Ni dhehebu la kipentecost pekee nchini linalopeleka wamisionari nje ya Tanzania kama Rwanda, Burundi, Sudan kusini, DRC, na Magasca.
4.Linahubiri injili nchini kwa kasi zaidi kuliko huko nyuma.

Ukiangalia takwimu ya Nini T.A.G ilifanya huko nyuma na nini inafanya kwa sasa, na Neno linataka kanisa liweje utagundua kuwa ndiyo lina peak kwa viwango vikubwa.
Vipi kuhusu ujenzi wa majengo ya kuabudia,ilikuaje TAG wajengewe majengo ya kuabudia nchi nzima hususani vijijini tena kwa ramani moja wakati inasemekana huo msaada ulikuwa ni kwa makanisa yote ya kipentekoste Tanzania? Wadadisi wa mambo wakasema walipigwa changa la macho na mjanja mmoja wa huko TAG msaada ukaishia huko kwa kuwa ni yeye ndiye aliyeongea na msamaria wa nje kuja kujenga makanisa ya kipentekoste kumbe ni TAG peke yake!
 
Hahahahahaaa humjui nabii malisa wewe
Yule jamaa anaenda kuchomeka vibaya sana kama huko tuendako kukawa na hukumu...mzee wa "toa sadaka kwa namba za simu zinazopita kwenye kioo chako cha Tv kisha nitaziombea zirudi kwako maradufu kwa njia ya Mpesa TigoPesa na Airtel money".hahahah watu nao wanaitikia aaamen.yaani badala awahamasishe watu wakatafute ridhki zao kwa kufanya kazi anawaaminisha eti watoe aziombee zirudi kwao!
 
Yalikuwa makanisa ya mpito tu, na Hiyo TAG itafutika au kuisha kabisa, yatabaki Makanisa ya Wachungaji tu, nayo yatafutika pale mwenye Kanisa akifa
Rekebisha kauli yako. TAG sio kanisa la mpito. Na halitakaa likafutika.
 
Wachujgaji wa makanisa haya wengi ni wana usalama waliopenyezwa kwa sababu maalum,sio kumhubiri Yesu wa Nazareth,ndio maana unayaona yako mengi na wanaonyesha kila TV wakati waumini wao hata wengine hawafikishi 60

Wanachofanya ni kazi maalum ya kisaikolojia kuwaondoa wananchi kwenye hoja za kuihoji serikali kuhusu mambo ya uchumi,afya,elimu,na maendeleo kwa ujumla,na kuwaambia mambo yote na shida zao ni kazi ya mungu,hivyo waendelee kumuomba

Sehemu ngumu iliyowasumbua ni misikitini,lakini wamefanikiwa kuwakaba bakwata lakini bado usumbufu wa akina sheikh ponda na wengine upo,wao wanaita usumbufu
nitajuaje mchungaji ni mwanausalama
 
Sijui mtoa uzi anatumia kipimo gani na kuona kuwa kanisa la TAG limepoa. Hakuna hata kimoja kilichokuwepo miaka ya nyuma ambacho kimepotea au kupungua. Kinyume chake kila eneo la ukristo wa kweli limeonyesha kukua. Washirika wengi makanisani wameokoka na ndiyo sifa mama ya kuwa mshirika wa kanisa. Wengi zaidi wamejazwa na Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha kuliko zamani. Wahubiri leo ni wengi zaidi kuliko mwanzo ambapo ni wachache tu waliokuwa wanahubiri. Kuna wainilisti wa kitaifa wengi zaidi leo kuliko zamani. Miujiza kanisani ndio mahali pake na hufanyika kila ibada. Tatizo tu ni kwamba kanisa halina Tv yake, kwa hiyo yanayofanyika huko huwa hayafahamiki kwa kasi na watu walio nje. Wagonjwa bado wanaombewa na kupona na ni kitu cha kawaida sana. Kanisa limekua sana. Ila kama unahitaji kuona mbwembwe kama za "mitume na manabii" hapo utasubiri sana. Kanisa la TAG halifanyi huduma kama maonyesho, huduma hufanyika kwa staha ya hali ya juu na kuzingatia maadili kwa hali ya juu. Hutasikia habari ya mafuta ya upako, wala maji ya upako wala chochote kinachofanana na hayo. Ila NENO huhubiriwa na kufundishwa kikamilifu na Roho Mtakatifu hulithibitisha kwa ishara na miujiza. Karibu katika kanisa lolote la TAG kwa msaada na ushauri zaidi. Lakini mwisho, unatakiwa uokoke binafsi ili uwe tayari kumlaki Yesu mara arudipo mawinguni. Mungu akubariki, binafsi nimeokoka na ninampenda sana Yesu. Nimeamua kuachana na dhambi. Ya kale yamepita, tazama yote yamekuwa mapya. Na wewe unaweza kuachana na maisha ya dhambi na haujachelewa bado.
Asante kwa mchango wa maoni ila umeongea kiujumla sana. Hata usiende mbali kama wewe si mchungaji basi mwulize mch. wako a rate nafasi ya TAG kwa sasa atakuambia

Ni kweli hatuna tofauti na Wakatoliki au waruthel kiroho
 
Ya kale..""" ? Kale ya muda gani...??? Makanisa ya Kipentekoste yote ni juzi juzi tuu....Ni makanisa ambayo hayana msingi....akifa mchungaji na kanisa linaporomoka
kanisa halifi wewe! we unatazama taasisi na NGOs? Kanisa ladumu mpaka unyakuo
 
Kwanza nikutulize, Je wewe ni mshirika wa kanisa la TAG? Kama ndio, umefanya nini kulisaidia kanisa lisipoe? Au unafikiri hiyo ni kazi ya wachungaji na maaskofu peke yao?
Kama wewe sio mshirika (mtazamaji), unangoja nini kuokoka? Unapata wapi ujasiri wa kulikosoa kanisa ikiwa wewe sio mshirika na wala huhusika?
acha unamba jibu hoja
 
KWELI KANISA HILI LIMEPOA SAAANA SABABU 1. WACHUNGAJI WAMEKUWA NA TAMAA YA KUPENDA PESA KULIKO MAELEZO, WACHUNGAJI WA KANISA LA T.A.G WANASHINDANA KWA MAISHA YA ANASA NA KUWALAZIMISHA WAUMINI WAO WAWACHANGIE PESA WANUNUE MAGARI MAZURI. MFANO KUNA KANISA LIKO MOSHI- SOWETO NI LA T.A.G LIMELAZIMISHA KILA MUUMMINI ATOE LAKI MOJA NA ZAIDI ILI KUMNUNULIA MCHUNGAJI GARI BILA KUJALI UWEZO WA KIUCHUMI WA WAUMINI WAO 2. UBAGUZI NDANI YA KANISA UMEKUWA MKUBWA SANA, WENYE PESA WANAPEWA KIPAUMBELE MASKINI HAWATHAMINIWI 3. UKABILA 4. VYEO VYA UPENDELEO NDANI YA KANISA 5. RUSHWA KATIKA CHAGUZI ZA MAASKOFU, MFANO UCHAGUZI UKIKARIBIA HUWA MAASKOFU WANATOA PIKIPIKI NA MAGARI KWA WACHUNGAJI NA WAANGALIZI, UCHAGUZI UKIISHA TU HAWAGAWI TENA. 6. KUKOSA KANISA KUBWA HALINA TV WALA REDIO ILA VIJANA WADOGO TU KINA MWAMPOSA/BULDOZA WANA REDIO NA TV. 7. KUTOTOA HUDUMA ZA KIJAMII, KANISA LINA MATAWI NCHI NZIMA ILA HALINA HATA HOSPITALI..WANA SHULE MBILI ZA SEKONDARI NAZO ZINZ MIUNDMBINU MIBOVU KULILKO HATA SHULE ZA KATA.8. KUKOSA UPENDO MIONGONI MWA WACHUNGAJI WAO KWA WAO, WACHUNGAJI WA MAKANISA YA MIJINI WANAISHI MAISHA YA HALI YA JUU SANA ILA WENZAO WA VIJIJINI WANA HALI MBAYA SANA NA WALA HAWASAIDIANI 9.TABIA YA KURITHISHANA MAKANISA KIUKOO NA KINDUGU MFANO BABA AKIZEEKA ANAMUACHIA MDOGO WAKE AU MTOTO WAKE HILI NALO NI TATIZO KUBWA MFANO CALVARY TEMPLE ARUSHA(T.A.G)
Mkuu umemaliza
Ubarikiwe sana
Kama upo moshi mkuu tutafutane.
 
Kwa ufahamu wangu haya makanisa ya TAG nguvu ilianza kupungua tangu kipindi kile cha KULOLA kuanzisha EAGT. Lakini wakajitahidi sana kukaa ktk mstari wa unyoofu hapa na maanisha kuhubiri na kuishi sawa sawa na NENO la Mungu yaani utakatifu. Kilichikuja kuharibu ni usasa hasa baada ya kuanza ile mikutano ya jagwani na kwingineko kwa kushirikiana na foreign ministries hasa za USA. Wale walipoingia wakaleta usasa taratibu wanawake wakaanza kuvaa suruali na kujiremba kanisani na kila aina ya mapambo. Hapa wakapunguza nguvh ya Mungu. Shetani akaanza kuingia taratibu ktk hayo makanisa uzinzi ktk kwaya ukawa kawaida...wachungaji kufumaniwa ikawa kawaida. Wakaibuka waimbaji binafsi ndani ya makanisa ikazidisha mgongano was kimaslai among singers. Mara wachungaji binafsi wakapata kibali kujenga makanisa yako lna kuyaendesha ilimradi tuu yako affiliated na TAG ie
mlima wa moto .
Tatizo likawa kubwa zaidi watu wakaanza kutafuta maslai na si injili tena. Ule umoto wao wa injili miaka ya 2000 kurudi nyuma umepotea kwa kazi lkubwa sana. Na sasa kuibuka kwa makanisa mengi ya kibinafsi yanayohubiri miujuza ujiza ya kitapeli mara maji chumvi mafuta ya upako sijui utapata gari nyumba mke mume utaenda ulaya yamekuwa changamoto kweli kwa TAG. TAG washajua ni wapi wamekosea ila wanaogopa gharama za kurudi ktk mstari wao kuhubiri utakatifu kwa wachungaji wavaa suruali wanawake au wanaume waziznzi ni gharama kubwa. Kuanza kuwaambia watu waache mapambo na vimini ibadani ni gharama kubwa sana kwao koz watakosa sadaka zao na kwenda kwingine. Hapa ndo ilitakiwa wampate anaza KULOLA kuwanyoisha siyo hiyo mijitu ina phd ya theolojia haina chchote. However wapo wachungaji ndan TAG kam KATUNZI anajua anafanya nini
katunzi yuko EAGT
 
Haya mambo ni mpaka FPCT. Akina mama na mabinti ni full kujiremba vitambaa tupa kule,vijana ni viduku na vijinsi vya kubana.Mabinti na vijana hakuna kuogopana ni stori mbovu kwa kwenda mbele Uchumba haueshimiwi, ndoa zinafungwa tayari zina kitu na box
 
Back
Top Bottom